Tanzania: Mahakama imemuachilia huru Michael Wambura makamu wa rais wa zamani wa TFF

Michael Wambura
Maelezo ya picha, Makamu wa Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF), Michael Wambura
Muda wa kusoma: Dakika 2

Mahakama nchini Tanzania imemuachilia huru aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF), Michael Wambura baada ya kuingia makubaliano na Jamhuri ya kulipa zaidi ya shilingi Milioni 100 ambazo alijipatia kwa njia isiyo halali

Tayari Bw. Wambura amelipa shilingi Milioni 20 za Tanzania kama sehemu ya fedha hizo atakazolipa kwa awamu tano.

Wambura ambaye amefungiwa maisha kujihusisha na soka, alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Februari 11 mwaka huu, akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashitaka 17 yakiwemo ya kutakatisha fedha zaidi ya shilingi za Tanzania milioni 100.

Kwa mujibu wa sheria za Tanzania, mashtaka ya uhujumu uchumi hayana dhamana, na wote wanaoshtakiwa nayo husalia rumande mpaka kutoka kwa hukumu zao.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Biswalo Mganga aliwasilisha ripoti ya suala hilo kwa rais wa Tanzania John Pombe Magufuli na kuongeza kuwa kiasi cha Shilingi bilioni 107 za Tanzania sawa na takribani dola milioni 4.6 zitarejeshwa na watuhumiwa hao.

Hii ni baada ya watuhumiwa 467 wa makosa ya uhujumu uchumi nchini Tanzania kukiri makosa na kuomba msamaha.

Rais Magufuli alitangaza msamaha Septemba 22, kwa watuhumiwa wa makosa hayo ambao wataandika barua za kukiri makosa, kuomba radhi na kukubali kulipa fedha wanazotuhumiwa kujipatia kinyume cha sheria.

"DPP mfanye haraka, msichukue muda mrefu kupitia maombi hayo ili watu hawa warudi kwenye jumuiya zao. Ikichukua mwezi ama mwaka hata dhana nzima ya msamaha itaondoka," ameagiza rais Magufuli Jumatatu wiki hii.

Hii ni baada ya watuhumiwa 467 wa makosa ya uhujumu uchumi nchini Tanzania kukiri makosa na kuomba msamaha.

Ruka Instagram ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa Instagram ujumbe

Katika vita hiyo, vigogo kadhaa wa serikali walifutwa kazi kwa tuhuma za uzembe na rushwa.

Watu kadhaa pia wamefunguliwa mashtaka ya uhujumu uchumi na kesi nyingi kati ya hizo bado zinaunguruma.

"Najua wanateseka. Unaona wanavyopelekwa mahakamani, wengine wamekonda kweli, inatia huruma na inaumiza. Najua wengine wanataka kuomba msamaha..." alisema Magufuli Septemba 22, wakati akitangaza msamaha.

John Magufuli

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Rais wa Tanzania, John Magufuli

Hata hivyo alionya kuwa kwa wale watakaoshindwa kuomba msamaha, waendelee kubanwa hata kama kesi zao zitachukua miaka 20.

"Nimetoa siku saba hizi na baada ya hizi sitatoa tena...watakaoendelea kukaa gerezani wasimlaumu mtu," aliseisitiza

Jumla ya Shilingi bilioni 107 za Tanzania sawa na takribani dola milioni 4.6 zinatarajiwa kurejeshwa na watuhumiwa hao