Bobi Wine akamatwa upya muda mfupi baada ya kuondolewa mashtaka na mahakama ya jeshi Uganda

Bobi Wine

Chanzo cha picha, AFP

Muda wa kusoma: Dakika 3

Mbunge wa Kyadondo nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine ameshtakiwa kwa uhaini nchini.

Alikamatwa muda mfupi baada ya mahakama ya kijeshi kumuondolea mashtaka ya umiliki haramu wa silaha nchini.

Wine alikamatwa upya na kushtakiwa katika mahakama ya hakimu mkuu kujibu mashtaka ya uhaini pamoja na wabunge wengine waliokamatwa.

Mbunge huyo ambaye pia ni mwanamuziki nchini kwa jina maarufu Bobi Wine leo aliwasilishwa katika mahakama ya kijeshi mjini Gulu kaskazini mwa Uganda.

Mawakili wake awali walijuzwa kuwa kesi itasikilizwa katika kambi ya kijeshi ya Makindye anakozuiliwa mjini Kampala.

Kumekuwa na shinikizo kubwa kimataifa la kutaka Bobi Wine aachiwe huru.

Wengi nchini Uganda wanatazama kesi hii kama jitihada za kumnyamazisha mkosoaji mkuu wa serikali aliyechaguliwa kuwa mbunge mwaka jana tu.

Mawakili wa jeshi wameeleza mahakama kuwa mashtaka dhidi ya Wine yameondolewa na kwamba mwanasiasa huyo akabidhiwe kwa polisi ili akabiliwe na mashtaka ya uhaini pamoja na na wabunge wengine waliokamatwa .

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Wakili wake Wine Medard Segona ameiambia mahakama kwamba licha ya kuwa wameridhishwa na hatua ya mahakama ya kijeshi , anapinga hatua ya sasa ya mteja wake kuhamishwa katika mahakama ya kiraia kukabiliwa na mashtaka mapya.

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Alitaka mbunge huyo aachiwe huru ili aweze kupelekwa kupokea matibabu.

Mahakama iliamua kuwa Bobi Wine yu huru, iwapo hakuna mashtaka mengine yatakayowasilishwa dhidi yake.

Wakati huo Wine alionekana akilia na kupangusa machozi huku hukumu hiyo ikisomwa. Alitoka nje ya mahakama akiwa anatemba kwa magongo na kuonekana kuwa na maumivu makali.

Nchini Kenya raia walimiminika katika mji mkuu wa Nairobi leo kushinikiza kuachiwa kwa Bobi Wine
Maelezo ya picha, Nchini Kenya raia walimiminika katika mji mkuu wa Nairobi leo kushinikiza kuachiwa kwa Bobi Wine

Hapo ndipo alipokamatwa upya.

Shinikizo kubwa kutaka Wine aachiwe

Jitihada za kumshtaki Bobi Wine mbele ya mahakama ya kijeshi zimekabiliwa na shutumA kubwa kimataifa na hata miongoni mwa makundi ya kutetea haki za binaadamu.

Nchini Kenya raia walimiminika katika mji mkuu wa Nairobi leo kushinikiza kuachiwa kwa mbunge huyo wa upinzani Uganda.

Mjini Kampala Polisi imemkata kiongozi mkuu wa upinzani Kizza Besigye.

Besigye amakamatwa mara kwa mara katika jitihada za maafisa wa utawala kuzuia maandamano ya kuipinga serikali kufanyika.

Maelezo ya video, Kizza Besigye: Upinzani Afrika usishurutishwe kukubali matokeo kwa kusingizia utulivu

Besigye alikamtwa mapema leo alipojaribu kuondoka nyumbani kwake Kasangati; na inaarafiwa amefikishwa katika kituo cha polisi cha Naggalama Uganda.

Awali polisi walizingira makaazi yake.

Kwa upande mwingine, Wanamuziki wakubwa wakiwemo Chris Martin , Angelique Kidjo na Damon Albarn, wametoa wito wa kuachiwa kwa Mbunge Bobi wine ambaye ana wiki sasa tangu kukamatwa kwake na mbunge mwezake na zaid ya watu 30. Wasanii hao wamejaza waraka wa kutaka mbunge huyo wa upinzani kuachiwa.

Waraka huo umeanzishwa na Rikki stain aliekua msimamizi wa zamani wa mawamuziki fella kuti ambae alikua mkosoaji mkubwa wa serikali ya Nigeria

Anasema kuwa likua akipigwa hata kwa kuzungumza.

Zaidi ya watu 80 akiwemo mwandishi mkongwe whole soyinka na wanamuziki wa kundi la U2 bassist Adam Clayton, muambiaji kiongozi Chrissie Hynde na Genesis Peter Gabriel.

Zaidi ya wasanii 80 wanataka Bobi wine aachiwe Huru akiwemo Chris Martin (kustoto), Angelique Kidjo (katikati) na Damon Albarn (kulia)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Zaidi ya wasanii 80 wanataka Bobi wine aachiwe Huru akiwemo Chris Martin (kustoto), Angelique Kidjo (katikati) na Damon Albarn (kulia)

Bobi Wine ni nani?

Nyota huyo wa mtindo wa Afrobeats aliingia katika taaluma ya muziki katika miaka ya 2000, hna anaelezea kipaji chake kuwa ni cha kuelimisha na kuburudisha. Mojawapo ya vibao vyake vya awali Kadingo, inahusu usafi wa mwili.

Jina lake rasmi Wine, ni Robert Kyagulanyi Ssentamu, alichaguliwa kuwa mbunge katika uchaguzi mdogo baada ya kusimama kama mgombea huru mwaka jana wilayani Kyadondo mashariki, Uganda ya kati.

Aliwashinda wagombea kutoka chama tawala National Resistance Movement (NRM) na chama kikuu cha upinzani Democratic Change (FDC).

Bobi Wine akiwa na wafuasi wake

Chanzo cha picha, AFP

Baada ya kutangazwa mshindi, aliahidi kuangazia zaidi kuwaunganisha raia.

"Jambo langu la kwanza ninalotaka kufanya ni kufanikisha maridhiano kati ya viongozi wa Kyadondo Mashariki...Ninataka siasa zitulete pamoja... jinsi muziki ufanyavyo."