Mamia waandamana ubalozi wa Afrika Kusini Dar es Salaam kutaka ndege ya Air Tanzania kuachiwa

Zaidi ya watu 100 jijini Dar es Salaam wameandamana mpaka ubalozi wa Afrika Kusini wakishinikiza kuachiwa kwa ndege ya Air Tanzania inayozuiliwa jijini Johannesburg.
Waandamanaji hao waliokuwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali kwa lugha za kingereza na kiswahili wamefika katika ubalozi huo uliopo kati kati ya jiji asubuhi ya leo.
Walikuwa wakisisika wakiimba: 'Tunataka ndege yetu, tunataka ndege yetu.'
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Ndege hiyo iliyokuwa inatoka Johannesburg, Afrika Kusini kwenda jijini Dar es Salaam, Tanzania Agosti 23, 2019 ilizuiwa kuruka kwa amri ya Mahakama Kuu ya jimbo la Gauteng.

Haijulikani watu hao walitumia njia gani kujikusanya ama wanafungamana na kundi gani la kisiasa ama kiharakati.
"Hili ambalo wamelifanya la kuandamana halikubaliki. Tuheshimu sheria hata pale tunapoona jambo linafanyika halipendezi lakini kuheshimu sheria ni jambo la maana sana," amesema Mambosasa.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Kwa nini ndege imezuiliwa?
Ndege hiyo aina ya Airbus A220-300 imeshikiliwa katika uwanja wa Oliver Tambo jijini Johannesburg kwa amri ya mahakama.
Msemaji mkuu wa serikali ya Tanzania Dk Hassan Abbas hivi karibuni amefafanua kuwa ndege hiyo imeshikiliwa kutokana na kesi ya fidia inayomhusu raia wa Afrika Kusini Bwana Hermanus Steyn na Serikali ya Tanzania.
Mtu huyo ambaye alikuwa anamiliki ardhi, mifugo na mali nyingi, zilitaifishwa na serikali ya Tanzania miaka ya 1980 na walifikia makubaliana na serikali ya Tanzania.
"Kesi hii ni madai ya muda mrefu ya fidia ya ardhi iliyotwaliwa tangu miaka ya 1980 huko hivyo sio kesi kwamba ni ATCL ndiyo inadaiwa, Hapana.Tunaipambania ndege hii kwa maslahi ya Taifa letu na tunaamini siku moja itarudi kuendelea na shughuli zake za kawaida" amesema Dkt. Hassan Abbasi.

Katika maelezo yake Dk Abbas amesema Steyn aliridhia mali hizo kutaifishwa lakini hoja ikaja alipwe fidia kiasi gani.
Amesema ilipofika miaka ya 1990 walikubaliana fidia atakayolipwa, miaka ya 2000 akalipwa na kuna kiasi kilichobaki ambacho mhusika amefungua kesi akitaka amaliziwe kulipwa.
"Ukiangalia awamu zote (za uongozi) kulikuwa na makubaliano, ukiangalia hatua za kimahakama wanakubaliana lakini malipo hayakufanywa lakini yalikuja kufanyika katika awamu ya nne," amesema Dk Abbas.
Dk Abbas amesema mdai huyo amekwenda Afrika Kusini kwa taratibu za mahakama, akibainisha kuwa zipo nchi ambazo mtu anaruhusiwa kuiomba hukumu ya nchi nyingine itekelezwe kwenye nchi aliyopo, akisisitiza kuwa ni taratibu za kawaida kwenye sheria.
"Sisi tunaheshimu utawala wa sheria kwa sababu ni mfumo wa kawaida. Sheria itafuata mkondo wake, ukisoma ile hukumu inaturuhusu kuipinga."
Tayari timu ya wanasheria wakiongozwa na wanasheria Mkuu wa Tanzania Profesa Adelardus Kilangi wapo nchini Afrika Kusini kushughulikia kesi hiyo ili ndege irejee angani.
Tayari Air Tanzania imeshatoa taarifa ya awali na kwa wateja wake na kuomba radhi kuwa kunaweza kutokea usumbufu wa hapa na pale kwenye ratiba ya safari.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 3
Hii ni ndege ya pili ya Tanzania iliyonunuliwa na serikali ya raisi John Magufuli kushikiliwa kutokana na madeni ya nyuma. Ndege ya kwanza kushikiliwa ilikuwa Bombardier Q400-8 iliyozuiwa nchini Canada mwaka 2017.