Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Brexit: Theresa May kujiuzulu kama Waziri Mkuu Uingereza Juni 7
Theresa May kujiuzulu kama kiongozi wa chama cha Conservative tarehe 7 Juni na kutoa fursa kuidhinishwa mchakato wa kuchaguliwa waziri mkuu mpya Uingereza.
Katika taarifa iliojaa hisia alioitoa huko Downing Street, Bi May amesema amefanya "kila awezalo" kutekeleza matokeo ya kura ya maoni kuhusu EU ya mnamo 2016.
Ni jambo linalosalia kuwa "na majuto mengi" kwamba ameshindwa kutimiza Brexit - Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya, ameongeza.
Lakini waziri mkuu mpya ndio suluhu " kwa manufaa ya taifa".
Bi May amesema ataendelea kuhudumu kama waziri mkuu wakati kukitarajiwa kuidhinishwa mchakato wa kumchagua kiongozi mpya wa chama cha Conservative.
Atajiuzulu kama kiongozi wa chama hicho Juni 7 na uteuzi wa waziri mkuu mpya unatarajiwa kuanza wiki inayoafuata baada ya hatua hiyo.
Sauti yake ilittereka na alikuwa mwingi wa hisia alipomaliza hotuba yake akisema: "Nitaondoka katika wadhifa huu hivi karibuni lakini imekuwa heshima kubwa maihsani mwangu kuhudumu.
"Waziri mkuu mwanamke wa pili, na bila shaka sio wa mwisho.
"Nachukua hatua hii bila ya uovu wowote, bali na shukrani za dhati na kubwa kutokana na kupata fursa kuitumikia nchi ninayoipenda."