Hillsong: Kanisa la matamasha ya muziki wa rock na wafuasi milioni 2

Tamasha la kanisa la Hillsong

Chanzo cha picha, HOLLY HONDERICH

Maelezo ya picha, Tamasha la kanisa la Hillsong

Wakati ambapo idadi ya watu wanaoenda makanisani inaendelea kupungua kote nchini Marekani, kuna kanisa moja ambalo limejizatiti vilivyo kubadili dhana hiyo.

Lakini mtindo unaotumiwa na kanisa hilo linalofahamika kama Hillsong umezua gumzo na baadhi ya watu wanauliza ikiwa linafanya biashara ama linawapa chakula cha kiroho wafuasi wake?

Wafuasi wa kanisa hilo hutumbuizwa kwa matamasha ya kila aina ambayo yanahusisha muziki wa mtindo wa rock huku mavazi yao piwa yakiwa ni ya kisasa, tisheti na jinzi za kubana.

Ukihudhuria tamasha la kanisa la Hilsong utadhani umefika ukumbi wa burudani, kadri muziki unavyoshika kasi ndivyo kila mmoja anarusha mikono juu na kuimba nyimbo inayopigwa jukuwaani na bendi ya kanisa.

Kwa wale wasiojua kuimba maneno ya nyimbo hiyo , maandishi yake yanawekwa kwenye runinga kubwa imbayo inaangaza kanisani kote.

Sauti ya ala ya muziki hupanda na kushuka kuwapa nafasi watu kuimba utadhani ni tamasha la muziki la bendi maarufu ya vijana wa London Mumford and Sons.

Bendi ya Hillsong United, huuza nyimbo zake kwa mashabiki wake katika barabara za mjini wa Washington.

Inajumuisha wanachama kumi waliovalia: jeans ya kubana, T-shirts kubwa kupita kiasa na waliochorwa tattoo.

Muonekano wao unawavutia vijana wengi kujaa katika kanisa hilo.

Bendi ya Hillsong United ikitumbuiza mashabiki wa Washington katika ukumbi was waterfront venue

Chanzo cha picha, HOLLY HONDERICH

Maelezo ya picha, Bendi ya Hillsong United ikitumbuiza mashabiki wa Washington katika ukumbi was waterfront venue

Tofauti na matamasha yalioandaliwa na wanamuziki kama Billie Eilish, ambaye alitumia ukumbi huo siku chache zilizopita, wanaohudhuria tamasha la Hillsong United hawatumii vileo.

Kwanza hakuna pombe inayouzwa katika ukumbi huo na picha zinazoonesha vileo haziruhusiwi.

Pili kuna baadhi ya vijana wa kanisa wanaochangisha pesa na la tatu ni kwamba kuna msalaba wa CGI ambao umewashwa jukwaani hapo kuashiria tamasha linaloendelea ni la kidini.

Hili sio tamasha la kawaida ni ibada ya kanisa .

Wafuasi maarufu

Bendi ya Hillsong United, ni kiungo muhimu kwa kanisa la Hillsong ambalo lilanzishwa na wanandoa Brian na Bobbie Houston mjini Sydney, Australia, mwaka 1983, na kanisa hilo limepata ufuasi mkubwa katika mataifa tofauti duniani.

Linapatikana katika mabara sita katika miji 23 na kila Jumapili huwavutia karibu wafuasi 130,000 ambao wanahudhuria ibda ya kanisa la Hillsong duniani .

Hillsong inajivunia kuwa wafuasi maarufu kama vile: Justin Bieber na mke wake, Hailey Baldwin Bieber.

Hillsong imewavutia watu maarufu kama vile Kevin Durant, Hailey Baldwin na Chris Pratt

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Hillsong imewavutia watu maarufu kama vile Kevin Durant, Hailey Baldwin na Chris Pratt

Wachezaji wa NBA Kevin Durant na Kyrie wamekuwa wakitafuta ushauri wa kidini kutoka kwa mchungaji mkuu wa kanisa la Hillsong tawi la New York, Carl Lentz.

Wengine ni Chris Pratt, Kylie Jenner na Kourtney Kardashian ambao wana uhusiano wa karibu na kanisa hilo.

Hillsong hata hivyo walikataa ombi la kuhojiwa.

"Kwa sasa ni kanisa maarufu sana," alisema Mack Brock, ambaye alihudhuria tamasha la Hillsong, Amerika Kusini mwaka huu.

Hillsong liinajiita "kanisa la kisasa, "ambalo lengo lake ni kuhubiri neno la mungu kote duniani".

Ujumbe huo unapitishwa kupitia bendi yake maarufu ya Hillsong United.

Msanii wa muziki

Chanzo cha picha, Getty Images

Kufikia sasa Kanisa la Hillsong linajivunia kumiliki taasisi mbili za masomo (moja mjini Sydney na nyingine mjini Phoenix, Arizona), kongamano kuu la kila mwaka, na kituo cha televisheni kinachopeperusha matangazo yake saa 24, mikakati ya kijamii na pia lebo ya muziki.

Bendi ya Hillsong United inatajwa kuwa maraarufu zaidi na inawafikia watu wengi hususan vijana.

Bendi hiyo ina zaidi ya mashabiki milioni 2 katika mtandao wa kijamii wa Instagram,na wengine milioni 1.5 kutoka kwa wanachama wake 10.

Nyimbo zao zinasikilizwa na karibu watu milioni 3.5 kwa wiki katika mtandao wa muziki wa Spotify.

Mashabiki hao ni karibu mara mbili ya mashabiki wa kituo maarufu cha waumini wa dini ya Kikristo.

Nyimbo yao maarufu hadi wa leo inafahamika kama, Oceans, ambao umechezwa zaidi ya mara milioni 155 katika Spotify pekee.

Hii inamaanisha umechezwa mara mbili zaidi ya wimbo wa hivi karibu uliimbwa na Billie Eilish akimshirikisha Justin Bieber.

Mack Brock ametumbuiza katika matamasha zidi ya 30 Amerika Kaskazini

Chanzo cha picha, FACEBOOK/MACK BROCK

Maelezo ya picha, Mack Brock ametumbuiza katika matamasha zidi ya 30 Amerika Kaskazini

Hillsong inaongoza "katika muziki wa kanisa" Brock anasema. "Nadhani ni wao wanaofanya kazi nzuri."

Kuongezeka kwa umaarufu wa Hillsong, ni jambo la kupigiwa mfano hasa ikizingatiwa kuwa idadi ya watu wanaoenda kanisani imepungua kote duniani.

Kwa miaka kadhaa idadi ya watu wanaoenda kanisa nchini Marekani imeendelea kushuka, sambamba na wale ambao hawajihusishi na dini yoyote.

Kwa kipindi cha miaka saba- 2007 hadi 2014 - idadi ya waumini wa dini ya Kikristoimeshuka kwa 8%.

Idadi kubwa ya watu waliojumuishwa katika hiyo 8% ni vijana ambao sasa wanavutiwa na kanisa la Hillsong.

Uhusiano uliopo kati ya Ukristo na muziki wa rock sio jambo geni lakini kutokana na ufuasi mkubwa wa vijana katika kanisa Hillsong huenda mtindo huo wa muziki ukapata umaarufu zaidi.

Jonathon Douglass, Matt Crocker, Taya Smith and Joel Houston of Hillsong United discuss their multi-platinum album, "People" at Build Studio in April in New York

Chanzo cha picha, Image copyrightNICHOLAS HUNT/GETTY IMAGES

Tamasha la kanisa hilo la kukutana na watu Amerika Kaskazini linajumuisha miji 30 nchini Marekani na Canada.

Mwezi Novemba mwaka huu wanatarajiwa kuelekea Amerika ya Kusini katika tamasha la ibada litakalowatumbuiza watu nchi Brazil, Argentina na Peru.

''Hatua ya kuwatembelea wafuasi wetu walipo ni sehemu ya lengo letu kuu'' alisema mmoja wa waandalizi wa safari hizo.

Ibada ya kanisa la Hillsong huhudhuriwa na watu ambao wanaweza kujaza ukumbi wa burudani wa Hammerstein mjini Manhattan.

Brock na wafuasi wengine wa kanisa hilo wanapinga madai kuwa mtindo wa mavazi wa viongozi wa kanisa hilo inaegemea zaidi malengo ya kibiashara.

Lakini kinachovutia zaidi ni muonekano wa mavazi ya wafuasi wa kanisa hilo.

Wanachama wa bendi wanavalia nguo ambayo vijana wa kisasa wangelipendelea kuvaa na muonekano wao ni wa marafiki zao katika mtandao wa I Instagram.

"Wanaenda na wakati," anasema Joe Adevai, aliysomea chuo cha Hillsong mjini Sydney kabla ya kuwa kiongozi wa kanisa hilo mjini New Jersey.

Aliongezea kuwa "Wanaenda na utamaduni wa wa kisasa,". "Unawezaje kuvalia mitindo ya mavazi ya kisasa na uwe Mkristo?" wengine waliuliza

Licha ya hayo yote Hillsong ni kanisa kama makanisa mengine duniani lakini viongozi wake wameamua kuwavutia wafuasi ambao hawataki kuhukumiwa kutokana na mtindo wao wa maisha.

.