Ni kwanini Morocco inaweza kushuhudia mapinduzi?

Chanzo cha picha, Getty Images
Utafiti mkubwa wa BBC unaonyesha kuwa takriban nusu ya Wamorocco wanaangalia uwezekano wa kuhamia kwingine na wanataka mabadiliko ya mara moja ya kisiasa. Kutokana na hilo Je Morocco inaweza kufuata hatua za Sudan na Algeria na kuwapindua viongozi wao? , anauliza Tom de Castella
Kwneye veranda alikoketi akitazama mji wa Casablanca kw achini , mwanamme anavuta sigara na kufikiria juu ya ndoto ambayo ilinyakuliwa kutoka kwake.
Saleh al-Mansouri ana umri wa miaka ishirini pekeelakini anafahamu ni nini maana ya kuvuka bahari kuelekea Ulaya . Aliishi nchini Ujerumani kw amiaka kadhaa hadi maombi yake ya uhamiaji yalipo kataliwana akalazimika kurejea nyumbani Morocco.
"Watu huenda kule kutafuta vitu kadhaa ambavyo hawana hapa ," Anasema Bwana Mansouri . Baadhi ni kwa sababu za kiuchumi - anazungumzia juu ya nguo ambazo huwezi kuzinunua , mtindo wa maisha bora - lakini mambo mengine hayana mashiko. "Kama uhuru," anasema, kabla ya kuongeza kusema kuwa : "Kuna mambo mengi... kama heshima.
"Hakuna huduma hapa Morocco kwa ajili ya umma. Ni ukosefu wa huduma ambao unawafanuya watu kuhama."

Takriban nusu ya Wamorocco wanafikiria kuhama. Uwiano ni wa juu baada ya kupungua kwa kipindi cha muongo , unaeleza utafiti uliofanywa na BBC Idhaa ya kiarabu umeonyesha+++
Ukitazama kwa kina zaidi utafiti ambapo unajumuisha maeneo ya Mashariki ya kati na Afrika magharibi wa mwaka 2018 na 2019 ambao ulifanywa na mtandao wa utafiti wa Arab Barometer, unaibua swali : Je Morocco inajiandaa kwa maandamano makubwa?.
Maandamano makubwa ya kuipinga serikali katika mataifa ya Sudan na Algeria yalisababisha mabadiliko ya ghafla ya kisiasa mnamo mwezi wa April yaliyoitwa Arab Spring 2.0.
Wakati kumpindua Omar al-Bashir nchin Sudan na Abdelaziz Bouteflika nchini Algeria kuliwashitua watu wengi, mambo yalikuwa wazi katika utafiti uliofanyw ana BBC idhaa ya kiarabu.
Miezi kadhaa kabla ya maandamano kuziangusha waliofanyiwa utafiti kuhusu serikali za Algeria na Sudan walitoa maswali yaliyoonyesha kuwa walikuwa na hasira, waogana wanaotaka suluhu.

Theluthi tu ya Wasudan walisema kuwa nvchi yao inakaribia kuwa ya kidikteta kuliko kidemokrasia , katika kanda hiyo. Nchini Algeria ilikuwa ni 56%, ya tatu nyuma ya Libya.
Takriban theluthi mbili ya Waalgeria walisema kuwa uchaguzi wa mwisho wa nchi hiyo haukuwa wa huru na haki, zaidi ya maeneo yote yaliyofanyiwa utafiti . Ni robo tu ya Wasudan na theluthi ya Waalgeria walioamini kuwa uhuru wa kuongea upo katika nchi yao.
Nchi nyingine iliyojitokeza katika data - Morocco.
Kukatatamaa na mkanganyiko
Maeneo mengi yaliyofanyiwa utafiti yalionyesha utadhi wa mageuzi . Lakini nchini Morocco nusu ya waliofanyiwa utafiti walisema wanataka mabadiliko ya kisiasa ya mara moja.
" Kuna hali halisi ya kukata tamaa na mkanganyiko miongoni mwa vijana," anasema mwandishi wa habari na mwanaharakati wa upinzani Abdellatif Fadouach.

Takriban 45% ya watu walio chini ya umri wa miaka 24 katika masuala mengi nchi imegawanyika. Kiasi cha 70% ya watu wazima walio na umri wa chini ya miaka 30 wanataka kuhama nchi ikilinganishwa na 22% ya watu walio na umri wa miaka arobaini . Huku nusu ya watu wenye umri wa miaka zaidi ya 60- wakiwa na mtizamo chanya kuhusu serikali yao , idadi ya wale walio na umri kati ya miaka 18-29 ni 18%.
Arab Spring iliwapatia vijana matumaini kuwa jamii inaweza kubadilika.
Morocconi taifa la kifalme na baada ya maandamano kulipuka mwaka 2011, Mfalme Mohammed VI alitangaza mpango wa mageuzi. Katiba mpya ilitolewa iliyopanua zaidi mamlaka ya bunge na waziri Mkuu na kumuachia mfalme mamlaka kadhaa. Nyingi kati ya ahadi za mageuzi hazikuwahi kutekelezwa kikamilifiu, anasema, Bwana Fadouach.
uangalizi wa wanasiasa wasomi
Usimamizi katika soko la ajira unazuwia soko halisi la uchumi, anasema, akiongeza kuwa fursa za kazi -kama vile kupata vibali vya kodiau vya uvuvi- ni zawadi kwa wanasiasa walioko mamlakani na katika kasri ya Ufalme.
"hata matumaini kidogo kwa ajili ya hali ya kesho bahati mbaya hufupishwa na hali ya mambo kurudi nyuma kama yalivyokuwa awali," anasema. Hamu ipo ya kuleta mabadiliko miongoni mwa wanasiasa wasomi, anaamini . " Wakati wowote Morocco inaweza kushuhudia kile kilichotokea katika Algeria na Sudan na Syria na Misri kabla , Libya au Tunisia."

Chanzo cha picha, PAUL HARRIS
Ukizungumza na wazee utasikia hamu ya kuendelea kwa mambo yalivyo.
Abdallah al-Barnouni ni mhasibu mstaafu anayeishi Casablanca. Hana mawazo kama ya vijana wanaotaka mabadiliko ya haraka : "Kizazi cha leo, watoto wa leo, wanataka kufika haraka. Wanataka kila kitu haraka - magari, nyumba, kazi, wanataka kufikia kiwango cha juu cha maisha haraka."
Hakuna ishara ya ghasia za mageuzi. . Walau kwa sasa bado.
Marais waliopinduliwa tangu kuanza kwa Arab uprisings
- rais wa Tunisia Zine al-Abidine Ben Ali l aliondoka mamlakani 14 Januari 2011
- rais wa Misri Hosni Mubarak aling'olewa madarakani 11 Februari 2011
- Rais wa libya Muammar Gaddafi aliuawa 20 Octoba 2011
- rais wa Yemen Ali Abdullah Saleh alipinduliwa 27 Februari 2012
- Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika alijiuzulu tarehe 3 Aprili 2019
- Rais wa Sudan Omar al-Bashir alipinduliwa tarehe 11 Aprili 2019

katika Sudan na Algeria umma ulianza kuonyesha kutoridhika kuanzia majimbo maskini kabla ya kusambaa katika mji mkuu . Hilo linaweza kutokea tena?
"Ni vibaya kubashiri," anasema Abderrahim Smougueni, mwandishi wa habari wa gazeti la Morocco la kila wiki TelQuel Arabi. Baadhi ya ishara zipo katika Morocco. " Kuna kuongezeka kwa hali ya watu kutoridhika na mkanganyiko dhidi ya serikali na waziri mkuu." Watu walikuwa wanaitarajia serikali ipigane vita dhidi ya ufisadi, anasema. Badala yake I wanaweka kodi kwa watu wa kipato cha kati , na kutengo watu muhimu.

hata hivyo kuna tofauti muhimu. Sudan na Algeria sio mataifa yenye ufalme.
Jeshi la ufalme
Nchini Morocco hata hivyo mawazo yaliyoafikiwa ni kwamba mfalme alikuwa juu ya siasa na alikuw ani mtu wa kuzuwia maandamano makubwa. Swali ni ikiwa hali hiyo bado ipo. "kwa chochote kile ambacho watu wanakifikiria kuihusu serikali, wana imani na mfalme ," Bwana Smougueni anasema. Wengine wanasema ni muda mfupi umesalia "Kabla ya Arab Spring pale kuafikiwa ndani ya katika Ufalme," Anasema Bwana Fadouach . "Lakini leo huenda imani na ufalme isiwepo"

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa Bwana Smougueni bado hili halijawa vuguvugu kubwa , kutakuwa na msururu zaidi wa maandamano ya kiufundi na migomo kuhusu mageuzi katika sekta muhimu za kiuchumi kama afya na elimu.
Na bado, mikoa ambayo kwa majimbo ambayo yalionekana haiwezi kuwataka mabadiliko kwa sasa inatawaliwa na kutokuwa na uthabiti . tangu harakati za kutaka mageuzi kau kuibuka kwa vita.
Kwa maneno mengine, maandamano ya umma yanaweza kusambaa kama moto wa nyikani katika ulimwengu wa kiarabu. Na hakuna hakikisho kuwa mambo yatamalizika vizuri.
Morocco bado haijawa na kipindi cha Arab Spring - vuguvugu la maandamano la tarehe 20 Februari 2011 halikusababisha mabadiliko muhimu. Mfalme bado anashika hatamu na mageuzi ya kisiasa bado yana kikomo.
Michael Robbins kutoka taasisi ya Arab Barometer anahoji juu ya kuangushwa kwa utawala wa kifalme. Lakini data zinapaswa kutoa onyo kwa serikali ya Morocco ,anasema. "Wamorocco, hususan kizazi cha vijana wana uwezekano mkubwa wa kutaka mageuzi ya haraka kuliko raia katika nchi nyingine. Pia wanaonekana kuwa karibu kupata sababu ya kuwachochea ."
Morocco iko njia panda . mengi yanategeme ni nini vijana ambao ni wengi wananakidai kutoka kwa mfalme wao na serikali yake ambayo haina umaarufu.













