Mmiliki wa Twitter kusitisha matangazo ya kisiasa

Mmiliki wa Twitter, bwana Dorsey

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mmiliki wa Twitter, bwana Dorsey

Wiki hii, mmiliki wa Twitter Jack Dorsey alisema kuwa nguvu ya mitandao ya kijamii sio kuleta mijadala mikali inayoweza kubadili mtazamo wa uchaguzi na kuahidi kuwa atasitisha matangazo yote ya kisiasa katika mtandao wake.

Bado wanatazamia kama mtandao wa Facebook utalazimishwa kufanya hivyohivyo.

Bwana Dorsey kuingilia kati namna watu wanavyowasiliana katika twitter.

Maamuzi yake yamekuja saa chache kabla mmiliki wa Facebook's Mark Zuckerberg kuzungumzia suala la mafanikio ya kifedha akiwa kwenye mkutano.

"Tunaamini kuwa ujumbe wa kisiasa unapaswa upatikane na sio kuletwa" alisema bwana Dorsey wakati akieleza hatari anazoziona zinazoletwa na matangazo ya kisiasa.

"Mashine inaonyesha namna ujumbe wa kisiasa unaolenga jambo fulani au mtu fulani, unakuwa na taarifa ambazo zinapotosha watu kwa taarifa za uongo."

"Sio jambo ambalo linatufurahisha kulisema, 'Tunafanya kazi kubwa ya kudhibiti watu kuacha kucheza na mfumo wetu na kusambaza taarifa za kupotosha watu , lakini kama mtu atatulipa kufuatilia na kulazimisha watu kuona matangazo ya siasa… basi ni vyema... wanaweza kusema chochote wanachotaka !'"

Facebook ina kila sababu ya kujiweka mbali na matangazo ya kisiasa katika jitihada zake za kutambua taarifa zisizo sahihi.

Mark Zuckerberg

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mmiliki wa Facebook Mark Zuckerberg aliambiwa na wanasiasa wa Marekani jinsi ya kuendesha mtandao wake

Katika mkutano wa hivi karibuni kuhusu matokeo ya Facebook , bwana Mark Zuckerberg alisisitiza kuwa sera yake sio kutengeneza fedha .

Matangazo ya kisiasa yanachangia asilimia 0.5 tu katika mapato ya mtandao wa kijamii.

"Ninaweza kuwathibitishia kuwa ninapata asilimia ndogo sana kutokana na matangazo ya siasa", alisema Zuckerberg.

Kilichopo wazi katika vyama vya kisiasa kuwa ni bora zaidi kwa wao kuupoteza mtandao wa Facebook zaidi ya kurasa za Twitter ambazo wanazilipia.

Alex Balfour, ambaye ni mshauri wa masoko aliyeshauri makampuni makubwa ya michezo kutumia Facebook kutangaza taarifa zao, anaelezea namna inaweza kufanikiwa.

"Kuna maslahi makubwa zaidi ya 30,000 ambayo yanaweza kupatikana kwenye Facebook na Instagram

Mambo haya ni sawa kabisa na kuvutiwa kwao na mbwa au katika timu ya mpira, hata kama ulisafiri hivi karibuni au labda una rafiki anayesheherekea siku yake ya kuzaliwa."

aliongeza pia kuwa huwezi kuwatambua watu umri, jinsia au wapo sehemu gani.

Facebook imeweza kuyafanya matangazo ya kisiasa kuwa wazi zaidi. "Tangazo liko wazi kuonyesha kuwa ni nani amelilipia na Facebook iliruhusu mtu yeyote kuangalia maktaba yao Facebook na kuangalia jumla ya fedha iliyotumika katika kila kampuni.

Bwana Alex amesisitiza kuwa Facebook imeenda mbali zaidi kwa kuweka taarifa zake kuwa wazi.

Aidha Facebook haioneshi dalili yoyote kuwa inataka kufuata nyayo za Twitter kusitisha matangazo ya kisiasa.