Mjerumani Ursula von der Leyen ateuliwa kuongoza Tume ya Ulaya

Picha ya maktaba ya Ursula von der Leyen

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Ursula von der Leyen aliungwa mkono na Angela Merkel lakini uteuzi wake ulipingwa katika na muungano tawala nchini Ujerumani
Muda wa kusoma: Dakika 3

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamemteua waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Ursula von der Leyen kuwa rais wa Tume ya Ulaya.

Uteuzi wa Bi Von der Leyen, ambaye ni mshirika wa karibu wa Kansela Angela Merkel, haukutarajiwa baada ya wagombea wakuu kukataliwa.

Uteuzi wake ukiidhinishwa na Bunge la Ulaya atakuwa mwanamke wa kwanza kuwa rais wa Tume ya Ulaya.

Mkuu wa Shirika la fedha Duniani IMF Christine Lagarde ameteuliwa kuongoza Benki Kuu ya Ulaya (ECB).

Uamuzi uo umefikiwa baada ya siku kadhaa ya mashauriano magumu.

Katika yote viongozi wa EU walipewa jukumu la kuwateua watu watano kuchukua nyadhifa za juu katika Muungano huo.

Wazri Mkuu wa Ubelgiji mwenye siasa za kadri Charles Michel ameteuliwa kuchukua nafasi ya rais wa Baraza la Ulaya iliyokuwa inashikiliwa na Donald Tusk huku Josep Borrell wa Uhispania akipendekezwa kuwa mkuu wa sera za kigeni.

Wadhifa w benki kuu ya Ulaya kwa sasa unashikiliwa na Mario Draghi, ambaye alisifika kwa kuokoa sarafu ya wakati wa mzozo wa madeni uliyokumba mataifa yanayotumia sarafu hiyo

Maelezo ya video, Donald Tusk akitangaza majina ya viongozi walioteuliwa katika nyadhifa za juu za kazi katika Tume ya Ulaya

Teuzi zote lazima ziidhinishwe na Bunge la Ulaya

'Uteuzi ulizingatia usawa wa Kijinsia'

"Tumekubaliana kuhusu uteuzi huu kabla ya kikao cha kwanza cha bunge la Ulaya,"alisema Bw. Tusk.

Alisifu "usawa wa kijinsia"uliozingaztiwa katika uteuzi huo ba kuongeza kuwa Ujerumani ilipinga uteuzi wa Bi von der Leyen kutokana na masuala ya muungano wa vyama.

Hata hivyo aligusia kuwa Bi Merkel aliunga mkono uteuzi wake.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Presentational white space

Kiongozi huyo wa Ujerumani aliwaarifu wanahabari kuwa uteuzi wake ulipingwa kwa mujibu wa mkataba uliofikiwa na muungano tawala mjini Berlin.

Ikiwa Bi von der Leyenataidhinishwa kushikilia wadhifa huo itakuwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 60, Mjerumani kupewa wadhifa huo.

Grey line

Walioteuliwa

Ursula von der Leyen - Rais wa Tume ya Ulaya

Ursula von der Leyen

Chanzo cha picha, EPA

Bi von der Leyen alizaliwa mjini Brussels, lakini familia yake ilihamia Ujerumani akiwa na miaka 13.

Alisomea masuala ya uchumi katika chuo cha LSE mjiniLondon na matibabu mjini Hanover kabala ya kujiunga na siasa.

Amekuwa mwanachama wa chama cha Bi Merkel cha conservative Christian Democrats (CDU)tangu mwaka 2005.

Christine Lagarde - Mkuu wa Benki Kuu ya Ulaya

Christine Lagarde

Chanzo cha picha, AFP

Bi Lagarde, 63, ambaye ni Mfaransa, alikuwa mwanamke wa kwanza kuongoza Shirika la Kimataifa la fedha duniani (IMF) walipoteuliwa katika wadhifa huo mwaka 2011.

Alisomea Marekani kabla ya kuhitimu katika chuo cha sheria mjini Paris na kupata shada ya uzamifu yasiasa katika Taasisi ya Aix en Provence

Aliteuliwa waziriwa biasha wa Ufaransa mwaka 2005 na baadae waziri wa fedha mwaka 2007.

Charles Michel - Rais wa Baraza la Ulaya

Charles Michel

Chanzo cha picha, Reuters

Bw. Michel, 43, ni wakili na Meya wa zamani wa mji wa Jodoigne nchini Ubelgiji. Amekuwa Kamishena wa Umoja wa Ulaya na mwanachama wa bunge la Ulaya

Mwezi Oktoba mwaka 2014 alichaguliwa Waziri Mkuu wa Ubelgiji akiwa na miaka 38 na kuwa mtu mwenye umri mdogo kushikilia wadhifa huo nchini Ubelgiji tangu mwaka 1841.

Josep Borrell - Mkuu wa EU wa sera za kigeni

Josep Borrell

Chanzo cha picha, EPA

Waziri huyu wa mambo ya nje wa Uhispani aliye na umri wa miaka 72 anajiandaa kurejea katika wadhifa wa ngazi ya juu ya siasa za Umoja wa Ulaya baada ya kuhudumu kama raisi wa Bunge la Umoja huo mwaka 2004 hadi 2007.

Alianza kazi kama mwanachama wa chama cha kisosholisti cha Uhispania mwaka 1975 na ana sifa ya kuzungumza wazi wazi mabo yalivyo.

Uteuzi wake ukiidhinishwa atachukua wadhifa mkuu wa sera za kigeni kutoka kwa Federica Mogherini amabye ni raia wa Italia.

Grey line

Uteuzi wa tano ambao ni wa- rais wa Bunge la Ulaya utafanywa siku ya Jumatano .

Waziri mkuu wa Ireland Leo Varadkar amesema uteuzi wa wanawake wawili katika nyadhifa za ngazi ya juu umetuma ujumbe mzito kuwa Umoja wa Ulaya unaongoza katika masuala ya kuzingatia usawa wa kijisia.