Kwa picha: Tamasha la mungu wa kike aitwae Osun Osogbo anayeaminiwa kufanikisha uzazi

Tamasha la Osun Osogbo ni utamaduni unaodhaniwa kusherehekewa kwa miaka 600 iliyopita, kwa sasa unaendelea katika jimbo la Kusini - magharibi mwa Nigeria la Osun.

Tamasha hili la wiki mbili linaaminiwa kuwa ndio tamasha kubwa zaidi la mwaka la utamaduni wa kidini la watu wa kabila la Yoruba

Huwavutia waumini na watalii sio kutoka Nigeria tu bali hata maeneo mengine ya dunia

Imani za kitamaduni zinazomuhusisha mungu huyu bado zinaaminiwa kufanyika nchini Nigeria.

Tamasha huadhimishwa kwa densi za kila siki za watu , nyiumbo, ngoma na kuonyeshamavazi ya kumridhisha muungu wa uzazi Osun.

Watumbuizaji wa kundi maarufu la Eyo wakidensi kutoka jimbo la Lagos wanashiriki katika tamasha la mwaka huu.

kivutio kikuu katika tamasha hili ni Arugba, mwanamke bikira ambaye anapaswa kuisaidia jamii kwa kuongoza maombi ya kutoa kafara kwa mto

Arugba, ambaye pia anatambulika kama 'mbeba kibuyu', ana kibuyu kikubwa kichwani kilichofunikwa na kitambaa chenye rangi mbali mbali.

Kibuyu kina kafara kwa ajili ya jamii nzima na zile zilizotolewa na watu waliohudhuria tamasha .

Kila Arugba lazima abakie kuwa bikra kwa muda wote atakapokuwa na jukumu hilo.

Kabla ya kutoa kafara kwenye mto, waamini hutoa sala katika kaburi la muungu.

Wataalamu wa dini za kitamatuni nchini Nigeria wanasema tamasha hili lilianzishwa na waasisi wa mji wa Osogbotakriban miaka 600 iliyopita.

Walikuw ana mpango wa kujenga nyumba zao kwenye kingo za mto, lakini walianza kuangusha miti ndipo roho ya muungu wa mto Osun alipowaabia watoke mahali hapo na akawaamrisha waende mbali.

Eneo hilo limekuwa ni eneo takatifu la kuabudu mzimu huyo tangu wakati huo.

Mwaka 2003, heka 67 zilizobakia za msitu asilia , zilitambuliwa na Unesco kama moja ya maeneo ya turathi za Dunia

Chifu mwenyeji wa tamasha la Oba Jimoh Olanipekun, ambaye cheo chake ni Ataoja wa Osogbo, pia anajukumu kubwa latika tukio. Hapa anatunukiwa na wafalme waliotembelea eneo hilo kutoka miji mingine iliyopo jirani.

Tama hili pia huwavutia wageni kutoka nchi za nje miongoni mwao wakiwemo watalii, huku wengine wakivutiwa na kile wanachokiona kama uhusiano kati ya dini na utamaduni.

"Tuna kikundi kikubwa cha watu wenye shauku kwa ajili ya Orisha nchini Sloveniana maeneo yote ya Yugoslavia ya amani , kwa hiyo wengi miongoni mwa watu hawa wote huja Nigeria kusherehea na Wanaigeria kwasababu wanashirikiana utamaduni unaofanana ... sote tunaabudu utamaduni ," mmoja wa waumini kutoka Slovenia aliiambia BBC.

" Tunafurahishwa sana na tamasha hili na tunapata baraka za Osun hapa,kutoka chanzo chake chenyewe fna tunawashukuru watu wa Nigeria kwa kuwezesha kuwepo kwa mahali hapa kuwa mahala ambapo watalii na waumini wanaweza kufika ."

Wafanyabiasha hutumia fursa ya maelfu ya wageni wanaotembelea mji huu kuuza vipuli nasanamu za kidini.

Wamishonari wa Kiskristo walijaribu kupinga imani za utamaduni huu awakati Nigeria ilipokuwa chini ya ukoloni wa kiingereza.

Taratibu za kidini zilizohusika na ibada ya Orisha wakati huo zilihusisha kafara za binadamu ambazo zilizilisitishwa na mamlaka.

Lakini tangu miaka ya 1980, umaarufu wa tamasha umekuwa ukiongezeka kwa sehemu kubwa kwasababu ya uanaharakati wa Susanne Wenga mzaliwa wa Australia , ambaye alijenga upya kaburi na kuhakikisha libnalindwa

Bi Wenger aliwasili Nigeria miaka ya 1950 ,baadaye alitalikiana na mumewew na akaamua kubakia Osogbo maisha yake yote.

Pia anafahamika kama Adunni Olorisha.

Alifariki dunia mwaka 2009 akiwa na umri wa miaka 93.

Picha zote kwa hisani ya BBC.