Ujauzito na sonona: 'Nilihofia kuwa watamchukua mtoto wangu kama nitaeleza hali yangu'

Kipindi ambacho mwandishi wa habari Anna Ceesay alipokuwa mjamzito wa mtoto wake wa pili, alianza kusononeka na kuwa na hofu, lakini ilikuwa ni siri kwa kila mtu hata mume wake ambaye ni muigizaji Babou Caesay.

Mwandishi huyo sasa ameamua kuanza kusaidia wazazi wengine kujua hali zao za afya ya akili.

Kwa mzazi yeyote mwenye watoto wadogo atakwambia kuwa ana muda mdogo sana katika siku kwa ajili yake mwenyewe, lakini muda wowote anaweza kupata kufikiria na kuhisi jambo lingine.

Matatizo ya Anna Ceesay mwenye umri wa miaka 33 yalianza wakati mtoto wake wa kike akiwa na miaka mitatu huku akiwa na mimba ya miezi sita ya mtoto wake wa pili.

"Majira ya alfajiri huwa ninahisi kuwa sio mzima, ninahisi uchovu na kuchanganyikiwa".

"Mara nyingine huwa hali hiyo inaondoka na mara nyingine huwa haiondoki, hivyo kuna siku zilikuwa nzuri zaidi ya nyingine," alisema Anna.

Hali hiyo ya sonona huwa inawakosesha raha, wanakuwa na hofu ya vitu ...lakini kuna wakati kuacha kila kitu huku kuna mengi yanaendelea huwa ngumu.

Caesay alikuwa analea watoto peke yake kwa sababu mume wake alikuwa hayuko, alikuwa anafanya kazi katika nyumba yao iliyopo Bromley , kusini mwa London ambayo ilikuwa inafanyiwa marekebisho.

Hata baada ya marekebisho ya nyumba, dalili za kuchanganyikiwa ziliendelea kumuandama Anna.

"Nilikuwa nina wasiwasi sana haswa nikiwa napika", alisema Anna. "Nilijihisi kuwa ninaenda kuwapa watu sumu katika chakula kila wakati ninapopika mchuzi wa kuku,

licha ya kuwa nilikuwa ninapika kila mwisho wa juma."

"Nilikuwa ninapenda kuangalia maelekezo katika mtandao wa google ninapohitaji kupika kuku kulingana na uzito wa kuku mwenyewe, ingawa nilikuwa ninanunua kiasi hichohicho cha kuku kila wiki.

Nilikuwa ninajiambia kuwa nitakosea na nitawawekea kulisha watu chakula chenye sumu, na kuna mtu atakufa."

Anna alifanikiwa kuficha tatizo lake la sonona kwa kila mtu aliyekuwa karibu yake, akiwemo mume wake, wazazi na rafiki zake.

Yeye mwenyewe tu hakuweza kukubali kuwa ana tatizo.

"Nadhani siko peke yangu , kwa kuwa na hisia kuwa jambo halipo sawa, kuna wakati unajarbu kuliondoa katika akili yako ili maisha yaendelee kama kawaida.

"Ukiwa na watoto wadogo inabidi ujitahidi. Hivyo ilinibidi kuwahudumia watoto kwanza na kujijali mwenyewe ni baadae.

Ilinichukua miezi kadhaa kuanza kufikiria, 'Unajua nini? Siwezi kufanya hili mwenyewe na ninahitaji kupata msaada, na nilivyoamua kufanya hivyo, nilikuwa ninaogopa sana."

Siku moja alipompeleka mtoto wake shule ya awali, Ana aliegemea usukani wa gari na kuanza kuangalia namba ya huduma ya msaada inayotowasaidia watu wanaosumbuliwa na afya ya akili.

Akiwa na miezi nane ya ujauzito, amekuwa akiangalia namba ya huduma wa msaada kwa zaidi ya wiki lakini siku moja alipata ujasiri wa kupiga simu.

"Mara ya kwanza, nilisema neno moja kwa sauti na nilipowapigia namba ya Panda inayotoa msaada kwa wanaotoa huduma kwa wenye matatizo ya afya ya akili kwa ajili ya msaada iliniwia vigumu.

Nilikubali tu kuwa ninahitaji msaada ilikuwa ni hatua ngumu kwangu kwa sababu mimi ni mtu ambaye nina tabia ya kujivunia kuwa nina uhuru na jasiri, hivyo kuomba msaada kwa kitu ambacho sijawahi kufanya kabla iliniwia vigumu".

"Nilivyoweza kuongea na namba hiyo, nilijihisi sina nguvu na ndipo tulipomtaarifu mume wangu ambaye alikuwa mbali hivyo alishtuka sana pia"

Mume alikiri kusema kuwa mfumo wao wa maisha ndio umewafanya kutotatua tatizo kwa wakati.

"Kwanza kwa mtu ambaye nnampenda kufikwa na tatizo hilo, nilipata msongo wa mawazo na kusikitishwa sana.Kwa haraka ilinibidi nirudi nyumbani haraka niwezavyo," mume wake alieleza.

Anasema wakati huo ndio kipindi ambacho ilimbidi awe mkimya na kusikiliza kila ambacho Anna alikuwa anasema.

"Ilikuwa ni mshtuko mkubwa sana kwangu na halikuwa jambo rahisi kukabiliana nalo"

Matatizo ya afya ya akili wakati na baada ya ujauzito

Profesa Lorraine Sherr, ambaye ni mwanasaikolojia wa chuo kimoja mjini London anasema ujauzito unaweza kusababisha matatizo ya afya ya akili au kuchochea yaliyokuepo,

Dalili zake ni pamoja na majonzi , kukosa usingizi na uchovu wa viungo na kadhalika.

Alisema kuwa jambo la muhimu la kufanya unapokumbana na tatizo la afya ya akili ni kuzungumza na watu na sio kubaki nayo hiyo hali mwenyewe , tafuta msaada kwa wataalamu wa afya.

"Kawaida ukipata jeraha unaenda kutafuta usaidizi, ni sawa na ukipata tatizo la akili unapaswa kufanya hivyo"

Anna anasema alipata fundisho kubwa la namna fikra zake hazipaswi kumsukuma kufanya maamuzi. Lazima ziweze kukabiliwa.

Kwa upande wake Babou anasema, alijihisi kuwa hana msaada lakini ulikuwa wakati ambao mke wake alimuhitaji zaidi.

Anna anasema alipofikiria kila kitu anaona kuwa mume wake alikuwa msaada mkubwa kwake na muelewa.

Kuna unyanyapaa mkubwa katika tatizo la afya ya akili, lakini jamii inapaswa kuelewa tatizo na kuwasaidia wanawake wajawazito wanapokumbana na tatizo hilo.