Ni mwiko sasa kunywa au kuuza pombe za viroba Uganda

Waganda wanahofia kuwa marufuku ya viroba itawashinikiza wanywaji kununua pombe haramu
Maelezo ya picha, Waganda wanahofia kuwa marufuku ya viroba itawashinikiza wanywaji kununua pombe haramu

Uganda imepiga marufuku unywaji na uuzaji wa pombe zinazouzwa kwenye mifuko ya plastiki au viroba ambavyomaafisa wanasema kuwa vina madhara makubwa ya kiafya.

Viroba hivyo vya pombe za spiriti au Konyagi - wakati mwingine huwa na kiwango cha kileo cha asilimia 45 kilichokubaliaka - hupendelewa zaidi na wanywaji wenye mapato ya chini kwababu huwa vinauzwa kwa bei ya chini , sawa na senti 13 za Marekani.

Waganda ni miongoni mwa wanywaji wakuu wa pombe barani Afrika.

Watengenezaji wa vinywaji hivyo nchini Uganda sasa watatakiwa kusindika vinywaji vyao kwenye machupa yenye ukubwa wa chini ya mililita 200.

Viroba vimekuwa vikibebwa mifukoni na kwenye mikebe ya hesabu ya watoto wa shule, amesema waziri wa Uganda
Maelezo ya picha, Viroba vimekuwa vikibebwa mifukoni na kwenye mikebe ya hesabu ya watoto wa shule, amesema waziri wa Uganda

Waziri wa biashara na vyama vya ushirika nchini Uganda Amelia Kyambadde ameiambia BBC kuwa viroba vilikuwa hata vinanunuliwa na watoto wa shule.

" Kwasababu vinywaji hivi ni nafuu , watu huvibeba ndani ya mikoba yao, mikebe ya zana za hesabu (mathematical sets) , na mifukoni mwao . Unywaji wake umekuwa ni wa kiwango cha juu sana ," amesema.

Mwandishi wa BBC mjini Kampala Dear Jeanne anaripoti kuwa Waganda wanahofia kuwa marufuku ya viroba itawashinikiza wanywaji kununua pombe haramu.

Unaweza pia kusoma:

Uganda ni nchi ya saba kwaunywaji wa pombe barani Afrika kwamujibu wa ripoti ya dunia kuhusu unywaji wa pombe ya shirika la Afya duniani WHO ya mwaka 2018.

Asilimia 21% ya Waganda hujihusisha na unywaj wa pombe wa kupindiukia , WHO linasema.

Marufuku hiyo ni moja ya hatua chache ambazo zimechukuliwa na Uganda kujaribu kukabiliana na unywaji wa pombe kupindukia.

Haina sera ya taifa juu ya pombe, na kuna udhibiti mdogo sana wa vileo na matangazo

Hata hivyo, serikali inasema kuwa inaandaa sheria ya kudhibiti ,utengenezaji wa pombe nyumbani.

Nchi jirani ya Tanzania pia ilipiga marufuku viroba mwaka 2017.

Unaweza pia kutazama:

T