Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Operesheni Dragoon: Jinsi vikosi vya Afrika vilivyoongoza mapambano Vita Vikuu vya pili vya Dunia
Huenda hujawahi kusikia lakini Oparesheni Dragoon - ilifanyika miaka 75 iliyopita - ili kuikomboa Ufaransa.
Ilihusisha majeshi ya muungano kutoka mataifa ya Ufaransa, Marekani, Canada na vikosi vya Uingereza.
Operesheni hiyo ilisaidia kukomesha Vita Vikuu vya Pili vya Dunia na wanajeshi wengi wa Afrika walishiriki vita hivyo.
Operesheni hiyo ilifanyika siku ambayo majeshi ya Ufaransa na washirika wake walishambulia vikosi vya Ujerumani iliyokuwa chini ya utawala wa kidikteta wa Adolph Hittler.
Agost 15, miezi miwili baada ya moja ya mzozo mkubwa zaidi wa kivita kushudiwa duniani wanajeshi walichukuliwa na Ufaransa kutoka sehemu mbali mbali katika juhudi ya kuisaidia kukabiliana na uvamizi wa wanajeshi wa Ujerumani.
Jina lake fiche lilikuwa ''Operation Dragoon'' na ukumbusho wake mpaka leo unasherehekewa kila mwaka na viongozi wa mataifa ya Afrika
Mwaka huu Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliwaalika marais wa Ivory Coast na wa Guinea, Alassane Ouattara na mwenzake Alpha Conde.
Wanajeshi kutoka makoloni ya Ufaransa za Kiafrika walichangia thuluthi mbili ya jeshi la Ufaransa mwaka 1944 - baada ya taifa hilo kupata hasara kubwa kwa kuvamiwa na Ujerumani mwaka 1940 .
"Wanajeshi wa (Kifaransa) waliotua Kusini mwa Ufaransa walitoka mataifa ya Kaskazini mwa Afrika," mwanahistoria wa Kifaransa Raffael Scheck aliiambia BBC.
Inakadiriwa kuwa zaidi ya wanajeshi milioni moja wa Kiafrika walishiriki Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.
Awali ilipangiwa kufanywa siku ya Kuu ya kukomboa Ulaya kutoka kwa Wanazi wa Ujerumani kaskazini mwa Ufaransa Juni tarehe sita mwaka 1944, na Operesheni ya Dragoon ilifutiliwa mbali kwa kukosa nguvu kazi.
Hata hivyo mkakati wa kuwarudisha nyuma wanajeshi wa Ujerumani ulikwama.
Lengo lilikuwa kukomboa bandari za Ufaransa katika bahari ya Mediterrania, ambayo pia ingelisababisha vita na kuwaongezea presha Wajerumani.
"Vikosi vya Ufaransa vilishiriki katika oparesheni ya kukomboa miji ya bandari ya Toulon na Marseille," Scheck alielezea.
"Vikosi hivyo vilikuwa na changamoto kubwa ya mahali pa kutia meli nanga na pa kutua ndege zake kwa hiyo walifanya kila juhudi kuhakikisha wanafikia lengo hilo."
Lakini oparesheni ya Dragoon iliwafanya wanajeshi Ungereza na Ufaransa kutofautiana sana.
Uingereza ilipinga hatua nyingine uvamizi wa Ufaransa na badala yake ilitaka ijikite zaidi katika oparesheni ya pamoja nchini Italia.
Lakini tamaa ya Ufaransa kutaka nafasi zaidi ilishinda siku na kuendelea mbele na azma yake.
Mwisho mzuri
Kwa mujibu wa nyaraka za jeshi la Marekani, operesheni hiyo ilijumuisha zaidi ya wanajeshi 500,000 na karibu 230,000 kati yao walikuwa raia wa Ufaransa.
Mashambulizi yalifanywa kwa urahisi zaidi ya vita vya kwanza kwa sababu Ujerumani ilikuwa imelemazwa kutokana na shambulio la awali.
Huku operesheni ya ''Overlord'' ikichukua miezi miwili na wiki tatu kukamilika , ile ya Dragoon iliendelea kwa zaidi ya mwezi mmoja.
Ilisadikiwa kuwa oparesheni iliyopata ufanisi mkubwa kwasababu vikosi vya Ufaransa vilikomboa : Bandari zaidi, na washirika waliweza kupeleka vyakula na wanajeshi zaidi kupigana dhidi ya ukombozi wavamizi Ulaya.
Kwa mwanahistoria wa vita nchini Uingereza Antony Beevor, hatua hiyo ilisaidia kuvunja uvamizi wa Ujerumani nchini Ufaransa.
Wakosoaji hata hivyo wanasema nguvu kazi iliyotumika katika uvamizi wa pili ilikuwa na athari ya moja kwa iliyosababisha vita baridi.
'Deni la damu iliyomwagika'
Wanasema vikosi hivyo vingelitumiwa kuzuia muungano wa Soviet kujiimarisha Mashariki mwa Ulaya.
Mawasiliano kati ya viongozi wa Uingereza na Marekani yanaonesha Waziri mkuu Winston Churchill na kamanda mkuu wa jeshi la muungano Dwight Eisenhower, walitofautiana kuhusu oparesheni hiyo.
Hata hivyo George Marshall, mkuu wa utumishi wa umma wa marais wawili wa Marekani wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia (Franklin D. Roosevelt na Harry Truman) baadaye alinukuliwa akisema ilikuwa "moja ya uparesheni iliyopata ufanisi mkubwa na jambo la maana tulilofanya".
Lakini huenda jukumu lililotekelezwa na majeshi wa kiafrika nchini Ufaransa wakati wa vita vikuu vya pili vya Dunia limesahaulika.
Wanajeshi wa Afrika waliondolewa nchini humo na serikali ya mpito kufikia mwisho wa mwaka 1944.
"Ufaransa iliamua jeshi lake liwe na wazungu pekee. Kwa hivyo ilichukua sare za kijeshi kutoka kwa wanajeshi weusi na kukabiliana na wale walipinga hatua hiyo," Raffael Scheck aliongeza kusema.
"Iliwaacha wengi wao na machungu."
Mamlaka nchini Ufaransa ziliongezea utata suala hilo kuanzia mwaka 1959 kundelea mbele, baada ya mataifa yaliyokuwa makoloni yake kupata uhuru, malipo ya uzeeni ya wanajeshi hao hayakuongezwa hadi mwaka 2010.
Lakini mwaka 2017, rais wa Ufaransa Francois Hollande alikiri kuwa taifa hilo lina wajibu wa ''kufidia damu'' ya mashujaa wa Afrika.
"Ukitafakari ukombozi wa Ufaransa, taswira ya kwanza inayokujia akilini ni picha ya mji wa Paris ukikombiolewa kutoka kwa vikosi vya Wanazi au afisa wajeshi la Marekani akiwa ndani ya gari la kivita ," alisema mwandishi wa habari wa Ufaransa Audrey Pulvar, ambaye alishiriki kampeini ya utambulisho wa jukumu la wanajeshi wa Afrika katika vita vya ukombozi.
"Hujipati ukifikiria kuwa vikosi vya makoloni ya ufaransa vilkomboa mji wa Marseille. Wakati umewadia kwa Ufaransa kuwajumuisha wanajeshi hawa katika kumbukumbu ya pamoja ya historia yake".