Magari ya umeme: Magari mapya yanapaswa kuwa na kelele kwa ajili ya usalama

Alama ya waya wa umeme kwenye gari linalotumia umeme

Chanzo cha picha, Reuters

Muda wa kusoma: Dakika 1

Magari mapya yanayotumia umeme yanapaswa kuwekwa chombo kitakachotoa kelele, hii ni chini ya sheria mpya ya EU ambayo inaanza kutekelezwa Jumatatu.

Hatua hii mpya imekuja kutokana na madai kuwa magari ya umeme hayana sauti na kuwafanya watu ambao hawatumii magari wakiwa barabarani kuwa hataranini kwa kuwa magari hayo hayasikiki mlio wake yakiwa karibu.

Aina zote mpya za magari aina ya Four-wheel yanapaswa kufungwa chombo hicho ambacho kitakuwa kikitoa mlio kama wa injini.

Kifaa hicho kiitwacho acoustic vehicle alert system (Avas) lazima kitoe mlio wakati gari inarudi nyuma au kusafiri kwa umbali wa kilometa 19 kwa saa

Umoja wa Ulaya unasema magari yanapaswa kuwa na kelele yakiwa karibu na watembea kwa miguu yanapokuwa yakitembea taratibu, ingawa madereva watakuwa na uwezo wa kukizima kifaa hicho kama wanafikiri kuna ulazima.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Taasisi zinazosimamia mbwa wanaotoa usaidizi kwa watu wenye uhitaji barabarani kama vile wale wasioona na walemavu wa viungo wamesema kuwa ni vigumu kubaini kama magari yasiyo na sauti yako karibu, na wameunga mkono mabadiliko haya, lakini wanasema kuwa vyombo vya moto vinavyotumia umeme vinapaswa kutoa sauti vikiwa kwenye mwendo wowote.

Waziri wa barabara Michael Ellis amesema serikali ilitaka ''faida ya usafiri wa kutunza mazingira kumfikia kila mmoja'' na ameeleza kuelewa maoni ya wale wenye ulemavu wa kutoona.

''Matakwa mapya yatawafanya watu wanaotembea kwa miguu kuwa na hali ya kujiamini wakiwa wanavuka barabara,'' aliongeza.

Ifikikapo mwaka 2021 magari yote ya umeme yanapaswa kuwa na kifaa cha AVAS, si kwa magari mapya pekee.

Serikali ilitangaza mipango ya kupiga marufuku magari yanayotumia mafuta ya petroli na Dizeli kuuzwa mwaka 2040.