Athari na manufaa ya kuwa mtu mfupi

Kwa wanaume, baadhi hutamani kuwana urefu lakini Allan Mott, ambaye ni mfupi kwa 18cm kuliko wanaume wenye kimo cha wastani Canada amejikubali kwa ufupi alio nao.

Ushawahi kupendwa na watu wa jinsia ya pili popote unapokwenda?

Ndio yalionikuta nikiwa shuleni. Nilipotokeza tu, wasichana wakubwa walikuwa wakipiga kelele kwa furaha na kunifukuza mpaka nashindwa kuimbia tena. Wanaponikamata, wananikumbatia na kunibusu shavuni kabla ya kuniachilia niende nikacheze au nifukuzwe tena na mwingine.

Kuanzia kukabiliwa na mapenzi hayo mpaka kuishia kuwa tu mvulana mdogo darasani. Nilikuwa mcheshi , lakini kutokana na kuanza kuchezewa shere , niliondoka mara nyingi na kwenda kwenye maktaba kusaidia kupanga vitabu wakati watoto wenzangu wakicheza.

Wakati nikikuwa, daktari wa watoto alikadiria kwamba pengine huenda nikarefuka hadi 167cm, au pengine hata 172cm nikibahatika, ambacho ndicho kimo kinachokaribiana na wasatani wa urefu wa mwanamume nchini Canada.

Lakini makadirio hayo yalikuwa mbali mno na uhalisi. Niliacha kurefuka baada ya kuadhimisha miaka 13 tangu kuzaliwa. Niliishia kuwa na urefu wa 157cm, ambazo ni 10cm juu yakimo cha mbilikimo.

katika miaka iliyopita tangu hapo. Nimeishia kuamini mambo mawili kuhusu kuwa mtu mfupi :

1. Sio jambo zuri

2. Hakuna anayetaka kukusikia ukilalamika kulihusu

Huwa sipendi kulizungumzia. watu wameshaahi kuniambia, "Hebu tueleze, yaani watu hawajawahi kukuchukulia tofuati kwasababu wewe ni mfupi!" (Kila anayenimabia hili kwa kawaida ana urefu wa angalau 180cm.)

Lakini najua uhalisi wa maana ya kuwa mtu mfupi katika jamii yetu. Kuna unyanyasaji mkubwa kuhusu urefu kama ilivyokuwa kuhusu masuala ya jinsia, kabila na hata dini.

Sio siri kwamba wanawake hulipwa pesa kidogo kuliko wanaume kwa kazi sawa. Kitu ambacho watua wanastahili kujua ni kwamba urefu wa mtu ni suala muhimu katika utofauti wa mishahara.

wanaume wafupi hufunzwana jamii kujikubali na kukubali chochote wanachopata. Ninapopata kazi na niependekezewa mshahara kiwango fulani, hisia ninayokuwa nayo ni: "Ni chini ya kiwango nilichotarajia, ahh lakini sawa nitachukua tu." Pengine mtu mrefu atahisi anastahili kulipwa zaidi na aseme: "Hapana nahitaji elfu 10 zaidi."

Ushawahi kuingia katika ukumbi ukahisi unakaguliwa na kupuuzwa katika muda usiozidi sekundi kadhaa?

Watu wafupi wanalifahamu hilo vizuri sana.

Mwanamume mrefu anaposimama na kujitetea anaonekana kujiamiani, lakini kwa mtu wa urefu wangu anayepigania kusikika huonekana kama mtu asiyejiamini anyehitaji usaidizi.

Mara nyingi nilijikuta napigana nisikike, lakini nikaishia kuonekana kama mtu mwenye maudhiko na mshindani.

Hata kama nina hoja nzuri kiasi gani, mara nyingi nilipuuzwa kwasababu ilikuwa imeshaamulika kwamba sina la maana la kuchangia.

Nimewaona wafanyakazi wenzangu wanawake wakiyapitia kama haya. wakati wanahisi unyanyasaji wanaopitia ni wa kijinsia, mara nyingi nabaki nikiwaza ni kwa kiasi gani unyanyasaji huo unatokana na urefu wa mtu?

Vipi linapokuja suala la kutafuta mchumba?

Ukweli ni kwamba ukiwa mtu mfupi unapaswa kutarajia wanawake 8 kati ya 10 kukupuuza punde wanapokuona.

Na kwa waliosalia wawili huenda wakakupa dakika mbili tu ikizidi sana za muda wao.

Kila ninapowaambia rafiki zangu wa kike kwamba wanawake hawapendi wachumba wafupi, karibu wote hukana na kusema: "Sio kweli. Bila shaka kuna wanawake wengi wanaopenda wanaume wafupi."

"Ushawahi kutoka na mwanamume mfupi?" Nawauliza

"Ummm hapana…" wanajibu

"Je unaweza?"

Kimya kinatanda.

Kwa mujibu wa Freakonomics, kitabu chake Steven Levitt na Stephen Dubner, wanaume wafupi huenda wasipate majibu wanapotafuta wachumba mitandaoni kuliko kundi jingine lolote la watu.

Licha ya kwamba kuna namna ambavo sheria hii hukiukwa ambao ni mfano watu wanaopenda kuutaja.

"Wanawake walimpenda Prince na alikuwa mfupi!" Utasikia watu wakisema mara kwa mara.

Sasa ina maana maishani mwangu yote nivae viatu vya mchuchumio, na niwe nguli wa muziki, kama alivyokuwa Prince ambaye pia ni mtumbuizaji mashuhuri wa kizazi chake.

Baadhi ya watu pasi kujua huhusisha urefu na nguvu, uhodari na kutokana na hilo wengi hufikiria wau warefu ni viongozi bora kuliko wenzao walio wafupi.

Nakiri kwamba pengien saa ningine ninayafanya maisha ya mtu mfupi yakae mabaya kuliko ilivyo.

Je maisha yangu yangelikuwa rahisi zaidi iwapo ningeongeza urefu wa 15cm shuleni? Pengine, lakini sio kwamba maisha nilioishi yamekuwa ni ya uchungu mtupu na huzuni.

Mimi ni mimi kwasababu ya urefu wangu , Imenipa fursa ya kufanya lolote nitakalo maishani mwangu.

Na ninapozidi kukuwa kwa umri, nahisi ni kana kwamba nazidi kunawiri.

Miaka michache iliyopita, nilifikiria ni ucheshi ninapojigoa kwa kimo changu, lakini nikapatana na jamaa mmoja aliyeniambia nitakupiga ngumi ukisema kitu kingine kibaya kujihusu."

Basi nimeamua , nitafanya mzaka kuhusu namna ninavyovutia.

Jambo nililogundua ni kwamba watu wanapenda wanapocheka na mimi khusu kitu kizuri.

Jamii huenda haione kuwa sura yangu ni ya kuvutia, lakini nitaendelea kulisisitiza hilo kwamba mimi ni mzuri.