Hatua ya Malkia Elizabeth ya kuidhinisha shughuli za bunge zisimamishwe ina maana gani?

Chanzo cha picha, Reuters
Bunge litavunjwa tu kwa siku kadhaa baada ya wabunge kurejea kazini mwezi Septemba - na wiki chache kabla ya muda wa mwisho ambao Uingereza ilipewa kuondoka katika muungano wa Ulaya.
Boris Johnson amesema Malkia atatoa hotuba baada ya kuvunjwa kwa siku chache kwa shughuli za bunge tarehe 14 Octoba, kuainisha "ajenda zake za kusisimua sana ".
Malkia Elizabeth ameombwa na serikali kuvunja bunge siku chache tu baada ya wabunge kurejea kazini mwezi Septemba - kwenye Jumuiya ya Ulaya (EU) maarufu kama Brexit.
Mhariri wa masuala ya siasa wa BBC Laura Kuenssberg anasema kuwa hatua hii itatoa fursa kwa utawala mpya wa Waziri Mkuu Boris Johnson kuandaa hotuba ya Malkia - ukiainisha mipango ya serikali - tarehe 14 Oktoba.
Lakini ina maana kuwa wabunge huenda wasiwe na muda wa kupitisha sheria yoyote inayoweza kumzuia Waziri Mkuu kuiondoa Uingereza nje ya EU bila mkataba tarehe 31 Oktoba.
Wabunge wasiokuwa na madaraka au nafasi yoyote serikalini na mwanakampeni aliyesalia Dominic Grieve wamekiita "kitendo hicho kuwa kisichokubalika", wakaonya kuwa kinaweza kusababisha kupigiwa kwa kura ya kutokuwa na imani dhidi ya Bwana Johnson, akiongeza kuwa "Serikali hii itaanguka."

Chanzo cha picha, Getty Images
Lakini chanzo kutoka ofisi ya Waziri Mkuu kilitetea uamuzi huo , kikisema: "Ni wakati muafaka kwa serikali mpya na waziri mkuu kuweka mipango kwa ajili ya nchi kabla hatujaondoka katika Muungano wa Ulaya ."
Wazo la kusimamisha kazi za bunge bila kulivunja - limesababisha utata, huku wakosoaji wakisema litawazuwia wabunge kuweza kutekeleza wajibu wao wa kidemokrasia katika mchakato wa Brexit.
Viongozi wenye sifa kubwa katika siasa za Uingereza, akiwemo waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza John Major, wametishia kwenda mahakamani kuzuwia wazo hilo.
Upinzani, ukiongozwa na msemaji wa chama cha kitafa cha Uskochi SNP - ambacho hakipendelei kujiondoa katika Muungano wa Ulaya Joanna Cherry tayari anajiandaa kwenda katika mahakama za Uskochi kupinga hatua hiyo.
Laura Kuenssberg amesema ni idadi ndogo tu ya mawaziri katika serikali waliofahamu mapema kuhusu mpango na kwa hiyo italeta mzozo mkubwa.
Amesema serikali itadai kuwa ulikuwa ni "mfano wa kiwango cha mchakato wa hotuba ya Malkia," licha ya kelele zinazozingira.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe

Bwana Johnson anasema anataka kuondoka EU tarehe 31 Oktoba kwa mkataba lakini "ikiwa ni suala la kufa au kupona" basi yupo tayari kuondoka bila mkataba.
Msimamo huo umeibua upinzani mkubwa kutoka kwa wabunge kadhaa ambao wameungana kujaribu kuzuwia uwezekano wa kutofikiwa kwa mkataba, na Jumanne walitangaza kuwa wamepanga kutumia bunge kufanya hivyo.
Lakini kama bunge litasitishwa tarehe 10 Septemba, kama ilivyopendekezwa , itawapatia tu siku chache mnamo wiki ijayo za kushinikiza kwa ajili ya mabadiliko yao.
'Ni kashfa kubwa''
Mwanasheria mkuu wa zamani wa uingereza Bwana Grieve - ameiambia BBC Radio 5 Live kuwa : "Kama Waziri mkuu ataendelea kushikilia msimamo huu na kuatorudi nyuma , basi ninafikiri uwezekano ni kwamba utawala huu utaanguka.
" Kuna muda w akutosha wa kufanya hivyo , kama ni muhimu na nitapiga kura kuiangusha serikali ya Conservative ambayo inashikilia msimamo wake wa hatua ambazo si za kikatiba kabisa ."
Naibu kiongozi wa chama cha Leba Tom Watson alituma ujumbe wake wa Twitter akisema hatua hiyo ni "kashfa kubwa mbele ya demokrasia yetu ".
Waziri Mkuu wa Uskochi Nicola Sturgeon amesema kuwa wabunge lazima washirikiane kwa pamoja kuzuwia mpango huo wiki ijayo , au "siku ya leo itakumbukwa katika historia kama siku nyeusi katika demokrasia ya Uingereza ".
Lakini mwenyekiti wa chama cha Conservative James Cleverly alitetea mpango na kuutaja kama "kile ambacho serikali zote mpya hufanya".

Bunge kwa kawaida husitsha kw amuda kwa kipindi kifupi kabla ya vikao kuanza . Hufanywa na Malkia kwa ushauri wa waziri Mkuu.
Vikao vya bunge kwa kawaida hukaa kwa kipindi cha mwaka, lakini vikao vya sasa vimekuwa vikiendelea mfululizo kwa zaidi ya miaka miwili tangu mwezi Juni baada ya uchaguzi wa mwaka Juni 2017.
Wakati bunge linapositishwa kwa muda , huwa hakuna mijadala wala kura zinazopigwa - na sheria nyingi ambazo huwa hazijakamilika kwa ajili ya kupitishwa na bunge huwa hazipitishwi kabisa.
Hii ni tofauti na "kuvunja " Bunge - ambapo wabunge huondoka kwenye viti vyao kufanya kampeni katika uchaguzi mkuu.

Bunge lilirejea kazini kutoka mapumziko ya msimu wa kiangazi - au mapumziko mafupi -wiki ijayo na mapumziko mengine yalitarajiwa kati ya tarehe 13 Septemba na tarehe 8 Oktobato kwa kipindi cha msimu wa mikutano ya kisiasa .
Kulikuwa na tetesi , hata hivyo kuwa vikao hivyo vingefutwa au kufupishwa ili kuendeleza mazungumzo ya kuelekea Brexit.
mara ya mwisho bunge lilisitishwa mara mbili kwa ajili ya hotuba ya Malkia ambayo haikuwa baada yauchaguzi mkuu , lilifungwa kwa siku nne za kazi na siku 13 za kazi.
kama kipindi hiki cha usitishwaji wa shughuli za bunge kitatekelezwa kama inavyotarajiwa , bunge litafungwa kwa siku 23 za kazi.
Kiomngozi wa zamani wa Wabunge wasiokuwa na madaraka au nafasi yoyote serikalini Iain Duncan Smith ameimbai BBC Radio 5 Live kuwa uamuzi wa kusitisha shughuli za bunge "si ishara ya kitu kibaya kabisa ",na tarehe za usitishwaji wa vikao ni ''kipindi ambacho ni sawa'' na kile cha mapumziko ya vikao vya chama.
Amesema kuwa Bwana Johnson alikuwa anajaribu kuona mkataba mpya wa Brexit unakubaliwa , na wabunge ambao "walikuwa wakijaribu kumzuwia swanahitaji kujifikiria upya ya umakini".
Wabunge wanapaswa kuidhinisha tarehe za mapumziko, lakini hawawezi kuzuwia usitishwaji wa muda wa shughuli za bunge.













