Facebook inaweza kuamrishwa kufuta ujumbe unaokiuka sheria kote duniani

Facebook logo

Chanzo cha picha, Getty Images

Facebook na mitandao mingine inayotumia programu tumishi kuotoa huduma sawa na hiyo inaweza kuamrishwa kufuta ujumbe unaokiuka sheria kufuatia uamuzi wa kihistoria wa mahakama ya juu ya muungano wa Ulaya, EU.

Mitandao ya kijamii italazimika kufuta ujumbe wowote ulio na maudhui yanayokiuka sheria badala ya kusubiri kuripotiwa .

Facebook inasema uamuzi huo umeibua "maswali muhimu kuhusu uhuru wa kujieleza".

Kesi hiyo inahusu nini?

Kesi hiyo ilitokana na ujumbe wa matusi uliowekwa kwenye mtandao wa Facebook kumhusu mwanasiasa wa Austria Eva Glawischnig-Piesczek, ambao mahakama ya nchi ilisema imemchafulia sifa.

Chini ya sheria ya Ulaya, Facebook na mitandao mingine haifai kuwajibikia maudhu yasiofaa yanayowasilishwa na watumiaji wao, hadi watakapofahamishwa kuhusu kosa hili wakati ambapo watalazimika kufuta ujumbe haraka iwezekanavyo.

Mahakamani

Haijabainika ikiwa uamuzi huo wa EU unaolazimu mitandao ya kijamiii kufuta ujumbe wenye maudhui yasiofaa unaweza kutekelezwa kwani huenda ukapingwa kupitia amri nyingine ya mahakama.

Mahakama ya juu zaidi nchini Austria iliimba mahakama ya juu zaidi ya Ulaya kufafanua masuala haya.

  • Ikiwa nchi ya EU ikibaini ujumbe usiofaa katika mahakama yake inaweza kuamrisha mitandao na prongamu tumishi kufuta nakala ya ujumbe huo
  • Ikiwa mitandao husika inaweza kua mrishwa kufuta ujumbe wenye"maudhu sawa" na ule ulioharamishwa ikiwa ujumbe huo "haujabadilishwa"
  • Ikiwa mitandao ya kijamii inaweza kuamrishwa kufuta ujumbe usiofaa kote duniani, kama kuna sheria sawa na hiyo kimataifa

Facebook haiwezi kukata rufaa kuhusiana na uamuzi huo.

Inamaanisha nini kinadhari?

"Ikiwa kuna amri ya mahakama inayosema mtu ameharibiwa jina, Facebook pia itatumia njia mbadala kubaini kosa hilo," Profesa Steve Peers, kutoka Chuo Kikuu cha Essex, aliaambia BBC.

Mwanaharakati wa kupigania haki ya faragha ya mtu binafsi Max Schrems aliongeza kuwa uamuzi huo utaathiri makundi ya watu maalum wanaotumia mtandao wa Facebook.

Mitandao ya kijamii imekua ikiwataka watumiaji wake kuelezea kwanini wanataka ujumbe ufutwe kabla ya mtandao husika kuingilia kati.

Lakini kwasababu kurasa zingine ni za wanachama pekee , waathiriwa huenda wasiweze kuzifikia.

Facebook

Chanzo cha picha, Getty Images

Sasa uamuzi juu ya suala hilo unasalia na Facebook, Bi Schrems alipendekeza.

Facebook imesema mataifa yatalazimika "kuweka ufafanuzi wakina kuhusu ni nini 'kinafanana' au 'sawa' kinadharia ".

Imesema uamuzi huo ''unahujumu kanuni ya muda mrefu kwamba nchi moja haina haki ya kutekeleza sheria zake dhidi ya nchi nyingine".

Hata hivyo mitandao ya kijamii inaweza kulazimishwa kufuta ujumbe kote duniani chini ya muongozo wa sheria ya kimataifa pekee.

"Hakuna sheria ya kimataifa kuhusiana na kosa la kumharibia mtu jina," alisema Prof Peers.

"Facebook haiwezi kusema kuwa hatuwezi kufanya hivyo nchini Marekani, japo inakiuka sheria ya Austria, haivunji sheria ya Marekani."