Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Teodoro Obiang Nguema: Rais wa Equatorial Guinea atimiza miaka 40 madarakani
Rais wa Equatorial Guinea ,Teodoro Obiang Nguema Leo (Jumamosi) anasherehekea miaka 40 madarakani na kuwa kiongozi wa Afrika aliyepo madarakani kwa mda mrefu zaidi zaidi.
Obiang Nguema alichukuwa hatamu ya uongozi wa nchi hiyo kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka 1979.
Makundi ya kutetea haki za binadamu yamemtaja Obiang Nguema, aliye na miaka 77, kuwa kiongozi katili, mfisadi na wa kiimla zaidi barani Afrika.
Katika uchaguzi wa mwaka 2016 alishinda uchaguzi wa Urais kwa 90%, kwa mujibu wa matokea yaliyotangazwa rasmi na Tume ya Uchaguzi.
Sherehe yake ya kuadhimisha miaka 40 madarakani zinafanyika katika miji mitatu mikuu ikiwa ni pamoja na mji wa kiuchumi wa Bata,Mongomo, nyumbani kwa rais na Djibloho -- mji mpya uliyojengwa katikati ya msitu kutokana na fesha za mauzo ya mafuta.
Shirika Amnesty International mwezi uliyopita lilitoa wito kwa serikali ya Obiang Nguema kuchukua hatua za "kuheshimu, kulinda, na kudumisha haki za binadamu kote nchini humo".
Lakini wakosoaji wanasema hakuna ishara kuwa Equatorial Guinea itazingatia wito huo.
Obiang Nguema ambaye ameponea mapinduzi kadhaa ya kijeshi amekuwa akikabiliana vikali na wapinzani wake na wale waliowahi kupanga njama ya kumg'oa madarakani katika taifa hilo lililokuwa koloni ya Uhispania.
Upinzani
Mwezi Disemba mwaka 2017, serikali iliripoti madai ya kutibua jaribio la mapinduzi lililopangwa na wapinzani wake waliotorokea mataifa ya kigeni the government reported thwarting a coup allegedly orchestrated by foreign exiles.
Mwezi Juni mwaka huu, watu 130 waliohusika na jaribio hilo la mapinduzi walihukumiwa kifungo cha miaka 96 jela.
Chama kikuu cha upinzani Citizens for Innovation (CI), kilipigwa marufuku na mamlaka kuendesha shughuli zake mwezi Februari mwaka 2018.
Wanachama 21 CI, ikiwemo mbunge pekee wa chama hicho walihukumiwa miaka 30 jela kwa kosa la kusababisha "vurugu na kushambulia maafisa wa serikali".
Mrithi wake
Obiang Nguema anaaminiwa kumuandaa mwanawe wa kiume, Teodorin, kumrithi atakapoachia urais wa nchi hiyo.
Teodorin alipandishwa cheo na kuwa makamu wa rais mwaka 2016 na pia anasimamia idara ya ulinzi na usalama.
Kutokana na mienendo yake kupenda anasa, Teodorin alihukumiwa kifungo cha nje cha miaka mitatu na mahama moja mjini Paris baada ya kupatikana na kosa la utumiaji mbaya wa fedha za umma kununua mali nchini Ufaransa.
Alituhumiwa kwa kutumia zaidi ya mara 1,000 mshahara wake rasmi kujenga jumba la kifahari katika mji mkuu wa Ufaransa pamoja na magari ya kifahari miongoni mwa mali zingine za thamani .
Pia alipigwa faini ya euro milioni 30 sawa na ($33.5 milioni) na mahakama hiyo.
Mwaka 2019, waendesha mashtaka wa Uswizi walimuondolea Teodorin, mashtaka ya uhalifu wa kiuchumi lakini walizuilia magari yake 25 ya kifahari kama dhamana ya kesi hiyo.
Mwezi Oktoba mwaka jana, alipandishwa cheo cha Kanali mkuu wa jeshi bila kupitia nyadhifa zingine kama brigedia mkuu wa jeshi.
Mwezi uliyofuata aliongoza mkutano wa baraza la mawaziri kwa mara ya kwanza.
Ufisadi
Taifa hilo dogo la Afrika Magharibi ni mzalishaji mkubwa wa mafuta na lina idadi ya watu milioni 1.2.
Equatorial Guinea ilianza kuuza mafuta yake kimataifa mwaka 1995 tangu wakati huo taifa hilo limesifika kwa kuwa na kiwango cha juu pato jumla la serikali.
Taifa hilo hata hiyo limetajwa mara kadhaa limetajwa kuwa fisadi zaidi duniani na mashirika yasiokuwa ya kiserikali
Mwaka 2018 liliorodheshwa na Umoja wa Mataifa katika nafasi ya 141 kati ya mataifa 189 katika udumishaji wa haki za binadamu.
Shirika la Transparency International liliorodhesha nchi hiyo katika nafasi ya 172 kati ya mataifa 180 kuhusiana na masuala ya rushwa.
Rais Obiang Nguema mara kadhaa amenukiliwa akisema kuwa ripoti hizo ni ukosoaji wa mataifa ya ''Magharibi'' dhidi ya nchi yake
Lakini je, wajua ni viongozi gani wa sasa wameongoza mataifa yao kwa muda mrefu zaidi Afrika?
- Miaka 39: Jose Eduardo dos Santos - Angola, alichukua uongozi baada ya kifo cha rais wa kwanza wa taifa hilo Agostinho Neto Septemba 1979
- Miaka 38: Robert Mugabe - Zimbabwe, alishinda uchaguzi wakati wa kujinyakulia uhuru kwa taifa hilo Aprili 1980 hadi alipoango'lewe madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi.
- Miaka 37: Paul Biya - Cameroon, alichukua uongozi baada ya kujiuzulu kwa rais wa kwanza wa nchi hiyo Ahmadou Ahidjo, Novemba 1982
- Miaka 38: Denis Sassou Nguesso - Congo, aliwekwa uongozini na jeshi mwezi Oktoba 1979 na akaongoza hadi mwezi Agosti 1992. Alirejea tena Oktoba 1997 na kuendelea hadi sasa.
- Miaka 37: Yoweri Museveni - Uganda, alichukua uongozi rais baada ya kundi lake la waasi kuchukua madaraka mwezi Januari 1986