Watu 30 wahukumiwa kifo Misri kwa mauaji ya mwendesha mashtaka

A picture taken on July 10, 2013 shows Egyptian state prosecutor Hisham Barakat sitting at his office in Cairo.

Chanzo cha picha, STR/AFP/Getty Images

Maelezo ya picha, Hisham Barakat aliuawawa kwenye mlipuko

Mahakama ya Misri imependekeza adhabu ya kifo kwa watu thelathini waliotiwa hatiani kwa kuhusika kwenye mauaji ya mwendesha mashtaka mkuu wa nchi hiyo.

Hisham Barakat alikufa kwenye shambulio la bomu lililotegwa kwenye gari miaka miwili iliyopita.

Alikuwa miongoni mwa maafisa waandamizi wakuu kuuawa na wanamgambo katika miaka ya karibuni.

Bwana Barakati alihusishwa na maelfu ya kesi ya wapiganaji wa Kiislamu kufuatia mapinduzi ya serikali ya Misri iliyokuwa ikiongozwa na Muslim Brotherhood.

Mamlaka za dini za nchi hiyo sasa wataamua iwapo waidhinishe hukumu ya vifo iliyopitishwa na mahakama.

Egyptian security forces stand guard at the site of a bomb attack that targeted the convoy of Egyptian state prosecutor, Hisham Barakat, who died hours after the powerful explosion hit his convoy, in the capital Cairo on June 29, 2015.

Chanzo cha picha, KHALED DESOUKI/AFP/Getty Images

Maelezo ya picha, Eneo la mlipuko mwaka 2015

Misri iliwalaumu kundi la Musclim Brotherhood na lile la Gaza la Hamas kwa mauaji ya Bwana Barakat licha ya makundi yote mawili kukana kuhusika

Mwaka uliopita wizara ya mambo ya ndani ilitoa video ikionyesha wanaume kadha wakikiri kuhusika kwenye mauaji hayo na kusema kuwa walienda huko Gaza kupata mafunzo kutoka kundi la Hamas.

Baadaye baadhi yao walikana madai hayo mahakamani wakisema kuwa walikuwa wameteswa ili kukiri.