Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
NeuraLink: Kampuni ilioanzishwa na Elon Musk ina mipango ya kudukua ubongo wa mwanadamu
NeuraLink, kampuni ilioanzishwa na Elon Musk ili kutafuta mbinu za kuunganisha ubongo wa mwanadamu na tarakilishi imewasilisha ombi kwa wadhibiti wa Marekani kuanza kupima kifaa chake miongoni mw awanadamu.
Mfumo huo umejaribiwa katika tumbili ambaye aliweza kudhibiti tarakilishi na ubongo wake kulingana na bwana Musk.
Kampuni hyo ilikuwa inalenga kuwaangazia wagonjwa wenye matatizo ya uti wa mgongo, neva na ubongomiongoni mwa binadamu.
Lakini hatahivyo lengo la bwana Musk ni kudukua ubongo wa mwanadamu kupitia tarakilishi.
Kushirikisha ubongo wa mwanadamu na ule wa mashine
Kifaa ambacho kampuni imetengeneza kina kifaa kidogo kinachoweza kuchunguza- chenye electrodes zaidi ya 3,000 zilizounganishwa na nyuzi zinazoweza kubadilika - ambazo ni nyembamba kuliko nywele za binadamu - na ambazo pia zinaweza kufuatilia shughuli za neuroni 1,000.
Umuhimu wa mfumo huo, kulingana na kampuni hiyo ni kulenga maaneo fulani katika ubongo hatuaainayofanya upasuaji kuwa salama.
Pia kinaweza kutathmini yaliorekodiwa kupitia mashine ambayo itaamua ni aina gani ya matibabu yatakayopewa mgonjwa.
Neuralink hatahivyo haikutoa maelezo jinsi mfumo huo unavyoweza kubadilisha vitendo vya ubongo ama jinsi kifaa hicho kilivyoweza kuchochea seli za ubongo.
''Sio kwamba tayari tutakuwa tuna uwezo wa kushirikisha ubongo wa mwanadamu katika tarakilishi na kuchukua udhibiti wa bongo za wanadamu'', alisema bwana Musk.
Hiki ni kitu kitakachochukua muda mrefu. Lakini alisema kwamba wale watakaotaka kutumia mfumo huo utasaidiana na ule wa tarakilishi.
Awali Bwana Musk alikuwa amesema kuwa inteligensia ya mashine inaweza kuharibu jamii ya wanadamu.
Uunganishaji wa ubongo na tarakilishi utaimarisha zaidi ubongo wa mwanadamu , alisema akiongezea kwamba tayari watu wamekuwa wakifurahia hilo kupitia simu zao. Jinsi wanasayansi wanavyolenga kudukua ubongo wa mwanadamu
Baadaye baada ya muda wa maswali na majibu , alifichua kwamba kifaa hicho cha Neuralink kinafanya kazi na kwamba tayari kimefanyiwa vipimo katika tumbili huku mnyama huyo akiweza kudhibiti tarakilishi na ubongo wake , Kulingana na bwana Musk.
Sasa kampuni hiyo imewasilisha ombi la kutaka kuwajaribu wanadamu na mfmo huo ambalo litahitajika kuidhinishwa na kitengo cha usimamizi wa chakula na dawa nchini Marekani.
Bwana Musk pia analenga kuajri mwanasayansi mmoja zaidi katika kampuni hiyo ambayo kufikia sasa inaendeshwa na wafanyikazi 100.
Mpango wa kudukua ubongo wa mwanadamu- kampuni hiyo inasema utachukua miaka mingi ya kazi kufanywa ili kukabiliana na changomoto za kiteknolojia pamoja na kimaadili, lakini teknolojia hiyo huenda ikawa hatua kubwa katika kukabiliana na matatizo sugu ya kiafya kama vile ugonjwa wa kifafa na ule wa kutetemeka.
Miradi mingi ya bwana Musk inajaribu kufanya yale yanayowezekana.
Mradi wa Space X unalenga kuanzisha utalii wa kuelekea sayari ya Mars huku kampuni ya Boring ikijaribu kujenga mahandaki chini ya mji wa Los Angeles huku mradi wake wa Hyperloop ukilenga kuimarisha usafiri kwa njia nyengine.