Mwalimu wa Tibeti wa Wabudha aliyeshutumiwa unyanyasaji wa kingono amefariki

Sogyal Lakar

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Sogyal Lakar alionekana kama mwalimu bora zaidi wa Wabudha wa Tibeti baada ya Dalai Lama
Muda wa kusoma: Dakika 2

Sogyal Lakar, mwalimu wa Kibudha aliyeshutumiwa kwa kiasi kikubwa kwa unyanyasaji wa kingino na kuwatesa kimwili wafuasi wake amefariki akiwa na umri wa miaka 72.

Lakar, ambaye alifahamika zaidi kama Sogyal Rinpoche, aliuza mamilioni ya vitabu vyake na alionekana kama mwalimu bora zaidi wa wa dini ya Budha baada ya Dalai Lama.

Lakini aliandamwa na shutuma za unyanyasaji wa kingono na mateso mengine ya kimwili aliyowafanyiwa wafuasi Lakar, licha ya kwamba hakuwahi kupatikana na hatia ya uhalifu wowote.

Uchunguzi ulioitishwa na kikundi chake mwenyewe uligundua kuwa wafuasi wake walinyanyaswa nae

Ujumbe uliotumwa kwneye ukurasa wake wa Facebook ulisema kuwa alifariki nchini Thailand Jumatano baada ya kuugua kiharusi.Amekuwa akipokea matibabu ya saratani ya utumbo.

Ruka Facebook ujumbe

Haipatikani tena

Tazama zaidi katika FacebookBBC haihusiki na taarifa za kutoka mitandao ya nje.

Mwisho wa Facebook ujumbe

Akiwa ni mzaliwa wa Tibet mwaka 1947, Lakar aliaminiwa na wengi kuwa ni kizazi kipya cha Tertön Sogyal Lerab Ling, mwalimu wa 13 wa Dalai Lama.

Alisomea mahusiano ya dini katika Chuo Kikuu cha Cambridge nchini Uingereza na akawa na ufuasi mkubwa wa watu . Kitabu chake kilichoitwa - Kitabu cha Tibet cha Wanaoisha na Wanaokufa- The Tibetan Book of Living and Dying, kiliuzwa hadi nakala milioni tatu .

Lakini shutuma za tabia za unyanyasaji zilimuandama Lakar.

Mnamo mwaka 1994 mwanamke aliwasilisha mashtaka ya dola milioni 10 dhidi ya Lakar kwa kumnyanyasa kingono , kiakili na kimwili . Kesi yake ilitatuliwa nje ya mahakama.

Sogyal Lakar and the Dalai Lama

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Lakar aliaminiwa kuwa ni kizazi kipya Tertön Sogyal Lerab Ling, mwalimu wa 13 wa Dalai Lama.

Heshima yake ilishuka miaka miwili iliyopita wakati shutuma zaidi zilipojitokeza kuhusu tabia yake ya unyanyasaji. Uchunguzi huru wa wakili ulioagizwa na Rigpa, shirika la Kibudha lililioanzishwa na Lakar, ulibaini kuwa alitekeleza unyanyasaji mbaya.

"Baadhi ya wanafunzi ... hwamelkuwa wakikabiliwa na unyanyasaji mkubwa wa kingono, kimwili na kisaikolojia uliotekelezwa na yeye'', ilieleza ripoti, na kuongeza kuwa shirkika hilo lilishindwa kuchukua hatua licha ya kuwa na uelewa kuhusu shutuma.

Licha ya shutuma hizo , wengi miomgoni mwa wafuasi wa Lakar aliendelea kumuenzi na kumuheshimu.

"Ninajua ataendelea kutuongoza kwa busara na la muhimu zaidi kwa upendo ," mmoja wa wafuasi wake aliandika kwenye ukurasa wa Facebook baada ya kifo chake.

Lakini Mary Finnigan, ambaye alisaidia kuanzisha kazi za Lakar mjini London katika miaka ya 1970s na ambaye hivi karibuni alishiriki kuandika kitabu kuhusu Ngono na Ghasia miongoni mwa Wabudha wa Tibetan , ameiambia BBC kuwa Lakar alikuwa ''kiongozi katili wa kidini''

"Ninamuonea huruma kila mmoja ambaye anaomboleza kifo chake , lakini ni lazima nisema kwamba kifo chake hakiumizi hisia zangu juu ya maisha yake ," alisema.

"Alitumia vibaya utamaduni wa jadi wa kiroho kwa ajili ya kuendelea kudumu mamlakani, kupata pesa na kujiridhisha kingono ."