Sarafu mpya Kenya: Je, tayari kuna noti mpya feki zinazosambaa?

New Kenyan notes

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Sarafu mpya zilizinduliwa kutimiza masharti ya katiba, kukabiliana na ufisadi na fedha ghushi
    • Author, Na Reality Check
    • Nafasi, BBC News
  • Muda wa kusoma: Dakika 2

Kumekuwepo na taarifa zinazoenea katika mitandao ya kujamii kwamba noti mpya za thamani kubwa zaidi Kenya tayari imeghushiwa.

Noti hizo za shilingi 1000 zilizinduliwa wakati wa sikukuu ya Madaraka pamoja na noti nyingine kutimiza masharti ya kikatiba, kukabiliana na ufisadi na ueneaji wa fedha ghushi.

Ukurasa mmoja maarufu wa kijamii ulieneza ujumbe unaodai kwamba tayari kuna noti mpya bandia ambazo zinaenezwa.

Hata hivyo, hakuna ushahidi wowote kwamba taarifa hizo ni za kweli.

Taarifa hizi zilienezwa vipi?

Ukurasa maarufu ya kuhusu hali ya foleni au msongamano wa magari barabarani Kenya katika Twitter, Ma3Route, ambao una zaidi ya wafuasi milioni moja, ulieneza ujumbe na picha zilizokuwa zimepakiwa mtandaoni na mtu mwingine zikidai kwamba kulikuwa na noti bandia.

"Iwapo mtu anaweza kubaini chanzo cha picha hii, basi Wakenya wasio na hatia wataokolewa [kutoka kwa matapeli]. Hizi ndizo noti bandia zinazoenezwa," ujumbe huo wa Twitter ulisema.

Ujumbe huo uliashiria kwamba noti zilizokuwa kwenye picha hiyo zilikuwa bandia.

Hata hivyo, hivyo si kweli.

Noti zilizopigwa picha ni noti halali.

Aliyendika ujumbe huo alikanganyikiwa kati ya upande mbele na nyuma wa wa noti mpya za shilingi 1,000 za Kenya. Upande mmoja, kuna picha ya Majengo ya Bunge na upande mwingine Jumba la Kimataifa la Mikutano la Kenyatta (KICC).

Picha zote mbili zinapatikana kwenye noti mpya ya shilingi 1,000.

Picha hizo asili yake ni ukurasa wa mwandishi wa BBC ambaye alikuwa amepicha picha noti halali kutoka Benki Kuu ya Kenya.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Madai zaidi ya noti feki

Ujumbe mwingine ulioenezwa sana kwenye WhatsApp na Twitter unasema yupo mtu aliyetapeliwa $170 (shilingi 17,000 za Kenya) baada ya kukabidhiwa noti bandia za shilingi 1,000.

Inaambatanishwa na ujumbe unaowatahadharisha watu wawe "macho, kuna noti bandia."

Baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii wanasema rangi kwenye picha ya noti iliyowekwa ina mkolezo tofauti wa rangi.

Msemaji mmoja wa Benki Kuu ya Kenyua aliambia BBC kwamba ni vigumu kubaini uhalisia na uhalali wa noti kwa kutazama picha pekee.

Aidha, alisema kufikia sasa hawajapokea taarifa zozote za kuwepo kwa noti mpya bandia.

Kulikuwepo pia na taarifa kwamba mwanafunzi wa chuo kikuu kimoja Nairobi alikuwa amekamatwa na noti bandia za jumla ya shilingi 10 milioni.

Madai hayo yalichapishwa kwenye blogu kadha na kuenezwa na watu kupitia WhatsApp. Ilidaiwa pesa hizo ghushi zilikuwa za noti za elfu moja na mia tano.

Taarifa hizo zilidai kwamba mtuhumiwa ambaye ana miaka 21 alikamatwa baada ya wadokezi kutoa taarifa kwa polisi.

Lakini Benki Kuu ya Kenya inasema hakuna kisa kama hicho kilichoripotiwa.

Presentational grey line
Reality Check branding