Wabunge wa Tanzania waanza kutumia Tablet, je zina manufaa gani?

Wabunge walikabidhiwa vifaa hivyo Jumatatu kabla ya kuanza kwa vikao Jumanne mchana

Chanzo cha picha, Bunge la Tanzania /Twitter

Maelezo ya picha, Wabunge walikabidhiwa vifaa hivyo Jumatatu kabla ya kuanza kwa vikao Jumanne mchana
Muda wa kusoma: Dakika 2

Wabunge nchini Tanzania wataanza kutumia tablet kwa ajili ya kazi za bunge, huku bunge hilo likiondokana na matumizi ya karatasi.

Wabunge walikabidhiwa vifaa hivyo Jumatatu kabla ya kuanza kwa vikao Jumanne mchana katika mji mkuu wa nchi hiyo Dodoma.

Unaweza pia kusoma;

Katika akaunti ya rasmi ya Twitter ya bunge zilitumwa picha za wabunge wakipokea Tablet na ujumbe uliosema wanalenga kuachana na matumizi ya karatasi :

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Katibu wa Bunge Stephen Kigaigai alisema kuwa hatua hiyo itasaidia kuhifadhi pesa ambazo serikali imekuwa ikizitumia kuchapisha na kunakili nyaraka za serikali.

" Hata hivyo tumeziomba wizara husika kuja na baadhi ya nyaraka kwa ajili ya kuweka rekodi yake. Kwa mfano kwa matumizi katika maktaba," alisema.

Bwana Kigaigai anasema imekuwa ikichapisha nakala 500 za nyaraka za kutumiwa katika shughuli za bunge kwa siku lakini kwa sasa zitakuwa chini ya nakala 10.

Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa wabunge wote leo wameingia bungeni na Tablet.

Kuanzia sasa huenda ikawa nadra kumuona Spika Ndugai akishika karatasi, baada ya Bunge kuanza kutumia tablet

Chanzo cha picha, Bunge la Tanzania

Maelezo ya picha, Kuanzia sasa huenda ikawa nadra kumuona Spika Ndugai akishika karatasi, baada ya Bunge kuanza kutumia tablet

Spika wa bunge hilo Job Ndugai amezitaka taasisi nyingine nchini Tanzania kuiga mfano wa bunge kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili kupunguza matumizi ya karatasi.

Anatarajia hatua hiyo itasaidia kupunguza gharama ya kuchapisha kutoka shilingi bilioni 1.2 sawa na $519,000 hadi shilingi milioni 200.

Bunge limenunua takriban tableti 450 zenye thamani ya shilingi milioni 900 sawa na $389,000.

Unaweza pia kusoma:

Baadhi ya Watanzania wameelezea hisia zao kupitia mitandao ya kijamii juu ya hatua ya bunge kuanza kutumia Tablet:

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Ruka X ujumbe, 3

Mwisho wa X ujumbe, 3

Ruka X ujumbe, 4

Mwisho wa X ujumbe, 4

Ruka X ujumbe, 5

Mwisho wa X ujumbe, 5

Bunge la Tanzania limekuwa ni bunge la hivi karibuni miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki kutumia teknolojia katika kuimarisha utendaji wa haraka na kupunguza matumizi.

Katika nchi jirani ya Kenya wabunge walipewa iPad mapema mwaka huu katika hatua iliyotarajiwa kunusuru shilingi milioni 15 sawa na dola $150,000 ambazo zimekuwa zikitumiwa kuchapisha nakala za shughuli za bunge.

Uganda ilitoa iPad kwa wabunge nchini humo mwaka 2013.