Nigeria: Mtoto aliyetekwa ili kuwaongoza walemavu wa macho kuomba mtaani

Illustration showing Samuel Abdulraheem riding on a bike aged seven

Licha ya kutokea kwenye familia kubwa ya baba mwenye watoto 17 na wake wanne. Samuel alikuwa peke yake siku hiyo pamoja na mlezi wake.

Familia yake iliambiwa kuwa alikuwa nje anaendesha baiskeli.

Hawakujua kuwa hawatamuona tena kwa kipindi cha miezi sita.

Short presentational grey line

Jinsi walivyomtafuta

Hakuna ambacho hatukufanya katika kujaribu kumtafuta," dada yake Firdausi Okezie mkubwa alikumbusha.

Akiwa na umri wa miaka 21, alikuwa hajataarifiwa kuhusu kupotea kwa mdogo wake.

Mdogo wake wa kiume alikuwa anafurahia sana kukimbilia kupokea simu na kuongea naye wakati yeye alipopiga simu akiwa chuo kikuu.

Hivyo wakati simu ilipoanza kupokelewa na watu wengi kila mara alipopiga alipata wasiwasi kuwa kuna kitu ambacho hakiko sawa.

Siku moja baada ya masomo yake ,Firdausi aliamua kurudi nyumbani bila kutoa taarifa na ndipo baba yake ilimbidi aseme ukweli ambao ulikuwa unamuumiza.

Firdaus alisikitika kwa kutopata taarifa kuwa mdogo wake mpendwa amepotea kwa zaidi ya mwezi .

Samuel Abdulraheem and his mother when he was a toddler

Chanzo cha picha, Abdulraheem family

Maelezo ya picha, Samuel akiwa na mama yake ,miaka michache kabla hajapotea

"Awali, baba yangu alimfunga mlezi aliyekuwa anamuangalia mtoto lakini baada ya uchunguzi, aliachiwa huru,"Firdausi alisema.

Walijaribu kuficha taarifa hizi kwa mama yake Samuel, ambaye alikuwa ameachana na baba yao kwa muda.

Kila mara anapopiga simu au kuja kumtembelea huwa wanampa sababu mbalimbali za uongo.

Lakini baadae, mjomba alipewa jukumu la kumwambia mama yake ukweli.

Vilevile polisi waliongeza uchunguzi , familia iliweka tangazo katika gazeti na kuomba msaada kwa viongozi wa dini wa kikristo na kiislamu.

Ilifikia wakati ambapo baba yao aliwaomba wakubali kuwa kaka yao amekufa tayari kwa sababu wametumia kila njia bila mafanikio ya kumpata.

Short presentational grey line

Firdausi alikataa kukata tamaa. Aliamua kuandika juu ya kupotea kwa mdogo wake katika utafiti wa masomo ya juu mwaka mmoja baada ya kuhitimu masomo yake, alihama kutoka kusini kwenda Lagos kutafuta kazi.

Alibadili dini na kuwa mkristo na kuwa anahudhuria kanisa la 'Winners Chapel' moja ya makanisa makubwa yanayopatikana katika mji wa Ogan nje kidogo ya mji.

Kila mwezi desemba, kanisa huwa linawakusanya waumini kutoka maeneo mbalimbali duniani kwa ajili ya maombi ya muda wa siku tano.

Illustration showing Firdausi Okezie recognising her brother

Wakati shughuli hiyo inayofahamika kama 'Shiloh' ikiwa inawavutia mkusanyiko mkubwa wa watu kuja kusali na hata kufanya biashara ndogondogo nje ya kanisa.

Mwaka 2000, Firdausi akiwa bado hana ajira aliamua kuweka meza ambayo alikuwa anauza nguo ambazo zilikuwa zimetengenezwa na mama yake.

Wakati akiwa anasubiri fundi aje kumsaidia kufunga meza yake, alikaa kwenye kiti huku kichwa chake kikiwa kinaangalia juu.

Hapo ndio wakati alisikia sauti ya ombaomba ikimuomba msaada kwa jina la Mungu. Firdausiakiwa akiwa anaangalia juu.

Muombaji huyo alikuwa alikuwa ameshika fimbo na mkono wake wa kushoto ulikuwa umemshika kijana mdogo.

Firdausi alipiga kelele na kumkumbatia kijana huyo aliyekuwa anamuongoza muombaji kwa kuwa alikuwa ndio kaka yake aliyepotea.

Short presentational grey line

Utekaji

Samuel, sasa ana umri wa miaka 30, hakumbuki vizuri namna gani aliibiwa kutoka kwa familia yake, "Ninachokikumbuka ni safari ya gari moshi".

Alichukuliwa na mwanamke mmoja ambaye alikuwa na mkono mmoja anayeishi nje kidogo ya mji wa Lagos eneo ambalo lina idadi kubwa ya ombaomba.

Mwanamke huyu aliwaajiri ombaomba wenye ulemavu wa macho ambao walitakiwa kupeleka kwake dola 5 kila siku.

Walemavu hawa wanawake kwa wanaume huwa wanazungukamitaani wakiwa wanaongozwa na watoto wanojulikana kama watoto wa mtaani haswa katika maeneo ya foleni, kanisani na misikitini.

Samuel peke yake alikuwa analala na mama huyo katika mkeka kwenye kibanda chake.

Kwa miaka mingi, alisema wavulana wengine watano walikuja kukaa na mama huyo na kufanya kazi na ombaomba ambao walikuwa wamekodiwa.

Illustration showing a yard with blind beggars and their guides

Samuel anahisi kuwa lazima mama huyo alikuwa amefanya kitu ili kuwasahaulisha kufikiria nyumbani , maisha yao kila siku yalikuwa ni kuamka na kwenda kuomba hela , kula na kulala.

Short presentational grey line

Maisha ya utumwa

Ombaomba mbalimbali walikuwa wanaajiriwa kwa wiki au mwezi.

Mwisho wa siku , Samuel na ombaomba wengine walikuwa wanalala pembezoni mwa maeneo ya wazi.

Kama ombaomba alifurahi kufanya kazi na mimi, walikuwa wanamkodi kwa mara nyingine.

"Nilikuwa kama mtumwa, nilikuwa siwezi kusema nataka kuondoka au nataka kufanya kitu chochote."

Samuel aliweza kuwa na marafiki wachache ambao alikuwa anacheza nao mara chache jioni anaporudi kutoka kuomba.

Illustration showing Samuel Abdulraheem as a boy guiding a blind beggar

Wakati mwingine watu huwa wanawapa chakula wakati wanapokuwa wanaomba, na mara nyingine inawabidi kwenda kwenye migahawa ili kupata mabaki ya chakula yaliyotupwa katika kapu la uchafu.

" Huwa ninakuwa nna njaa sana wakati wa mchana, huwa ni ngumu kukaa chini na kuanza kula wakati upo kazini," anakumbuka.

"Nilikuwa sioni kuwa kuomba ni kitu kibaya au ombaomba ni wabaya. Niliona kuwa wanaamka na kwenda kazini kila siku."

Short presentational grey line

'Miujiza'

Tukio la Firdausi kukutana na mdogo wake lilikuwa la kushangaza sana na dada huyo aliona kuwa ni muujiza ambao umemtokea katika maisha yake.

"Nilianguka chini na kupiga kelele", Samuel alikuwa haelewi sababu inayomfanya dada huyo kupiga kelele.

"Ilinichukua muda lakini nilihisi ni mtu ambaye ananifahamu au nna undugu naye" Samuel alisema.

David Oyedepo

Chanzo cha picha, @davidoyedepoministries

Maelezo ya picha, David Oyedepo, muasisi wa Winners Chapel, alimuombea Samuel

Baada ya muda watu walikusanyika kwa wingi katika eneo hilo, pamoja na viongozi wa dini walifika na kumtaka Firdausi kusimulia mkasa wa miujiza iliyomtokea.

Presentational grey line
Presentational grey line
Short presentational grey line

Firdausi anajilaumu kwa kushindwa kusaidia watoto wengine ambao walikuwa wametekwa pamoja na kaka yake.

Samuel Abdulraheem Firdausi Okezie

Chanzo cha picha, Firdausi Okezie

Maelezo ya picha, Samuel akiwa na dada yake , miaka miwili baada ya kupatikana

"Katika nchi zinazoendelea, mtu anapaswa kwenda kutoa taarifa polisi kufuatilia jambo hilo lakini hapa polisi watakuambia uwape ela ya mafuta na wakati huo sikuwa hata na ajira," Firdausi alisema.

Short presentational grey line

Mwanafunzi

Miaka sita ya kutopata elimu ya darasani, Samuel alirudishwa kuanza elimu ya msingi katika shule ya binafsi.

Samuel Abdulraheem

Chanzo cha picha, Samuel Abdulraheem

Maelezo ya picha, Samuel Abdulraheem

Baada ya miezi mitatu, alivukishwa kutoka darasa la kwanza mpaka la nne. Na ndani ya mwaka mmoja aliweza kufaulu na kuingia elimu ya sekondari.

Samuel alitumia miaka mitatu tu katika elimu ya sekondari na alipofika miaka 17 alijiona yuko tayari kujiunga na elimu ya masomo ya juu.

Aliweza kufaulu kwa kiwango cha juu na kuweza kuanza kusoma masomo ya uhandisi.

Short presentational grey line

Sasa Samuel anafanya kazi ya uhandisi.

Samuel Abdulraheem
Samuel Abdulraheem
If anyone asks for money, I'd rather buy them food. Because, back then, it was better giving me food than money because the money went to the beggar and none came to me"
Samuel Abdulraheem
Kidnap victim
Presentational white space

Samuel anasema kuwa hana chuki kwa wale waliofanya apitie maisha yale magumu kwa sababu anaamini wao ndio wametengeneza mafanikio yake ya sasa.

"Ni maisha tu na ninajaribu kuwa mtu mwema niwezavyo kwa watu" alisema Samweli.

Aidha aliongeza kuwa kumbukumbu cha kuwa na njaa kila mara wakati alipokuwa anaomba zinamfanya asiwape ombaomba fedha bali anawapa chakula.

Alitoa rai kuwa watu wanapowaona ombaomba wakiwa na watoto wamewasindikiza, wajiulize mara mbili labda huyo mtoto anayemsindikiza ombaomba anahitaji msaada, "usitoe tu fedha na kuondoka".