Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Imani ndogo kwa chanjo ni janga duniani - Afrika mashariki mfano wa kupigiwa upatu
Imani ndogo kutoka kwa umma dhidi ya chanjo duniani inaathiri na kurudisha nyuma vita dhidi ya magonjwa hatari yanayoweza kuzuilika, wataalamu wanaonya.
Utafiti mkubwa duniani uliochunguza mtazamo wa watu kuhusu chanjo unaonyesha ni watu wachache walio na imani na chanjo duniani.
Uchambuzi wa wakfu wa Wellcome Trust unajumuisha majibu ya zaidi ya watu 140,000 katika mataifa 140.
Haya yanajiri wakati shirika la afya duniani WHO likiwa limeorodhesha ususiaji chanjo kama mojawapo ya tishio kumi kuu dhidi ya afya duniani.
Wellcome Global Monitor lilitekeleza utafiti uliokuwa na uwakilishi wa kitaifa katika nchi 142. Mada za utafiti zilijumuisha: imani kwa sayansi, taarifa ya afya; kiwango cha uelewa na shauku kwa sayansi na afya na mitazamao ya watu kwa chanjo.
Utafiti huo wa kimataifa unafichua kwamba idadi kubwa ya watu wanasema wanaamini kwa kiasi kidogo chanjo.
Walipoulizwa iwapo chanjo ni salama:
- 79% (wanane kati ya kumi) "kama ambaye" au "wanakubali pakubwa "
- 7%"kama ambaye" au "hawaamini kabisa"
- 14% hawakubali wala hawakatai au "hawajui"
Walipoulizwa iwapo wanaamini chanjo zinafanya kazi:
- 84% wanakubali pakubwa au kama ambaye
- 5% wanakataa au kama ambaye wanakataa pakubwa
- 12% hawakubali wala hawakatai au "hawajui"
Kwanini ina umuhimu?
Kuna ushahidi mwingi tu wa kisayansi kuwa chanjo nikinga bora dhidi ya maambukizi hatari kama surua au ukambi.
Chanjo huwalinda mabilioni ya watu duniani. Imefanikiwa kuangamiza kabisa ugonjwa wa - smallpox - na zinakaribia kuangamiza magonjwa mengine kama polio.
Lakini baadhi ya magonjwa kama surua, yanazuka upya na wataalamu wanasema watu wanaosusia chanjo, hatua inayotokana na hofu na kuenea kwa habari za uongozo kuhusu chanjo hizo ni mojawapo wa sababu.
Dkt Ann Lindstrand, mtaalamu wa chanjo katika shirika la afya duniani amesema hali iliopo sasa ni nzito sana. "Kususia chanjo kuna uwezo kwa baadhi ya maeneo kutatiza pakubwa hatua zilizopigwa duniani katika kudhibiti magonjwa yanayoweza kuzuilika kwa chanjo.
"Visa vyovyote tunavyoviona vya kuzuka upya kwa magonjwa ni hatua isiyokubalika ya kurudi nyuma."
Surua/Ukambi umerudi
Mataifa yaliokaribia kuangamiza ukambi yameshuhudia milipuko mingi ya ugonjw ahuo.
Data zinaonyesha ongezeko la visa katika takriban kila sehemu duniani, huku kukiwa na 30% ya visa zaidi vilivyoshuhudia mnamo 2017 ikilinganishwa na 2016.
Uamuzi unaotokana na sababu yoyote ile ya kususia chanjo ni hatari sio tu kwa wengine, lakini kwa mtu binfasi kurudiwa na maambukizi.
Iwapo watu wa kutosha watapata chanjo, inasitisha ugonjwa kutosambaa katika umati wa watu - jambo ambalo wataalamu wanaliita "herd immunity"au kinga ya wengi.
Mifano ya ufanisi
Watu wengi wanaoishi katika maeneo masikini wapo salama. Kiwango kikubwa kipo Asia kusini ambako 95% ya watu wanakubali, ikifuatiwana Afrika mashariki ambako 92% ya watu wanaziamini chanjo.
Bangladesh na Rwanda zina makubaliano yanayokaribiana kuwiana kuhusu usalama na ufanyaji kazi wa chanjo na zimefanikiwa kupata kiwango kikubwa cha watu waliopewa chanjo licha ya changamoto nyingi katika kuzifikisha chanjo kwa watu.
Rwanda ilikuwa nchi ya kwanza ya kipato cha chini duniani kuhakikisha wanawake kote wanapata chanjo ya HPV inayotoa kinga dhidi ya saratani ya shingo ya uzazi.
Kwanini kuna imani ndogo?
Baadhiya watu wanaoishi katika maeneo mengine yalio ya kipato cha juu ni miongoni mwa wanaoamini kwa uchache kuhusu usalama wa chanjo
Nchini France - nchi mojawapo miongoni mwa nyingine za Ulaya ambazo sasa zinashuhudia mlipuko wa surua - mtu mmoja kati ya watatu haamini kuwa chanjo zi salama. Hicho ni kiwango kikubwa kwa asilimia kwa taifa lolote duniani.
Raia wa Ufaransa pia ni miongoni mwa walio n auwezekano mkubwa kukataa kwamba chanjo zinafanya kazi, 19%, na wanakataa kuwa chanjo ni muhimu kwa watoto 10%.
Serikali ya Ufaransa sasa imeongeza chanjo nane za ziada za lazima kwa tatu zilizopo ambazo watoto nchini humo hupewa.
Nchi jirani Italia - 76% wanakubali kuwa chanjo ni salama - hivi maajuzi ilipitisha sheria inayoruhusu shule kuwapiga marufuku watoto ambao hawajachanjwa, au inawatoza faini wazazi baada ya takwimu za wanaopokea chanjo kushuka pakubwa.
Uingereza bado ingali kufika kiwango hicho lakini waziri wa afya Matt Hancock amesema sio ajabu kukaidhinishwa chanjo za lazima ikibidi.
Kumeshuhudiwa pia milipuko ya surua nchini Marekani - mlipuko mkubwa kuwahi kutokea nchini humo katika muongo mmoja huku kukishuhudiwa visa 980 katika majimbo 26 katika mwaka 2019 kufikia sasa.
Imetengenezwa na Becky Dale na Christine Jeavans; ubunifu wa Debie Loizou; utengenezaji wa Scott Jarvis na Katia Artsenkova