Jessi Combs: Dereva wa mashindano ya gari wa Marekani afariki kwa ajali

Chanzo cha picha, Reuters
Dereva na mtangazaji maarufu wa TV Jessi Combs amefariki katika ajali alipokuwa akijaribu kuvunja rekodi mpya ya kasi aliyojiwekea mwenyewe.
Familia ya Combs imethibitisha kuwa amekufa katika ajali ya gari lililoongezwa kasi ya jet-p kusini mashariki mwa Oregon, lakini maelezo zaidi hayakutolewa mara moja.
Katika taarifa, familia ilisema kuwa watamkumbuka kwa tabasamu lake na mtizamo wake hasi wa mambo
Combs, ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 39, alifahamika kama "mwanamke mwenye kasi kubwa zaidi katika uendeshaji wa magari ya magurudumu manne ".
Alipewa hadhi hiyo mwaka 2013 alipofikia kasi ya kilomita 641 kwa saa. Combs amekufa alipokuwa akijaribu kuvunja rekodi ya kuendesha kilomita 824 kwa saa - ambayo ilifikiwa na Kitty O'Neil mwaka 1976 - ambapo alipata ajali.
"Ndoto ya kuu zaidi ya Jessi ilikuwa ni kuwa dereva mwanamke mwenye kasi kubwa zaidi duniani , ndoto ambayo amekuwa akiifukuzia tangu mwaka 2012... na ameondoka katika dunia hii akiwa ndiye mwanamke aliyeendesha gari kwa kasi kubwa zaidi katika historia ," imesema familia yake.

Dereva mwenza Terry Madden pia alitoa rambi rambi zake kwenye mtandao wa habari wa kijamii.
"kwa bahati mbaya tumempoteza jana katika ajali ya kutisha . Nilikuwa wa kwanza pale na niamini tulifanya chochote ambacho binadamu anawez akufanya kumuokoa ," alisema kwenye ujumbe wa Instagram Jumatano.
Combsalikuwa akijaribu kuweka rekodi mpya ya kasi wakati alipopatwa na mauti.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa Instagram ujumbe

Jessi Combs alikuwa nani ?
Jessi ambaye alizaliwa South Dakota mwaka 1980, alianza kupenda mashindano ya magari tangu alipokuwa na umri mdogo akiungwa mkono na familia yake.
Alikwenda katika chuo cha teknolojia cha Wyoming cha WyoTech na alimaliza masomo yake akiwa mwanafunzi wa kwanza darasani na shahada ya utengenezaji wa magari. Idara ya masoko ya chuo ilimuajiri mara baada moja kwa ajilli ya kutengeneza gari kwa ajili ya msaada, ndipo alipoanza kazi yake ya kuunda vyuma vya magari.
Mara moja Combs alianza kuonekana kwenye vipindi vya televisheni , wakati mwingine akishirikiana na mtangazaji mwingine kutangaza katika msururu wa kipindi cha magari cha Xtreme 4x4, ambapo alionyesha ujuzi wake wa kutengeneza na kubadili muundo wa magari yanayotumiwa kwa mashindano ya magari.
Lakini muda wake katika msururu wa vipindi nusura umalizike kwa mkasa . Kipande cha mashine kilianguka juu yake katika studio ya televisheni na kuvunja uti wa mgongo na nusura apooze. Aliacha kutangaza kwenye kipindi hicho 008 baada ya kupona kabisa.
Combs aliendeleakuonekana katika vipindi kadhaa vya televisheni mkiwemo Overhaulin', All Girls Garage na Mythbusters.
Mtangazaji wa zamani wa Mythbusters Adam Savage alimuita "mjenzi bora wa magari ,mhandisi, dereva, engineer, driver, mbunifu, na mwenye mawasiliano ya kisayansi " katika Twitter , akiongeza kuwa "bila yeye tumebaki chini sana bila yeye ".
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe

Combs aliwatia moyo wanawake wengine wanaofanya kazi za vyuma . Alikuw ammoja wa muasisi wa Real Deal, kipindi kilichofundisha ujuzi wa kiuhandisi wanawake . Kwa mujibu wa wavuti wa , Real Deal.
Pia alibuni kiwanda kilichofua bidhaa za chuma ambazo zilitengenezwa maalum kwa ajili ya wanawake.
Wanawake wanaofua vyuma ...wamekuwepo duniani tangu Vita Kuu ya II ya Dunia, alisema katika vido moja iliyonadi shughuli zake. "Ni vizuri kwamba hatimae tumeweza kuwa na kitu ambacho kinatufaa, kwa hiyo tunaweza salama na hivyo kuweza ufanya kazi ambayo hasa tunataka kuifanya ."
Lakini kando na kazi zake ya vyuma na televisioni, Combs walikuwa mshindani mkubwa katika mashindanoi ya magari. Alijiunga na timu ya North American Eagle Supersonic Speed Challenger mwaka 2013, ambapo aliweza kufikia ukomo wake wa kasi wa kuendesha ya kilomita 641 kwa saa.
"Inaweza kuonekana kama uendawazimu kidogo kutembea moja kw amoja katka mtari wa moto ... wale wenye utashi , ndio wanaopata mafanikio ya mambo makubwa . Watu husema nina uendawazimu . Ninasema asante ," Combs aliandika katika ujumbe wake wa Instagram wiki hii.












