Meli ya mafuta ya Iran : Kwa nini Marekani ilijaribu kumhonga naodha wa meli hiyo

Meli hiyo iliondoka Gibraltar mwezi Agosti, licha ya juhudi za marekani za dakika za mwisho

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Meli hiyo iliondoka Gibraltar mwezi Agosti, licha ya juhudi za marekani za dakika za mwisho
Muda wa kusoma: Dakika 2

Idara ya maswala ya kigeni nchini Marekani imethibitisha ilitoa mamilioni ya madola kwa nahodha wa meli ya mafuta ya Iran ambayo ipo katikati ya mgogoro wa kidiplomasia.

Brian Hook, kiongozi wa idara ya Iran Action Group, alituma barua pepe kwa nahodha wa meli ya Adrian Darya 1 kuhusu kuiegesha mahala ambapo Marekani inaweza kuikamata.

Meli hiyo ilituhumiwa kusafirisha mafuta nchini Syria na ilikamatwa kwa muda mfupi na mamlaka ya Uingereza katika taifa la Gibraltar mnamo mwezi Julai.

Iliachiliwa mwezi uliopita baada ya Iran kusema kwamba haikuwa ikielekea Syria.

Idara ya maswala ya kigeni nchini Marekani ambayo ilikuwa imejaribu kuzuia kuachiliwa kwake , baadaye ilitoa kibali cha kuikamata.

Ripoti hiyo ya ombi hilo la fedha kwa nahodha huyo kwanza lilionekana katika gazeti la Financial Times siku ya Jumatano na limethibitishwa na idara hiyo ya maswala ya kigeni ya Marekani.

Marekani iliipiga marufuku meli hiyo.

Taarifa ya Idara ya fedha imesema kwamba meli hiyo ilikuwa ikitumika kusafirisha mapipa milioni 2.1 ya mafuta ghafi kutoka Iran kulisaidia jeshi la Iran Revolutionary Guard tawi la jeshi la taifa hilo ambalo Marekani imelitaja kuwa gaidi.

Je barua hiyo ilisemaje?

Kulingana na gazeti la Financial Times , bwana Hook alituma barua pepe kwa nahodha huyo wa meli ya Adrian Darya 1, Akhilesh Kumar, kabla ya kuiwekea vikwazo meli hiyo.

''Naandika kuhusu habari njema'', ilisema barua hiyo.

''Utawala wa rais Trump upo tayari kukupatia mamilioni ya madola ili kuipeleka meli hiyo mahala ambapo utawala wa Marekani unaweza kuikamata.

Maafisa wa Iran wanasema Stena Impero ilivunja "sheria za kimataifa za safari za majini "

Chanzo cha picha, Reuters

Barua hizo zilishirikisha nambari ya simu ya idara ya maswala ya kigeni ili kuhakikisha kuwa nahodha huyo ambaye alikuwa akiendesha meli hiyo baada ya kukamatwa kutofikiria kwamba ilikuwa feki.

Bwana Hook aliambia gazeti hilo idara hiyo ya maswala ya kigeni ilikuwa ikishirikiana na jamii ya mabaharia ili kuzuia uuzaji wa mafuta haramu. Bwana Kumar alipuuza barua hiyo.

Marekani baadaye ilimwekea vikwazo yeye mwenyewe wakati walipoipiga marufuku meli hiyo ya Adrian darya 1.

Katika mtandao wa twitter waziri wa maswala ya kigeni nchini Iran Javad Zarif aliishutumu Marekani kwa utoaji wa hongo ya wazi.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Presentational white space

Je meli hiyo inakabiliwa na mgogoro gani?

Meli hiyo ina iliokuwa na wafanyakazi wake 29 kutoka India, Urusi, Latvia na Ufilipino ilikamatwa na wanamaji wa Uingereza tarehe 4 mwezi Julai baada ya serikali ya Gibraltar - eneo linalomilikiwa na Uingereza kusema kwamba inaelekea Syria swala ambalo ni ukiukaji wa vikwazo vya Muungano wa Ulaya.

Hatua hiyo ilizua mgogoro wa kidiplomasia kati ya Uingereza na Iran ambao uliendelea kwa wiki kadhaa huku nayo Iran ikilipiza kisasi kwa kuikamata meli ya Sweden iliokuwa ikipeperusha bendera ya Uingereza Stena Impero katika Ghuba.

Stena Impero bado ipo katika maji ya Iran ikiendeleza kuzuiliwa.

Kumekuwa na uvumi kwamba meli hiyo itaachiliwa iwapo Adria Darya itaachiliwa licha ya maafisa kukana habari hizo.

Msemaji wa wizara ya maswala ya kigeni alisema siku ya Jumatatu kwamba walikuwa wakisubiri agizo la mahakama kabla ya meli hiyo kuachiliwa lakini wakasema kwamba hakuna uhusiano wowote wa meli hizo mbili.ni?