Mwanamuziki wa hip hop wa Uganda Jose Chameleone aingia siasa

Chanzo cha picha, Chameleone/Tweeter
- Author, Na Dinah Gahamanyi
- Nafasi, BBC Swahili
- Muda wa kusoma: Dakika 2
Nyota wa muziki wa Hip hop nchini Uganda Jose Chameleone leo amefuata nyayo za Bobi Wine na kuingia katika siasa.
Inaelekea umekuwa ni mtindo wa kawaida kwa wanamuziki maarufu kugeuka kuwa wanasiasa.
Bobi Wine amekuwa akizingirwa na utata wa kisiasa tangu alipogombea kiti cha ubunge mwaka 2017.
Sasa, Jose Chameleone, ambaye jina lake halisi ni Joseph Mayanja, amesema kuwa anataka kuwa Meya wa mji mkuu wa Uganda Kampala. Amenukuliwa na gazeti la Uganda Observer akieleza.

Chanzo cha picha, AFP
Chameleone ni mmoja wa wanamuziki maarufu katika eneo la Afrika Mashariki.
Moja ya nyimbo zake zinazofahamika ni ule wa Shida za Dunia, unaozungumzia matatizo yanayowakabili watu:
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Akielezea matarajio yake, amesema:"Wakati huduma zinapokuwa katika hali mbaya, watu wanaanza kuamka ...Watu wana kiu ya uongozi unaofaa na hawajaupata".
"Wale wanaodhani kuwa ni mkumbo wa Bobi Wine wana ukweli kiasi fulani ," Chameleone alinukuliwa akisema..
Bobi Wine alipiga kengele halafu akasema 'Tumekuwa watu wazima wa kutosha sasa ; Tunaweza kufanya hili '. Kwani kuna shida gani ya kufanya hilo? Kila kitu katika dunia hii kina mtu fulani aliyekianzisha ."
Chameleone anakiri kuwa ameshawishiwa na Bobi Wine. Muimbaji huyo wa kibao ''Badilisha'' anaaminiwa kuwa amekuwa mfuasi wa chama tawala cha NRM, ambapo amekuwa akitumbuiza kwenye matukio ya chama hizo.
Chameleone hakuficha urafiki wake na mbunge wa Kyadondo mashariki Bobi Wine, hususan pale Wine alipojipata katika utata wa kisiasa na kukamatwa na maafisa wa polisi na kuwekwa mahabusu. Alimtembelea mahabusu kumfariji:
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Bwana Chameleone amekuwa akionyesha nia yake ya kuwa mwanasiasa kupitia jumbe zake za Tweeter.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 3

Mwisho wa X ujumbe, 4

Mwisho wa X ujumbe, 5
Bobi Wine, ambaye Jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi, alichaguliwa kuwa mbunge alipogombea kiti hicho kama mgombea binafsi mwaka 2017.
Tangu kuchaguliwa kwake amekwishafanya maandamano maarufu na amekuwa akikamatwa na kushtakiwa kwa uhaini. Anadai kuwa alipigwa na polisi alipokuwa katika mahabusu ya polisi.