Raphael Ongangi: Mfanyabiashara wa Kenya aliyetekwa nyara Tanzania apatikana Mombasa

Chanzo cha picha, Ongangi/facebook
Mfanyabiashara wa Kenya Raphael Ongangi aliyetekwa nyara nchini Tanzania kutokana na madai ya kisiasa amepatikana mjini Mombasa.
Raphael Ongangi alitekwa Jumatatu usiku katika viunga vya mitaa ya Oysterbay jijini Dar es Salaam na watu wenye silaha akiwa na mke wake Veronica Kundya.
Mkewe Veronica amethibitisha kupatikana kwa mumewe mapema leo siku ya Jumanne.
''Nimezungumza naye mwenyewe yupo Momabasa , tumezungumza kwa ufupi anashukuru sana'', ameliambia gazeti la Mwananchi.
Mwanaharakati wa haki za kibinaadamu nchini Kenya Boniface Mwangi ametuma ujumbe wa Twitter akisema kuwa Mfanyabiashara huyo ambaye ka sasa anadaiwa kulazwa katika hospitali ya Aga Khan mjini Mombasa alitupwa mjini humo na maafisa wa ujasusi.
Mwamngi amewashukuru wote waliohusika katika kampeni iliosababisha kuachiliwa kwake.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Kwa mujibu, wa taarifa zilizoripotiwa na vyombo vya habari nchini Kenya na Tanzania, watu wasiojulikana waliwafuatilia wanandoa hao na kisha kulizuia gari yao na kumchukua bwana huyo na kuondoka naye.
Awali bi Veronica anasema aliamriwa na watu hao ambao anadai walijatambulisha kama maafisa wa usalama kuwa asiseme chochote mpaka atakapotaarifiwa nao.
Na baada ya takribani saa moja akapokea simu kutoka kwa mumewe iliyomtaka kurejea nyumbani na wala asiripoti tukio hilo mahali popote.
Taarifa zilichapishwa kwenye mitandao ya kijamii zinaripoti kuwa Ongangi aliingia Tanzania mwanzoni mwa miaka ya 2000 kwa masomo ya elimu ya juu katika moja ya vyuo vikuu nchini humo.
Udukuzi wa mitandao ya Zitto kabwe
#Baada ya masomo alibaki nchini humo na kuanza biashara na inaripotiwa kuwa ana miliki na kuendesha biashara ya kusafirisha mizigo kutoka bandari ya Dar es Salaam kwenda Rwanda, Zambia na Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Tukio la Ongangi kutekwa lilichukua sura mpya baada ya Kiongozi wa chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe kuhusianisha kushikiliwa kwake mateka na kudukuliwa kwa mitandao yake ya kijamii.
Ongangi na Zitto wana usuhuba, na mfanyabiashara huyo ameshawahi kuwa msaidizi wa Kabwe.
Zitto aliwaambia waandishi jijini Dodoma wiki iliyopita kuwa waliomteka Ongangi walidukua mitandao yake ya kijamii.
Mkewe anasemaje?
Uongozi wa ACT-Wazalendo baadaye ulitoa taarifa kuwa mfanyabiashara huyo alihusika kwa kiasi kikubwa katika kufunguliwa kwa mitandao hiyo, na ndiye mtu pekee ambaye alikuwa na nywila (pasword) mbali na Zitto mwenyewe.
Baada ya kutekwa Ongangi na kabla ya Zitto kutoa taarifa hiyo, mitandao hiyo ya kijamii ya Zitto ilichapisha maudhui ambayo yalistaajabisha wengi.
Zitto anafahamika kwa kuwa na msimamo mkali wa kuikosoa serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais John Magufuli, lakini maudhui yanayotiliwa shaka yalionesha kulegeza kamba kwa mwanasiasa huyo.
"Ni kweli tumekuwa tukiikosoa Serikali kwa muda mrefu lakini lazima nikiri kuwa kuna mabadiliko makubwa yamefanywa na serikali hii ya JPM. Japokuwa ninajua kuna baadhi ya viongozi aliowateua wanamuangusha kiuhalisia MAGUFULI amefanya mengi," ndivyo ujumbe wa kwanza kupitia akaunti ya Zitto ya Twitter uliandika Alhamisi ya wiki iliyopita.
Kisha ukafuata huu: "Nilisema tangu mwanzo sitashiriki siasa za kupinga maendeleo yanayofanywa na serikali hii ya @MagufuliJP na sasa nimeamua kwa moyo wa dhati kabisa ninaamua kuunga mkono kwani ni kwa maendeleo ya wote. Kiongozi mbinafsi kwa vyovyote hawezi kuona haya yanayofanyika kwa sasa."
Ujumbe wa mwisho uliotumwa saa 7.26 mchana wa siku hiyo uliwalenga wabunge wa chama tawala CCM ambao wanaonekana kuwa ni wakosoaji wa ndani wa serikali yao: "Nawakaribisha pia @HusseinBashe na @Nnauye_Nape ambao wameshachukua kadi za uanachama ACT Wazalendo na wanaosubiri ni kuvunjwa tu kwa #Bunge na bila kumsahau mdogo wangu @JMakamba. Hakika ACT Wazalendo itaitikisa Chadema ambayo inatamba kuwa Chama Kikuu cha Upinzani."
Mwanasiasa huyo amesema mara ya mwisho kutumia akaunti zake ilikuwa Juni 11, 2019 baada ya kukamatwa na kuwekwa kizuizini na Idara la Uhamiaji Zanzibar ambao walimzuia kusafiri kwenda Kenya.
Mara baada ya kumwachia, Zitto hakupewa simu yake ya mkononi na kompyuta mpakato 'laptop.'
Mtandao huo wa Twitter wa Zitto tayari umeshafungwa baada ya kutokea tukio hilo.
Hat hivyo ujumbe huo uliwaibua Bashe na Nape ambao walionekana kuwarushia lawama wahusika ambao hawakuwataja majina.
Tunaendelea kukujuza zaidi....















