Mgogoro Sudan wachukua sura mpya baada ya wanajeshi kuwakabili waandamanaji

mAANDAMANO sUDAN

Chanzo cha picha, AFP/GETTY IMAGES

Muda wa kusoma: Dakika 2

Vikosi vya ulinzi nchini Sudan vimetumia nguvu kujaribu kuwatawanya waandamanaji waliokita kambi nje ya makao makuu ya jeshi jijini Khartoum.

Kwa mujibu wa waandamanaji hao, milio ya risasi imekuwa ikisikika na tayari watu nane wameripotiwa kufa na kadhaa kujeruhiwa kwenye rabsha hizo.

Sudan imekuwa chini ya utawala wa Baraza la Kijeshi la Mpito toka Rais Omar al-Bashir alipinduliwa mwezi Aprili.

Waandamanaji wamekuwa wakilazimisha utawala urejeshwe mikononi mwa serikali ya kiraia.

"Kwa sasa kuna jaribio la kutawanya waandamanaji waliokita kambi," imeeleza taarifa fupi kutoka kwa Jumuiya ya Wataalamu wa Sudani amabo ndio waratibu wa maandamano hayo ya kitaifa.

Mashuhuda wanasema kuwa kwa sasa waandamanaji wanachoma matairi na kuweka vizingiti ili kuwazuia maafisa usalama kuwafikia.

Mwanahabari Benjamin Strick, ambaye amebobea katika kusanifisha picha zinazotumwa kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, ametuma video kadhaa za kile kinachoendelea kwa sasa katika jijila Khartoum.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Jeshi la Sudani mpaka sasa bado lipo kimya juu ya kinachoendelea.

Waandamanaji wamekita kambi mbele ya makao makuu ya jeshi toka Aprili 6 mwaka huu, siku tano kabla ya Bashir kupinduliwa na jeshi.

Mwezi uliopita, viongozi wa waandamanaji na majenerali wa jeshi walitangaza kuwa wamefikia muafaka wa muundo wa serikali ya mpito ya miaka mitatu ambayo itaandaa uchaguzi wa kiraia.

Lakini wamesema bado wanatakiwa kufanya maamuzi ya nani aingie kwenye baraza huru ambalo ndilo litakuwa na maamuzi ya mwisho kwenye kipindi cha mpito cha miaka mitatu.

Hapajaweza kufikiwa makubaliano juu ya upande upi baina ya raia na wanajeshi uwe na wawikilishi wengi kwenye baraza hilo.

Presentational grey line

Safari ya mabadiliko

Women protesting

Chanzo cha picha, AFP

line
  • 19 Desemba 2018 - Maandamano yanalipuka baada bei ya mafuta na mkate kupanda
  • 20 Desemba 2018 - Waandamanaji jijini Khartoum waanza kuimba nyimbo dhidi ya serikali wakitaka "uhuru, amani, haki"
  • 22 Februari 2019 - Rais Omar al-Bashir atangaza hali ya hatari na kuvunja baraza la mawaziri
  • 24 Februari - Maandamano yanaendelea licha ya vyombo vya ulinzi kutumia silaha za moto kutawanya waandamanaji
  • 6 Aprili - Wanaharakati waanza kukita kambi mbele ya makao makuu ya jeshi wakiapa hawataondoka mpaka Bashir ang'oke madarakani
  • 11 Aprili - Majenerali wa jeshi wanatangaza kuwa Bashir ameng'olewa uongozini laki waandamanaji wasalia wakitaka serikali ya kiraia
  • 17 Aprili - Bw Bashir anapelekwa jela jijini Khartoum
  • 20 Aprili - Mazungumzo baina ya viongozi wa kijeshi na wawakilishi wa waandamanaji yanaanza
  • 13 Mei - Shabulio la risasi nje ya makao makuu ya jeshi linasabisha watu sita kuuawa
  • 14 Mei - Majenerali na viongozi wa raia wanatangaza mapatano ya kuunda serikali ya mpito ya miaka mitatu
  • 16 Mei - Mazungumzo yanaahirishwa baada ya jeshi kutaka baadhi ya vizuizi kuondolewa
map
presentational grey line