Marekani yamuekea vikwazo waziri wa mambo ya nje Iran Mohammad Javad Zarif

Chanzo cha picha, Reuters
Wizara ya fedha Marekani imemuekea vikwazo waziri wa mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif.
Vikwazo hivyo vinazuia mali yote aliyonayo Zarif Marekani, idara hiyo imeeleza.
"Javad Zarif anaidhinisha ajenda mbovu ya kiongozi mkuu wa Iran (Ayatollah Ali Khamenei)," Waziri wa fedha Steven Mnuchin amesema.
Zarif alituma ujumbe kwenye mtandao wa Twitter kuwa Marekani imemuekea vikwazo kwasababu inamuona kama tishio kwa ajenda yake.
Wasiwasi kati ya Marekani na Iran umeongezeka tangu Marekani kujitoa mwaka jana katika mkataba wa nyuklia mnamo 2015 ulionuia kuistisha shughuli za utengenezaji nyuklia Iran.
Kuna wasiwasi unaoongezeka kuwa idadi ya visa vya hivi karibuni katika ghuba huenda vikachangia kuzuka mzozo wa kijeshi katika enoe hilo muhimu la ubaharia.
Siku ya Jumatano, Marekani iliongeza muda wa marufuku ya fursa inayoruhusu Urusi China na mataifa ya Ulaya kuendelea ushirikiano wa kiraia wa nyuklia na Iran.
Mshauri wa usalama katika ikulu ya Marekani John Bolton amesema muda huo "umeongezwa kwa ufupi wa siku 90".
"Nadhani fikra hapa ni kutazama kwa makini na ukaribu shughuli hizo za nyuklia," aliongeza.
Marekani imesema nini?
Mnuchin amemtaja Zarif kama "msemaji mkuu wa utawala wa Iran duniani".
"Marekani inatuma ujumbe wa wazi kwa utawal awa Iran kwamba tabia yake ya hivi karibuni haikubaliki kabisa.
"Wakati huo huo utawala wa Iran unawanyima raia wake uhuru wa kuingia katika mitandao ya kijamii, Waziri wa nje Javad Zarif anasambaza propaganda na habari zisizo za kweli duniani kupitia jukwaa hilo,," Bwana Mnuchin ameongeza.
Zarif amejibu nini?
Zarif amesema hatua ya Marekani "haimuathiri yeye wala familia yake, kwasababu sina mali au faida zozote nje ya Iran".
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
"Sababu ya Marekani kunilenga mimi ni kuwa mimi ndiye 'msemaji mkuu wa Iran duniani . Ukweli ni uchungu kiasi hicho?" ameuliza.
"Asante kwa kunichukulia mimi kuwa tishio kubwa kwa ajenda yenu."
Kwanini kuna uhasama baina ya Marekani na Iran?
Hali ya uhasama kati ya Marekani na Iran ilianza zamani wakati wa mapinduzi ya Iran mnamo mwaka 1979, ambapo kiongozi aliyependelewa na nchi za magharibi Shah na kuanzishwa kwa utawala uliochukia Marekani kuchukua mamlaka.
Rais Trump amechukua msimamo mkali dhidi ya Iran tangu alipoingia madarakani mwaka 2016.
Utawala wake unataka kuanzisha upya mazungumzo ya mkataba wa nyuklia na kupanua mapendekezo yake zaidi ili pia ikabiliane na mpango wa makombora ya masafa marefu ya Iran ya na "kudhibiti " shughuli za kijeshi katika eneo zima la Mashariki ya Kati.
Vipi kuhusu mkataba huo wa nyuklia 2015?
Mwaka jana Marekani ilijitoa katika mkataba huo wa makubaliano kati ya Iran na mataifa yenye nguvu duniani.
Washington tangu hapo imeidhinisha vikwazo vikali vinavyouathiri uchumi wa nchi na pia washirika wengine wa makubaliano hayo ya 2015 - China, Ufaransa Ujerumani na Urusi pamoja na Uingereza zilizoishutumu uamuzi wa Trump na kusema wanaendelea kuuwajibika kikamilifu mkataba huo.
Iran ilijibu kwa kukiuka viwango vilivyoorodheshwa vya urutubishaji wa madini ya uranium chini ya mkataba huo.
Mnamo Mei Tehran ilishinikiza utengenezaji wa madini hayo yanayoweza kutumika katika kuunda silaha za nyuklia.
Wiki iliyopita mazungumzo yalifanyika Vienna kujaribu kuokoa mkataba huo.
Baada ya mkutano na wawakilishi kutoka Uingereza, Ufaransa Ujerumani Urusi na China, afisa mkuu wa Iran amesema mazungumzo yalikuwa katika 'mazingira mazuri'.














