WHO linaonya mlipuko wa maradhi ya Ebola unaelekea kuwa 'jambo la kawaida'

kaburi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Familia ikizuru kaburi la mpendwa wao aliyefariki kutokana na Ebola mjini Butembo

Shirika la afya duniani WHO limeonya kuwa maisha ya binadamu yanaingia katika mkondo mpya ambapo mikurupuko mikubwa ya magonjwa kama Ebola yanakuwa maradhi ya kawaida.

Mkurugenzi mkuu wa kushughulikia majanga ya dharura ya kiafya wa WHO Dkt Michael Ryan ameiambia BBC kuwa mikurupuko kama Ebola huenda ikaongezeka na kuwa mikubwa kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, kuharibiwa kwa misitu, idadi kubwa ya watu kuhama kutoka eneo moja hadi jingine, serikali zisizo thabiti na mizozo.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inakumbwa na mkurupuko wa Ebola, huo ukitajwa wa pili mkubwa katika historia, miaka mitatu tu baada ya janga la Ebola kuziathiri nchi kadhaa za Afrika Magharibi.

WHO imesema juhudi kubwa zinahitajika kuweza kukabiliana na majanga ya kiafya kama Ebola, kipindupindu na homa ya manjano.

Presentational grey line

Ebola ni nini?

  • Ebola ni ugonjwa unaoambukizwa na virusi ambapo aliyepata maambukizi hupata dalili za homa, uchovu, maumivu ya viungo na koo.
  • Kisha mgonjwa hutapika, kuharisha na kutoka damu.
  • Watu huambukizwa kwa njia ya kugusana, njia ya mdomo na pua, pia kwa njia ya damu, matapishi, kinyesi,majimaji ya kwenye mwili wa mtu mwenye Ebola
  • Wagonjwa hupoteza maisha kutokana na kupungukia maji mwilini na viungo kushindwa kufanya kazi.
Presentational grey line

Kumekuwwa na visa 2,025 vya ugonjwa wa Ebola na vifo 1,357 kutokana na mlipuko wa ugonjwa huo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Mlipuko mkubwa zaidi katika eneo la Magharibi mwa Afrika ulitokea kati ya mwaka 2014 na 2016 na uliwathiri watu 28,616 hususan katika mataifa ya Guinea, Liberia naSierra Leone.

Kuliripotiwa vifo 11,310 wakati huo japo mikurupuko mingine 12 iliwahi kushuhudiwa kati ya mwaka 2000 na 210 ambapo visa chini ya 100 viliripotiwa

Maelezo ya sauti, mahujaji wa DRC wazuiwa kuingia Uganda kutokana na tisho la Ebola

Kwanini mikurupuko ya sasa ni mikubwa zaidi?

"Tunainigia katika katika mkondo mpya ambapo mikurupuko mikubwa ya magonjwa kama Ebola yanakuwa maradhi ya kawaida na sio Ebola pekee,"Mkurugenzi mkuu wa kushughulikia majanga ya dharura ya kiafya wa WHO Dkt Michael Ryan ameiambia BBC.

Aamesema ulimwengu unakabiliwa na " hali ya hatari" ambayo inachangia kuongezeka kwa magonjwa hatari kama vile Ebola, kipindupindu na homa ya manjano.

Dr Ryan ameongeza kuwa Shirika la Afya Duniani linafuatilia kwa karibu visa 160 vya magonjwa kote duniani na tisa kati ya visa hivyo ni vimetajwa kuwa majanga ya kiwango cha tatu (ambyo ni kiwango cha juu zaidi cha majanga ya dharura ya kiafya kulingana na WHO).

Alsema: "Sidhani tumewahi kuwa katika hali ambapo tunashughulikia majanga mengi ya dharuru ya kiafya kwa wakati mmoja

"Hii ni hali mpya ambayyo imeanza kuwa ya kawaida, Sioni visa vya hivi vikibadili au kupungua."

Kutokana na hilo ametoa wito kwa mataifa na mashirika mengine "kujiandaa kwa majanga mengine kama haya".

Vikosi vya usalama vya DR Congo vikijiandaa kutoa usalama kwa msafara wa wafanyikazi wa afya

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Vikosi vya usalama vya DR Congo vikijiandaa kutoa usalama kwa msafara wa wafanyikazi wa afya

Mlipuko wa ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inaendelea kuwapa wasiwasi maafisa wa afya .

Iilichukua siku 224 kwa idadi ya visa vya ugonjwa huo kufikia 1,000, lakini siku 71 baadaye visa hivyo vilifikia 2,000.

Juhudi za kukabiliana na ugonjwa huo ziliathiriwa pakubwa na ghasia katika eneo la mashariki mwa tatifa hilo - kati ya Januari na Mei ambapo vituo vya afya vilishambuliwa mara 40.

Tatizo lingine ni kuwa badhi ya watu hawawaamini watoa huduma za afya, hivyo hufanya watu wenye dalili za ugonjwa huo kukwepa matibabu, hali ambayo inafanya kuwa vigumu kuzuia kuenea kwa virusi vya Ebola.

Mgonjwa wa Ebola akipakiwa kwenye gari kupelekwa kituo cha matibabu

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mgonjwa wa Ebola akipakiwa kwenye gari kupelekwa kituo cha matibabu

Dr Josie Golding, Mkuu wa kitengo kinachoshughulikia majanga ya dharura ya kiafya katika shirika la Wellcome Trust, amesema ulimwengu unahitaji kuongeza juhudi zaidi za kukabiliana na milipuko ya magonjwa kama haya.

Aliambia BBC: "Maambukizi ya Ebola Afrika Magharibi, yalichochewa zaidi na kutangamana kwa watu katika maeneo ya mpakani - na huo ndi ulimwengu tunaoishi sasa na hatuna uwezo wa kukomesha hilo ."

Aliongeza kuwa mabadiliko ya hali ya hewa huenda yakachangia milipuko mingi ya maradhi kwa mfano kipindundu baada ya kimbunga Idai kupiga Msumbiji,lakini anatumai kuwa magonjwa yanayotokana na mzozo wa kibinadamu yatakua ya kawaida.

"Jambo la msingi ni kujiandaa vizuri kukabiliana nayo kwa mfano tukiona watu wakikimbilia sehemo nyingine kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, tunahitaji kujipanga zaidi."