Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ni wakati wa kudhibiti matumizi ya sukari kama ilivyo kwa tumbaku?
Kwa kipindi cha muongo mmoja, uvutaji sigara umekua ukipigwa marufuku
Nchini Uingereza kupigwa marufuku kwa uvutaji sigara mwaka 2007 mpaka kuanzishwa kwa vifungashio vilivyo vitupu ili kuwafanya watu waondokane na tabia hatarishi.
Na sasa kuna dalili kuwa sukari inaelekea huko pia
Vinywaji vyenye sukari tayari vinakatwa kodi-na sasa shirika la think tank limeeleza kuwa pipi,vitafunwa na vinywaji vyenye sukari vyapaswa kuwa na vifungashio visivyovutia, ili kupunguza matumizi ya vyakula vyenye sukari.
Wito umetolewa na taasisi ya utafiti wa sera ya Umma ya IPPR, katika ripoti yao mpya.
Mkurugenzi wa IPPR Tom Kibasi anaamini hatua hii italeta mabadiliko tofauti.
''Vifungashio vitupu vitatusaidia kufanya uchaguzi sahihi'' Ameeleza.
Anataka njia hiyo iende sambamba na hatua zilizochukuliwa, kama kuzuia vyakula visivyo na manufaa mwilini (Junk food) kwa kupiga marufuku matangazo yake.
Je hatua hii ya vifungashio visivyovutia inaweza kuwa suluhu
Soko dhidi ya hatua hii
Wataalamu wa mambo ya masoko wamekuwa watu wa kukosoa haraka sana njia hii, chombo kiachosimamia biashara ya vyakula na vinywaji kimesema kuwa kutangaza bidhaa ni ''uhuru wa biashara'' na ni vigumu kushindana kwenye soko''.
Hoja hiyo hiyo ilitolewa pia na wanaosimamia soko la tumbaku, lakini serikali ya Uingereza inaonekana kutilia ngumu suala hilo.
Lakini serikali haijatoa njia hiyo ya vifungashio kama suluhu kamili, badala yake imesema inasubiri afisa mkuu wa idara ya afya Profesa Dame Sally atoe maoni yake.
Kwanini? imeelezwa kuwa hatua kali zinahitajika kuchukuliwa ikiwa malengo ya kupunguza matatizo ya uzito mkubwa kwa asilimia 50 kwa watoto yanahitaji kufikiwa ifikapo 2030.
Dame Sally ametakiwa kuzipitia upya njia hizo.
Dame ameeleza njia ya kutimiza azma hiyo ni kuongeza kodi kwa vinywaji vyenye sukari na vyakula vingine visivyo na umuhimu kiafya.
Kwa upande wa kudhibiti uvutaji sigara hatua zilizochukuliwa zinazonyesha zinafanya kazi-idadi ya wanaovuta sigara imepungua kwa kiasi cha theluthi katika kipindi cha miaka 10.
Ushahidi kutoka Australia-nchi ya kwanza kuanzisha vifungashio vitupu kwa bidhaa za tumbaku ambapo idadi ya wavutaji walipungua kwa kiasi cha robo.