Rushwa Kenya: Je kuziondoa noti za zamani zimesaidia kukabiliana na tatizo hili?

Chanzo cha picha, AFP
- Author, Reality Check
- Nafasi, BBC News
Tuhuma: Maafisa nchini Kenya wanasema hatua ya kuondoa matumizi ya noti za zamani katika jitihada za kukabiliana na rushwa au ufisadi imefanikiwa.
Noti za zamani za shilingi 1,000 zimesitishwa kuchapishwa Juni nchini Kenya na tangazo lililtolewa kwa yeyote aliye na noti hizo abadili kupata noti mpya zilizozinduliwa kufikia Septemba 30 kama njia ya kuwabaini waliojipatia fedha kwa njia haramu au wanaohodhi fedha.
Uamuzi: Zaidi ya 96% ya noti hizo za zamani zimerudishwa na kubadilishwa kwa noti mpya, licha ya kwamba kuna shaka kuhusu ufanisi wa hili katika kubaini fedha zinazohusishwa na ufisadi. Hatua hiyo haionekani kuuathiri uchumi kwa ujumla kwa kiwango muhimu.

Gavana wa benki kuu Kenya Patrick Njoroge amesema shughuli ya kuziondoa noti hizo ilikwenda vizuri na wamefanikiwa kuzifanya fedha zinazomilikiwa na watu ambao hawakutaka zichunguzwe, kutokuwa na thamani.
Kati ya shilingi milioni 217 za noti za 1,000 zilizokuwa zikizunguka kuanzia Juni mosi wakati zoezi hili lilipotangazwa, milioni 210 million (96.6%) zilirudishwa kufikia Septemba 30.

Chanzo cha picha, Getty Images
Na hilo linamaanisha usawa wa $74m ziliishia kutokuwa na thamani.
Licha ya kwamba baadhi ya ambao bado wana noti hizo za zamani huenda wakawa:
- wanaishi vijijini
- wamekwama ng'ambo
- wanaziweka kama kumbukumbu
Njoroge anaamini pia kuwa Kenya imeepuka matatizo yalioshuhudiwa India wakati mnamo 2016 taifa hilo liliondowa matumizi ya noti za thamani kubwa kama sehemu ya msako dhidi ya ufisadi na fedha haramu.
Ripoti ya benki kuu ya India imesema 99% ya noti hizo za zamani zilizokuwa ziktumia kabl aya marufuku ziliwasilishwa baadaye, kuashiria kuwa watu wengi waliokuwana fedha hizo kinyume cha sheria walifanikiwa kupata njia za kuzihifadhi kwenye benki kwa njia halali.
Visa 3,172 vya uzungukaji wa fedha vilivyotajwa kushukiwa wakati wa zoezi hilo nchini kenya vitachunguzwa, Njoroge anasema lakini 96% kati yao ulihusisha chini ya shilingi laki tano au $5,000.
Licha ya kwamba hili huenda pia likaashiria kuwa wale waliokuwa na fedha nyingi walifanikiwa kuzigawanya katika viwango vidogo vya fedha na kuepuka kuchunguzwa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwame Owino, wa taasisi ya masuala ya uchumi mjini Nairobi ameiambia BBC News: "Mojawapo ya sababu wa kuondolewa matumizi ya noti hizo - tunaarifiwa - ilikuwa ni haja ya kukabiliana na ufisadi na biashara haramu ya pesa, lakini hakuna aliyekamatwa kufikia sasa."
Na mwezi uliopita, benki kuu nchini iliripotiwa kuwa na wasiwasi kuhusu ongezeko la ghafla katika bei ya unga wa ngano katika sheemu moja nchini Kenya, huenda kutokana na watu wanaojaribu kukwepa udhibiti wa sarafu hiyo.
Kulikuwa na hofu pia kwamba zoezi hilo lingechangia wau kukimbilia kununua bidhaa, na kuchangia kuongezeka bei za bidhaa nchini.
Lakini hilo halikufanyika. Kiwango hicho kilishuka Septemba kwa 3.83%, kutoka 6.58% mnamo Aprili.
Baada ya mwezi wa kwanza kufuaia tangazo hilo, shilingi bilioni 25 ziliwekwa katika mabenki na kuchangia kushuka kwa kiwango cha fedha zilizo kwenye mzunguko nje ya mabenki.
Maafisa wanasema thamani ya sarafu ya shilingi ya kenya haikuathirika pakubwa.
Lakini imepanda kutoka 101.3 dhidi ya dola mapema Juni hadi 103.9 mwishoni mwa Septemba.
Noti hizo mpya pia zilinuiwa kuwa vigumu kutengeneza za bandia.
Lakini mwezi mmoja baada ya kuzinduliwa, washukiwa kadhaa walikamatwa na noti mpya feki.
















