Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Uturuki: Ni mataifa gani yanayoiuzia silaha Uturuki?
Mataifa mengi ya Ulaya yamesitisha uuzaji wa silha kwa Uturuki kufuatia uvamizoi wake wa kijeshi kaskaini mwa Syria.
Mataifa ambayo yamekuwa yakiuzia silaha Uturuki ni Marekani na Ulaya, lakini hivi karibuni taifa hilo limeelekea Urusi kununua mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora ya angani.
Hivyobasi ni mataifa gani yameipiga marufuku Uturuki na hatua hiyo inaliweka wapi taifa hilo katika ununuzi wa silaha?
Ni mataifa gani yamekataa kuiuzia Uturuki silaha?
Mataifa tisa ya Ulaya yameweka masharti kuhusu uuzaji wa silaha kwa Uturuki.
Taifa la jamhuri ya Czech , Finland , Ufaransa, Ujerumani, Itali, Uholanzi , Uhispania, Sweden na Uingereza yote pamoja na Canada yalitangaza kwamba yanasitisha uuzaji wa silaha kwa Uturuki.
Waziri wa maswala ya kigeni nchini Uingereza Dominic Raab amesema kwkamba Uingereza itaendelea kuiuzia silaha Uturuki lakini haitatoa vibali vipya vya silaha ambazo zitatumika katika operesheni ya kijeshi nchini Syria.
Ujerumani na Uhispania zimesema kwamba masharti yao yanaathiri kandarasi mpya pekee.
Muungano wa Ulaya haujazuia uuzaji wa silaha , ijapokuwa mawaziri wa kigeni wamekubaliana kuchukua misimamo mikali kuhusu sera yao ya uuzaji wa silaha kwa Uturuki .
"Vikwazo hivyo havitarajiwi kuwa na athari kubwa , dhidi ya operesheni za Ankara iwapo vitaendelea , kulingana mchanganuzi wa maswala ya ulinzi Yvonni - Stefania Efstathiou.
Lakini iwapo vikwazo hivyo vitaendelea dhidi ya silaha zinazotumika mbali na Syria, kunaweza kuwa na athari mbaya kuhusu sekta ya ulinzi ya Uturuki.
Je ni mataifa gani makuu yanayoiuzia Uturuki Silaha?
Katika kipindi cha mwaka 1991-2017, Uturuki ilikuwa ya tano kwa ukubwa katika ununuzi wa silaha duniani.
Uturuki kihistoria ilitegemea sana washirika wake wa Nato kama vile Marekani na Ulaya kwa mahitaji yake ya ulinzi na usalama.
Marekani ndio taifa ambalo limekuwa likiiuzia Uturuki silaha, ambayo ni asilimia 60 ya bidhaa za nje zilizoagizwa katika kipindi cha 2014 na 2018.
Miongoni mwa mataifa ya Ulaya , Ufaransa, Uhispania na Uingereza zimekuwa zikiiuzia Uturuki silaha chungu nzima.
Chini ya serikali zilizotawaliwa na serikali za Uturuki miaka ya 80 na 90, ni silaha zilizoagizwa kutoka Marekani ambazo zilikuwa nyingi.
Iijipatia ndege za kijeshi , makombora , ndege aina ya helikopta, vifaru, meli na vifaa vingine ambavyo bado vinatumika na jeshi la Uturuki.
Lakini Uturuki hivi majuzi ilielekea Urusi kununua mfumo wa ulinzi uliogharimu dola bilioni 2.5, uamuzi ulioshangaza washirika wake wa Nato.
Wanahoji kwamba ununuzi huo wa mfumo wa S- 400 kutoka kwa adui wa Nato unaweza kuathiri usalama kwa kuwa wanajeshi wa Uturuki ni washirika wa vifaa vya Nato pamoja na mifumo ya angani ya ulinzi.
Marekani ilijibu kupitia kuizuia Uturuki kutonunua ndege zake za kivita aina ya F-35 , zikiwa ndio ndege za kisasa zaidi duniani.
Kutokana na eneo lake zuri la kimkakati, Uturuki inamiliki kambi kadhaa za kijeshi za Nato na Marekani, ikiwemo mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora unaotoa onyo mbali na operesheni za Nato mashariki mwa Uturuki.
Pia inamiliki mabomu 50 ya kinyuklia ya Marekani katika kambi ya wanaanga ya Incirlik karibu na mji wa kusini wa Uturuki wa Adana.
Uturuki inamiliki viwanda vya kutengenezea silaha
Uturuki imetengeza kiwanda chake cha kutengeneza silaha katika muongo mmoja uliopita ikiwa na lengo la kutotegemea wauzaji wa kigeni.
Waziri wa Uturuki wa maswala ya kigeni Mevlut Cavusoglu hivi majuzi alisema kwamba Uturuki kwa sasa inazalisha zaidi ya asilimia 70 ya vifaa vyake vya kijeshi na pia ni muuzaji mkubwa wa silaha.
Sio rahisi kubaini jinsi viwanda hivyo vya kutengeza silaha vinaafikia mahitaji ya ulinzi ya taifa hilo, kulingana na mchanganuzi Yvonni - Stefania Efstathiou.
Licha ya kwamba kile ambacho Uturuki inadai kuwa vifaa vilivyotengezwa nchini humo , ukweli ni kwamba vimenunuliwa nje.
Kati ya 2014 na 2018, Uuzaji wa silaha za Uturuki uliongezeka kwa asilimia 170.
Lakini 2018, likuwa taifa la 14 kwa ukubwa linalouza silaha duniani, huku Saudia , UAE na Turkimenistan wakiwa wanunuzi wake wakubwa.