Charles Jaguar Kanyi: Mbunge wa Kenya aliyetoa kauli zenye utata

Chanzo cha picha, Jaguar/Facebook
Charles Njagua Kanyi al maarufu Jaguar ni mwanamuziki, mwanasiasa na mjasiliamali na inaaminiwa kuwa mmoja wa wasanii tajiri nchini Kenya na katika eneo la Afrika Mashariki
Alizaliwa katika familia ya maskini katika familia ya watoto watatu. Jaguar alisomea katika shule ya msingi mjini Nairobi na akiwa na umri wa miaka 11 alifiwa na mama yake ambaye wakati huo alikuwa ndiye mlezi wake pekee.
Alilazimika kufanya kazi za vibarua ili kujikimu kimaisha na moja ya kazi alizozifanya ilikuwa ni kazi ya ukondakta wa mabasi ya abiria, maarufu daladala au matatu, na kwa msaada wa marafiki aliweza kumaliza shule.
Maisha ya kimuziki:
Rekodi Jaguar ya kwanza ilifanyika namo mwaka 2004 na baadae akajiunga na kampuni ya muziki ya Afrika mashariki Ogopa Deejays mnamo mwaka 2005 ambapo na miziki mmoja baada ya mwingine miongoni mwake "kigeugeu." Uliovuma sana na kupokea tuzo nyingi.

Chanzo cha picha, Jaguar/Facebook
Mnamo mwaka 2013 Jaguar alianza kurekodi katika Studio kuu Switch Studios iliyoanzishwa na mmoja wa wazalishaji wa muziki wake wa muda mrefu, Philip Makanda zamani akiwa katika Ogopa Deejays.
Miongoni mwa nyimbo nyingine zilizompatia umaarufu ni Kioo na One centimeter, na kufanya ushirikiano wa kimziki( Kolabo) na wasanii maarufu wa muziki badarani Afrika kama Iyanya kutoka Nigeria, na Mafikizolo kutoka Afrika Kusini katika singo "Going Nowhere"
Tuzo za muziki:
- Mwaka 2011-Tuzo ya muziki wa Afrika mashariki- Mwanamuziki bora wa kiume Afrika mashariki
- Mwaka 2011- Tuzo yaNzumari- Mwanamuziki bora wa kiume Kenya
- Mwaka 2012 -Tuzo ya Kisima-Wimbo bora Kenya
- Mwaka 2012 - Tuzo ya Pearl (Uganda)-Mwanamuziki bora wa kiume
- Mwaka 2012- Tuzo ya muzikila kilimanjaro (Tanzania)-Wimbo bora Afrika Mashariki- Kigeugeu
- Mwaka 2012- Tuzo ya Nzumari-Mwanamuziki bora Afrika Mashariki
- Mwaka 2012-Mshindi wa tuzo ya Channel O- Wimbo bora wa Afrika Mashariki
- Mwaka 2013-Tuzo ya MCSK linalotolewa kwa msanii ambaye nyimbo zake zilichezwa zaidi katika vituo vya redio na kupendwa nchini Kenya.
- Mwaka 2014-Tuzo ya muziki ya Kilimanjaroya Afrika mashariki-Wimbo bora- Kipepeo
- Mwaka 2014- Tuzo ya AFRIMMA (Dallas Texas)-Aliteuliwa kama mwanamuziki bora wa kiume Afrika
Mafanikio ya kibiashara:

Chanzo cha picha, Jaguar/Facebook
Kwa miaka kadhaa Jaguar ameimarisha himaya yake binafsi ya ujasiliamali ambayo kwasasa inampatia kipato kikubwa cha kibiashara.
Kando na biashara yake ya muziki, Jaguar anamiliki magari ya kifahari na anafahamika kuwa na uwekezaji katika majumba ya makazi pamoja, usafiri na safari za anga.
Ajira:
Jaguar aliteuliwa na rais Uhuru Kenyatta kuwa Mkurugenzi wa wa Mamlaka ya taifa ya kupambana na ulevina madawa ya kulevya(NACADA) nchini Kenya

Chanzo cha picha, Jaguar/Facebook

Chanzo cha picha, Jaguar/Facebook
Tarehe 9 Agosti 2017 Jaguar alichaguliwa kuwa Mbunge wa jimbo la Starehe mjini Nairobi kupitia tiketi ya chama tawala cha Jubilee baada ya kuwashinda washindani wenzake Steve Mbogo, Boniface Mwangi na Mwaniki Kwenya.
Jaguar ni kipenzi cha wengi nchini Kenya na ni mwanasiasa ambaye amekuwa na mvuto hasa kwa wafuasi wake ambao wengi wao ni vijana na wanawake.
Mvuto wake umekuwa ukishuhudiwa kila mara anapojitokeza kukutana na wafuasi na wananchi kwa mikutana katika jimbo lake la Starehe ambapo umati mkubwa hujitokeza kumsikiliza na kumshangilia.













