Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Urusi 'huenda' inafanya majaribio ya nyukilia, maafisa wa Marekani wameeleza
Huenda urusi inakiuka mkataba wa nuklia kwa kufanya majaribio ya silaha za nyukilia zisizo na nguvu kubwa katika eneno la Arctic, Afisa wa juu wa intelijensia wa Marekani ameeleza.
Luteni Jenerali Robert Ashley, Mkurugenzi wa taasisi ya intelijensia ya Marekani, amesema Moscow ''pengine inakiuka '' sheria za mkataba.
Alikua akimaanisha mkataba wa pamoja wa Comprehensive Test Ban Treaty (CTBT) unaozuia majaribio ya nuklia.
Urusi, ambayo ilitia saini mwaka 2008, inasema inaunga mkono mkataba wa CTBT.
Marekani imetia saini lakini haijaanza kutekeleza mkataba huo.
''kwa uelewa wetu uendelezwaji wa silaha za nuklia unatusababisha tuamini kuwa shughuli za majaribio ya Urusi zitasaidia kuboresha uwezo wa silaha za nyukilia,'' alisema Luteni Jenerali Ashley.
Ameongeza kuwa Marekani ilitegemea Urusi, ambayo amesema ilikua inategemewa kujaribu silaha zake katika visiwa vya Zemlya, ili kuongeza ubora wa silaha za nuklia kwa kipindi cha muongo mmoja ujao.
Lakini wachambuzi wa mambo wamepokea taarifa hiyo ambayo hata hivyo haikuwashawishi. Shirika linalosimamia utekelezaji wa makubaliano ya mkataba wa nyukilia CTBTO imesema kwenye taarifa yake kuwa haishuku shughuli zozote zinazokwenda kinyume na mkataba.
CTBT, ambao inapiga marufuku majaribio ya silaha za nyukilia popote pale duniani, ulifikiwa na Mkutano mkuu wa umoja wa mataifa mwaka 1996.