Nyota wa runinga amtapeli mpenzi wake wa Tinder

Suzi Taylor

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Nyota wa luninga, Suzi Taylor mwaka 2015

Mshiriki wa kipindi cha Televisheni cha uhalisia amekamatwa na polisi kwa kosa la kumshambulia kwa kipigo mpenzi wake wa mtandaoni na kumtapeli fedha.

Suzi Taylor mwenye umri wa miaka 49, alimdai fedha nyingi mwanaume aliyekuwa anawasiliana naye kwenye programu ya kupata wachumba hata kabla ya kukutana na mwanaume huyo katika makazi yake siku ya jumatano, polisi alieleza.

Mwanaume huyo alipokataa kulipa fedha hizo, mwanaume mwingine anadaiwa kuwa aliingia kwenye nyumba waliokutana na kuanza kumshambulia.

Bi. Taylor ambaye alikuwa anaonekana kwenye televisheni katika kipindi cha ukarabati wa nyumba tangu mwaka 2015.

Siku ya Alhamisi , msichana huyo na mwanaume mwenye umri wa miaka 22 walishitakiwa kwa kosa la kumpiga mtu pamoja na makosa mengine.

Kwa mujibu wa polisi, watuhumiwa wanadaiwa kuwa walimlazimisha kwa nguvu mwanaume huyo kuhamisha fedha kutoka akaunti yake ya benki na kuziweka katika akaunti zao.

Vilevile wanadaiwa kuiba kadi yake ya benki na kutoa kiasi cha fedha.

Ingawa kiasi cha fedha kilichoibiwa hakikuwekwa bayana na polisi.

Mamlaka pia haikuelezea kwa kina kama mtuhumiwa huyo alikuwa amejeruhiwa kiasi gani na kipigo alichokipata na vilevile hawakueleza kama aliwahi kukutana na bi. Taylor kabla.

Bi.Taylor alikataliwa kutoa dhamana na amepelekwa mahakamani siku ya ijumaa na kesi hiyo itasikilizwa tena tarehe 25 Novemba.