Je, Waafrika wanaweza kuacha vyakula vyao vya kitamaduni?

Makamu wa rais, nchini Zambia amewataka raia wa nchi hiyo kubadili aina ya vyakula wanavyokula, kama vile kuacha kula ugali na kula vyakula vilivyo na virutubisho bora zaidi.

Mapendekezo hayo ni sawa na kuwaambia waitaliano kuacha kula tambi.

Ugali ni chakula maarufu maeneo ya kusini na mashariki mwa Afrika huku takwimu zikionyesha kuwa nchi hizo katika jangwa la sahara zinatumia asilimia 21 ya mahindi yanayozalishwa duniani.

Makamu huyo wa rais, Bi Inonge Wina amesema kuwa kuna uhitaji wa mabadiliko ya lishe wakati ambapo maeneo mengi ya nchi hiyo na nchi jirani yanakabiliwa na ukame na uhaba wa chakula kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.

Tatizo hili limepelekea raia millioni 1.7 wa nchi hiyo ambayo ni 18% ya idadi ya raia ambao wanakumbana na uhaba wa chakula. Huku takwimu zilizotolewa na Umoja Wa Mataifa zinasema asilimia 40% ya watoto chini ya miaka mitano wanautapia mlo .

Bi. Wina ambae ni mtaalamu wa afya na chakula amesema ili kupunguza tatizo hilo watu hawana budi kubadili namna ya kula kwa kula pia mtama, mihogo na viazi vitamu ambavyo pia itapunguza idadi ya milipuko ya utapia mlo kwa raia wa nchi hiyo.

Idadi kubwa ya raia wa Zimbabwe hula ugali mara mbili hadi tatu kwa siku. Na baadhi hawali mpaka pale wanapopata ugali kwanza, ambapo kwa nchini Zimbabwe chakula hiki huitwa nshima, huku kikiitwa nsima nchini malawi na sadza nchini Zimbabwe, Afrika ya Kusini na Nchini Lesotho wakikiita papa au pap na Kenya wakiita Ugali.

Chakula hicho cha mahindi kwanza huchemshwa na maji, huongezwa chumvi kidogo. Baadae kukorogwa kidogo katika uzito unaofaa na baadae kusongwa .

Clifford Chirwa ni mwanafunzi wa mwaka wane katika chuo kikuu cha Zambia yeye amesesema hakuwa na Imani na serikali kuweza kupambana na suala la mlo mbovu.

'Si raisi kwani kila tamaduni ina chakula chake ambacho hukiona bora. Kama ambavyo Nigeria wana chakula chao ambacho ni wali, hivyo nshima ni chakula cha tamaduni ya watu wa Zambia' aliiambia BBC.

Olipa Lungu ni mmiliki wa mgahawa uliopo sokoni mji mkuu wa Zambia, Lusaka amesema jitihada zake za kuboresha milo zimegonga mwamba. huku akisema chakula kingine kinachopendwa na watu ni chipsi, na hupikwa kama mtu akihitaji.

Mapendekezo hayo ya mradi huo wa Bi. Wina umeungwa mkono na Umoja wa Wakulima Wa Zambia.

'maajilio ya tabia nchi yanatuhamasisha kuanza kuhamasisha watu kutumia vyakula vinginekwani kwa mda mrefu tumekuwa tunategemea mtama na mpunga. Hatuli vyakula vingine, hivyo hii ni hatua nzuri ya makamu wa raisi ameichukua', msemaji wa Umoja huo Kaloma Kalevi aliiambia BBC.'

Baadhi ya wataalamu wa vyakula wamesema mahindi yanayouzwa sokoni yanakuwa yamekobolewa sana hivyo hukosa virutubisho muhimu kwa afya bora ya ngozi, nywele na ubongo.

Mahindi yanapoliwa bila kupikwa huwa na virutubisho kama vile Vitamini A, Vitamini C, chuma na nyuzi lakini vyote hupotea kadri yanavyoandaliwa.

Chakula cha mahindi ni maarufu hasa kwa familia masikini kwani mara nyingi hutolewa kama msaada na serikali, alisema daktari wa chakula wa Afrika Kusini Thandolwakhe.

'Mahindi ya njano ndiyo yenye virutubisho Zaidi kuliko mahindi meupe, lakini kwa bahati mbaya tumekuwa na kasumba kwamba mahindi ya njano ni haki ya watu wa tabaka la chini,'mtaalamu aliongeza

Vyakula kama mtama na ulezi vyakula mabavyo vina wanga, protini na mafuta. Pia vina vitamini A na B, Kalisi(Calcium), chuma, zinki, potasiamu, phosphororus, magnesiamu, shaba na manganese.

Lakini virutubisho hivi vinasaidia nini?

Vitamini A husaidia uoni

Vitamini B1 huleta wanga

Vitamini C husaidia kupunguza magonjwa na huimarisha mifupa

Chuma inahitajika kwaajili ya oxygen katika damu

Kalisi(Calcium) huimarisha mifupa na meno

Zinki husaidia kuunda majeraha

Tukiwa tunaangazia mabadiliko ya tabia nchi na athari zake katika upatikanaji wa chakula, vyakula hivi vinaweza kustahimili mabadiliko ya hali ya hewa,'alisema Bi. Msomi.

'Watu walipata elimu juu ya kilimo cha mahindi majumbani mwao hivyo wanaweza kupewa elimu juu ya kilimo cha vyakula hivi vingine'aliongeza