Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Pharrell anasema 'ameaibishwa ' na maneno ya wimbo wake
Pharrell Williams anasema kuwa utata uliozingira maneno ya mistari ya nyimbo zake ulimfanya abaini kuwa baadhi ya nyimbo zake "ziliendeleza" utamaduni wa ubaguzi wa kijinsia.
Muimbaji huyo anasema kuwa kwa mara ya kwanza hakuelewa ni kwanini baadhi ya watu waliyaona maneno ya mistari ya nyimbo zake kama "uchochezi wa ubakaji".
Lakini baadae alibaini kwamba "kuna wanaume wanaotumia lugha inayofanana na hiyo kuwadhalilisha kingono wanawake ".
Wimbo huo unaojulikana kama Blurred Lines (Mistari iliyofichwa) katika nyimbo zake ilikosolewa na baadhi ya watu ambao walidai kuwa maneno hayo yalichochea ngono bila muafaka.
Nyimbo hizo zilipigwa marufuku katika vyuo vikuu kadhaa na tangazo la biashara lililokuwa na wimbo na walioigiza katika video yake kupigwa marufuku kuchezwa katika vipindi vya mchana vya televisheni mwaka 2013.
Katika mahojiano na jarida la GQ, Pharrell, mwenye umri wa miaka 46, alisema kuwa alizaliwa ''katika enzi tofauti " na baadhi ya mambo mengine ambayo yaliokuwa yanaruhusiwa wakati huo "hayawezi'' kufanyika wakati huu.
Alitoa mfano wa matangazo ya kibiashara "yaliomuonesha mwanamke kama chombo" na "maudhui ya nyimbo ".
"Baadhi ya nyimbo zangu za zamani, siwezi kamwe kuziandika au kuziimba leo hii''.
"Ninaaibishwa na baadhi ya nyimbo hizo. Ilinichukua muda mrefu na kukua ili kufikia mahali pale."
Alisema kuwa mistari iliyofichwa ilimsaidia kupanda kimuziki lakini akakiri kuwa mwanzo "hakuelewa"ni kwanini nyimbo hizo zilipingwa kiasi kile na baadhi.
Wimbo - ambao aliuimba kwa ushirikiano na Robin Thicke -ulijumuisha mistari kama vile "Ninachukia sana mistari hii iliyofunikwa, ninajua mnaitaka " na " Lazima ninataka kuwa mbaya".
Muimbaji huyo alisema kuwa aliwaona baadhi ya wanawake waliupenda wimbo huo na wangeweza kuimba maneno hayo wakati wowote
"Na kisha nikagundua kuwa kuna wanaume ambao hutumia lugha hiyo hiyo kuwadhalilisha wanawake, na haijalishi hiyo sio tabia yangu. Au jinsi ninavyofikiria mambo.
"Ni muhimu kuelewa jinsi inavyowaathir wanawake. Na nikasema sasa nimeelewa Ni vizuri "
Aliongeza kuwa "Niligundua kwamba tunaishi katika nchi ambayo ina wabaguzi . Sikuwa nimegundua hilo . Sikutambua kwamba baadhi ya nyimbo zangu zilikuwa na mwelekeo huo ."
Wimbo wake ulikuwa namba moja kwenye chati za muziki za Uingereza kwa wiki kadhaa na awali Pharrell aliitetea mistari ya nyimbo hizo.
Katika mahojiano na Pitchfork alisema "Unapomuangalia vizuri katika wimbo mzima, ujumbe ni kwamba ni msichana mzuri, na hata wasichana wazuri wanataka kufanya mambo na hapo ndipo mistari inafichwa.
"Anaponesha hisia zake katika mtindo wake wa densi kwasababu ni msichana mzuri. Watu wanakasirika tu wanataka tu kuwa wendawazimu na ninayakubali maoni"
Pharrell na Robin Thicke pia wamekuwa na matatizo mengine kuhusu nyimbo hizo.
Waliambiwa walipe faini ya dola milioni 5 baada ya familia ya Marvin Gaye' kudai kuwa wimbo huo ni nakili ya wimbo wa gaye wa mwaka 1977 uliojukana kama Got to Give It Up.