Madai ya udhalilishaji kingono jeshini 'hayaripotiwi ipasavyo'

Wanajeshi wakitembea

Chanzo cha picha, Getty Images

Takriban madai 60 ya udhalilishaji wa kingono yaliyofanyiwa uchunguzi na polisi kwa miaka miwili hayakuripotiwa kwenye takwimu rasmi nchini Uingereza, BBC imebaini.

Takwimu za mwaka 2017 na mwaka 2018 hazikuhusisha makosa kama mawasiliano ya kingono na watoto.

Kundi la watetezi wa haki za binaadamu wanasema kuwa wizara ya ulinzi haiweki rekodi ya shutuma hizi ''ipasavyo au kwa usahihi''.

Wizara ya ulinzi imesema imejiridhisha kuwa data sahihi zilikuwa zimechapishwa.

Ripoti imedai kuwa idadi ya Vikosi vya Uingereza inajihusisha na vitendo vya ukandamizaji, unyanyapaa na ikiwemo udhalilishaji wa kingono.

Wizara hiyo imesema imepokea mapendekezo yote 36 ya ripoti kwa ajili ya kuondokana na changamoto hizo.

BBC pia iliongea na afisa wa polisi wa zamani anayeamini kuwa mfumo wa haki ndani ya wizara unakosa uzoefu wa kufanya uchunguzi kuhusu udhalilishaji wa kingono.

Mwanamke akiwa amekumbatia miguu yake

Chanzo cha picha, Getty Images

Elizabeth (jina la kubuni) alijiunga na jeshi.Ameiambia BBC kuwa amekuwa akidhalilishwa bna mwanajeshi.

''Mtu mmoja alikuja nyuma yangu akanikamata sehemu zangu za siri. ilishtua sana.''

Jeshi ilianza kufanya uchunguzi kisha aliyetelekeza vitendo huvyo alitiwa nguvuni na kushtakiwa, lakini baada ya kesi aliachiwa huru

Katika kuhitimisha hukumu ya mahakama, jaji alisema uchunguzi wa polisi haukufanyika vizuri- na kuwa makosa kama kutowahoji mashahidi muhimu na ukusanyaji wa ushahidi, kulichangia kuachiwa kwa muhalifu.

Elizabeth anasema: ''kuna kipindi nilikuwa najiuliza ni namna gani nitaendelea kulitumikia jeshi?, kwa sababu niliona nitalitumikiaje jeshi ikiwa sipati uungwaji mkono wakati huu ambao mambo ni magumu.''