Mgogoro kati ya Marekani na Iran: Marekani kubuni jeshi la nchi washirika kulinda maji ya Ghuba na Yemen

Jenerali Dunford katika mkutano na vyombo vya habari nba rais Trump

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jenerali Dunford katika mkutano na vyombo vya habari nba rais Trump

Jenerali mmoja mkuu amesema kuwa Marekani inataka kubuni muungano wa jeshi kulinda maji yaliopo Iran na Yemen.

Jenerali huyo wa jeshi la wanamaji Joseph Dunford amsema kuwa anataka kuhakikisha kuwa kuna uhuru wa uchukuzi wa majini katika eneo hilo ambalo lina njia muhimu zinazotumika kibiashara.

Mwezi Uliopita Marekani iliwalaumu wapiganaji wanaoungwa mkono na Iran kwa mashambulio dhidi ya meli mbili za kubeba mafuta.

Jenerali Dunford alisema kuwa Marekani imeanza mazungumzo na baadhi ya mataifa washirika ambao wana uwezo wa kuunga mkono pendekezo hilo.

Marekani itatoa meli za kuweka usalama katika maji hayo lakini mataifa mengine yatahitajika kutoa boti zitakazopiga doria katika meli hizo.

Jenerali Dunford amasema kuwa Marekani itashirikiana na majeshi ili kubaini uwezo wa kila taifa ili kuunga mkono mpango huo.

Mkondo wa bahari wa Hormuz na eneo la Bab al-Mandab ni muhimu kwa uchukuzi wa majini kwa kuwa maeneo hayo hutumika kama mlango wa kutoka bahari kuu kuingia katika Ghuba na bahari nyekundu.

Map of the Straits of Hormuz and Bab al-Mandab

Jenerali huyo alisema kuwa kiwango cha mpango huo kinategemea idadi ya mataifa yatakayoshiriki.

''Tukipata idadi ndogo ya mataifa washirika tunaweza kubuni kikosi kidogo'' , alsema.

Tutaongeza kikosi hicho iwapo mataifa yanayotaka kushiriki yatajitambulisha.

Kila siku takriban mapipa milioni nne ya mafuta hupitia katika eneo la Bab-al Mandab hadi maeneo mengine ya dunia .

Ni kwa nini Marekani ina wasiwasi kuhusu uchukuzi wa meli?

Marekani imeishutumu Iran kwa kushamblia meli mbili za mafuta kwa kutumia mabomu ya ardhini mnamo mwezi Juni , nje kidogo katika mkondo wa bahari wa Hormuz - madai ambayo Iran imekana.

Siku chache baadaye , ndege isio na rubani ilitunguliwa na vikosi vya Iran katika Ghuba.

Iran ilisema kuwa ndege hiyo ilikiuka anga ya Iran na ikatuma ujumbe mkali kwa Marekani.

Marekani ilisisitiza kuwa ndege hiyo ilikuwa juu ya anga ya maji ya kimataifa .

Rais Trump alituma ujumbe wa twitter akisema: Iran ilifanya makosa makubwa sana.

Marekani ilikuwa imepanga kutekeleza mashambulizi ya kulipiza kisasi lakini baadaye ikafutilia mbali mpango huo.

Iran imesema kuwa itaufunga mkondo wa Hormuz iwapo itazuia kuuza mafuta , kikwazo ambacho rais wa Marekani Donald trump ametishia kuliwekea taifa hilo iwapo halitakubali kuanzisha upya makubaliano ya mpango wake wa kinyuklia.

''Iran haitaki vita na taifa lolote, lakini iko tayari kujilinda '', alisema meja jenerali Hossein Salami, kiongozi mkuu wa jeshi la Iran IRGC baada ya ndege hiyo kutunguliwa.

Kumekuwa na hali ya wasiwasi kati ya Uingereza na Iran , baada ya Uingereza kusema kuwa utawalka wa Iran ndio uliohusika na shambulio la meli mbili za mafuta mnamo mwezi Juni.

Presentational grey line