Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ni azimio gani lililofikiwa kati ya Jeshi la Sudani na upinzani?
Baraza la utawala la kijeshi la Sudan na Muungano mkuu wa upinzani wameafikiana juu ya azimio la katiba llitalotoa fursa ya kipindi kipya cha serikali ya mpito.
Mpatanishi wa Muungano wa Afrika Mohamed Hassan Lebatt ametoa tangazo la makubaliano hayo mapema Jumamosi asubuhi, lakini kutoa maelezo zaidi
Sudan imekuwa katika limbo la ghasia tangu jeshi lilipomg'oa madarakani rais Omar al-Bashir mwezi Aprili.
Mazungumzo yaliyochukua muda mrefu juu ya azimio yamekuwa yakifanyika huku ghasia zikiendelea.
Mkataba wa azimio lililosubiriwa kwa muda mrefu umeibua sherehe katika nchi ya Sudan , ambayo imekuwa katika limbo la mzozo uliodumu kwa miezi kadhaa.
Maandamano yaliibuka mwezi Decemba baada ya serikali ya Bashir kutangaza hali ya dharura ya hatua za kuunusuru uchumi . Aliondolewa mamlakani na jeshi mwezi April baada ya maandamano ya muda mrefu nje ya wizara ya ulinzi mjini Khartoum.
Maandamano hayo yamekuwa ya kutaka mamlaka yahamishiwe mikononi mwa raia.
Azimio linasema nini?
Waraka unaaainisha masharti ya kipindi cha miaka mitatu cha mpito yalikubaliwa mwezi uliopita na baraza la jeshi na viongozi wa upinzani.
Mkataba wa kugawana madaraka ulielezea kuwepo kwa serikali ya raia sita na majenerali watano
"Ninatangaza kwa Wasudan , Waafrika na umma wa kimataifa kwamba wajumbe wa pande mbili wamekubaliana kwa ukamilifu juu ya azimio la katiba ," Lebatt amewaambia waandishi wa habari. Jumamosi.
Aliongeza kusema kuwa mikutano zaidi itafanyika kushughulikia masuala ya kiufundi ya sherehe ya kusaini, lakini hakutoa taarifa juu ya makubaliano yenyewe.
Muswada wa azimio ulioangaliwa na shirika la habari la Reuters ulisema kuwa kikosi cha uingiliaji kati wa haraka -Rapid Support Forces (RSF), ambacho kimekuwa kikishutumiwa kwa kuwauwa waandamanaji, sasa kitakuwa chini ya utawala wa jumla wa kijeshi , na huduma za ujasusi zitaongozwa na baraza la uongozi pamoja na baraza la mawaziri kwa ujumla.
Mkataba juu ya azimio unakuja baada ya baraza la kijeshi kutangaza kwama wanajeshi wa RSF walikuwa wamefutwa kazi na kukamatwa kuhusiana na mauaji ya waandamanaji , wakiwemo watoto wanne wa shule waliouawa wiki hii.
Mauaji yaliibua maandamano makubwa kote nchini humo na kusababisha kuchelewa kwa mazungumzo.
Tunafahamu nini juu ya kipindi cha mpito?
- Jeshi na waandamanaji wamefikia makubaliano kadhaa, huku kila upande ukiongeza maelezo zaidi huku wakijaribu kuondoa hali ya kutoaminiana na kujenga uhusiano wa kikazi.
- Hadi kufikia sasa wamekubaliana yafuatayo:
- Mgawanyo wa mamlaka utadumu kwa miezi 39
- Baraza la huru, baraza la mawaziri na bunge vitaundwa
- Jenerali ataongoza baraza kwa miezi ya kwanza 21, na raia ataongoza miezi 18 iliyosalia.
- Waziri mkuu , atakayeteuliwa na vuguvugu linalounga mkono demokrasia, ataongoza baraza la mawaziri
- Tmawaziri wa ulinzi na wa mambo ya ndani watachaguliwa na jeshi
Kipindi kirefu cha mpito kinaonekana kama ushindi kwa vuguvugu linalounga mkono demokrasia -majenerali walikuwa wametishia kuitisha uchaguzi wa haraka baada ya kamata kama ya 3 Juni
Waandamanaji wanadai utawala wa Bwana Bashir ulikuwa umekita mizizi sana na kwamba itachukua muda kuvunja mitandao yake ya kisiasa na kufungua njia ya uchaguzi huru na wa haki.