Utafiti mpya wazua mjadala kuhusu athari za kiafya za ulaji nyama

Chanzo cha picha, Getty Images
Utafiti wenye utata unasema kupunguza kula nyama, soseji, nyama ya kusagwa ni kupoteza wakati kwa watu wengi.
Utafiti huo ambao unatofautiana na tafiti za awali zilizofanywa na mashirika makubwa duniani- unasema kuna ushahidi mdogo kuwa ulaji nyama husababisha athari za kiafya.
Baadhi ya wataalamu wamepongeza "utafiti" huo lakini wengine wanahofia huenda "ukawaweka watu hatarini"
Kula zaidi ya vipande vinne vya nyama zilizopitia viwandani zaidi ya mara nne kwa wiki ni hatari, ulibaini uchunguzi wa awali uliofanywa miongoni mwa watu 1,000 nchini Ufaransa, na kuchapishwa kwenye jarida la Thorax.
Watafiti wanaamini kuwa hueda sababu ya matatizo hayo ikawa ni matumizi ya kemikali ya nitrite inayowekwa kwenye nyama hizo kuzizuwia kuoza ambayo hutumiwa kwenye vyakula kama Soseji , na samaki (salami).
Lakini wataalam wanasema kuwa uhusiano wa hatari hizo haujaidhinishwa na uchunguzi zaidi unahitajika kufanyika kuthibitisha hilo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Ulaji nyama kupita kiasi umetajwa kuwa chanzo cha saratani ya utumbo.
Shirika la Kimataifa linalofanya utafiti wa saratani liligonga vichwa vya habari wakati iliposema kuwa nyama husababisha saratani.
Pia ilisema kuwa nyama nyekundu huenda ikasababisha magonjwa lakini hakuna ushahidi wa kutosha.
Ulaji nyama ni hatari kwa afya?
Nchini Uingereza pekee inaaminiwa kuwa nyama iliyohifadhiwa kwa kemikali huchangia visa 5,400 ya saratani ya utumbo kila mwaka.
Pia ualaji wa nyama ya aina hiyo umehusishwa na kisukari aina ya pili.
Makubaliano ya kisayansi kula sana ni mbaya kwa afya yako.
Utafiti unasema nini?
Watafiti wanaoongozwa na Vyuo vikuu vya Dalhousie na McMaster nchini Canada - walichunguza ushadi ulioangaziwa na watafiti wa awali.
Matokeo ya utafiti uliochapishwa katika jarida la kimatibabu la Annals of Internal Medicine unaashiria kwamba ikiwa watu 1,000 watapnguza kula kiwango cha nyama wanachokula kila wiki:
- Katika maisha yao, kutakua na vifo vichache vinavyotokana na ugonjwa wa saratani
- Kwa miaka 11 kutakua na vifo vichache vitakavyotokana na maradhi ya moyo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Utafiti huo umepokelewaje?
Kevin McConway, profesa wa premeritus wa takwimu zilizotumika katika Chuo Kikuu cha Open, aliitaja kuwa "sehemu kamili ya kazi"
Na Profesa David Spiegelhalter, kutoka Chuo Kikuu cha from Cambridge, anasema: "Uhakiki huu wa kina bado haujapati ushahidi mzuri wa faida muhimu za kiafya zinazotokana na kupunguza ulaji nyama.
"Kwa kweli, haipatikani ushahidi wowote mzuri."
Lakini badala ya kuwa na hofu juu ya ulaji wa aina moja ya chakula, watu wanapaswa kula chakula chenye virutubisho vya kiafya na vya aina mbali mbali, walishauri wataalam.
Wataalam wanasema watu wanapaswa kula nyama nyekundu ambacho si zaidi ya gramu 70 kwa siku, ama kiwango hicho hicho cha yama zilizopitia viwandani kwa ajili ya kuwa na afya bora.
Kiwango hiki ni sawa na takriban Soseji moja ama viande viwili vya nyama kwa siku.













