Israel: Makaazi ya miaka 9000 yagunduliwa

Maelfu ya vitu, vito vya thamani, mbegu na vifaa vya kilimo vimepatikana katika eneo la jadi la makaazi yaliyodumu kwa miaka 9,000 nchini Israel.

Wana akiolojia wanaamini eneo hilo ambalo liko karibu na Motza, Magharibi mwa mji wa Jerusalem, wakati mmoja lilikua makaazi ya watu karibu 3,000.

Wachimbaji walipata mabaki ya jengo kubwa lenye vyumba kadhaa ambavyo watu walikua wakiishi wakati mmoja na kupata maeneo mengine ya matambiko yaliokua yakitumiwa na wakaazi hao.

Vitu vingine vilivyopatikana...

...ni pamoja ncha ya mkuki uliyotumika kwa shughuli za uwindaji na pengine kujilinda.

Vitu vingine vilipatikana ndani ya kaburi katika kile kinachoonekana kama vifaa vya kufanyia matambiko wakati wa kuzika.

Jiwe hili kinaashiria kichwa cha binadamu.

Bangili tofauti zilizotengenezwa kutokana na mawe pia zilipatikana. Zilikua ndogo kuashiria kuwa zilikuwa zikivaliwa na watoto, watafiti wanasema.

Vifaa vingine vilivyopatikana glasi vilivyotokana na matope ya moto wa volkeno, kutoka Anatolia.

Mamlaka ya Israel inayosimamia vitu vya kale inasema uvumbuzi huo utabadilisha mawazo ya wanahistoria wa kale katika eneo hilo ambalo liliaminiwa kuwa makaazi ya Yudea enzi hizo.

Picha zote kwa hisani ya Mamlaka ya Israel inayosimamia vitu vya kale.