Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Picha bora kutoka Afrika: 3-9 Novemba 2017
Mkusanyiko wa picha za kuvutia zaidi kutoka Afrika na kuwahusu Waafrika pande mbalimbali duniani.
Jumapili, Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Welby alikuwepo katika kanisa la Kiangilikana la All Saints, Nairobi. Alikutana na Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa muungano wa upinzani wa National Super Alliance (NASA) Raila Odinga.
Tamasha ya kutubu na kufurahia iliadhimishwa nchini Ivory Coast siku ya Jumamosi...
Jamii ya N'zima wanashiriki tamasha hii iitwayo Abissa au tamasha ya kuuliza swali. Inaitwa hivi kwa sababu wao hujiuliza: Je, jamii ya N'zima inastahili kuuona mwaka mpya?...
Mfalme na mwanawe wanabebwa mjini Grand Bassam...
Wakiwa wamevalia mavazi ya waliowadhulumu mwaka uliopita, wanacheza kwa sauti za chombo cha mziki aina ya tam-tam. Punde makosa yote yamesamehewa, wanafurahia mwaka mpya.
Siku iyo hiyo, Lamoj ambaye ni mwanamziki wa muziki wa Afrobeat alicheza katika maonyesho ya kibiashara jijini Lagos, Nigeria.
Siku ya Jumapili, wakazi wa Zimbabwe wanacheza ngoma katika mkutano wa injili ulitumika kama mkutano wa siasa iliyofanyika mjini Harare...
Wengi wa waliohudhuria walikuwa wakristo wa tabaka mbali mbali...
Mrengo wa vijana wa chama tawala Zanu-PF nao walipanga mkusanyiko huu ili kuonyesha uaminifu wao kwa mke wa Rais Mugabe, Grace Mugabe...
Alikuwepo na mumewe mwenye miaka 93, Rais Robert Mugabe. Bi Mugabe alitoa hotuba kali huku akionekana kuendeleza juhudi za kutaka kuchukua usukani kutoka kwa mumewe.
Jumanne, Moustafa, 15, anabeba nyuzi katika kiwanda kilichosalia pekee katika eneo nzee la mji wa Cairo, Misri...
Salama, 76, mmiliki wa kiwanda hiki alianza kufanya kazi hii akiwa miaka 7 wakati wa utawala wa mfalme Farouk aliyesemekana kuwashika wanaume wote ambao hawakuwa wanafanya kazi.
Sasa zaidi ya miaka 70 baadaye kiwanda hiki ndicho kimesalia pekee eneo la kale la Cairo. Nyuzi hizi hutumiwa kutengeneza kamba za viatu na migodoro.
Salama, 76, mmiliki wa kiwanda hiki alianza kufanya kazi hii akiwa miaka 7.
Wavuvi nchini Libya wanatia nanga katika bandari ya Tripoli, Novemba 3, 2017.
Samaki wauzwa katika soko la samaki mjini Tripoli, Libya Novemba 3, 2017
Picha hii ilipigwa Alhamisi, taipureta iliyo katika maonyesho yaliyofanyika katika jumba la makumbusho la polisi mjini Cape Town, Afrika Kusini.
Jumba hili la makumbusho pia linaonyesha mfano wa jinsi maafisa walivyokuwa karne ya 1913-1957.
Images courtesy of AFP, EPA, PA and Reuters