'Acha kujaribu kuniponya'

Chanzo cha picha, SARAH DOUSSE
- Author, Damon Rose
- Nafasi, BBC News
"Ni jambo la kawaida kwa watu wengi wenye ulemavu kukutana na ushawishi wa kutaka kuombewa hali yao ya ulemavu kama mimi.
Mara kadhaa nmekutana na wakristo ambao walikuwa wanataka kuniombea ili nipone.
Inawezekana walikuwa na dhamira nzuri lakini mara nyingi huwa najisikia vibaya na kuona kama wananihukumu kuwa nna mapungufu ambayo inabidi niyarekebishe au nirekebishwe.
Hivyo nilipanga kujua ni kitu gani ambacho wakristo huwa wanatoa kwa walemavu tofauti na ahadi zaidi ya tiba ya miujiza" mlemavu mmoja wa macho nchini Uingereza.
Simulizi ya maisha ya mlemavu mmoja wa macho
Bila ya kushawishiwa na yeyote , nilifika katika mtaa mmoja wa wakristo ambapo waliniambia kuwa wanataka kuniombea ili niweze kuona tena.
Tangu nimekuwa mlemavu wa macho nilipokuwa kijana mdogo , nimekutana na ushauri au maswali ya kuhusu ulemavu wangu kila mara jambo ambalo lilikuwa linaniudhi na lilikuwa linaninyima uhuru.
Jambo hili lilitokea mara ya kwanza nikiwa mtaa wa chini mjini London.
Treni ilikuwa imesimama na watu wengi walisimama kumshangaa mwanaume aliyeweka mkono katika bega langu na kuniuliza kama anaweza kuniombea ili niweze kuondokana na tatizo la upofu.
Lakini zaidi ya hayo, hapo baadae nilidhani kuwa kila mtu ambaye alikuwa amezunguka alikuwa anajua ukweli kuhusu maisha ya watu wa ulemavu.
Lakini siku moja nilipowaambia wafanyakazi wenzangu kuhusu mtu aliyejitokeza kuniponya kwa kigezo cha mimi kufuata dini yake,
waliongea kwa hasira na kusema kuwa mtu yeyote hawezi kulazimishwa kufuata imani fulani kutokana na shinikizo la kitu au mtu.

Ilifikia wakati ambapo nilikiri kuwa sina dini.
Ujumbe ambao nilipata kutoka kwa wakristo ambao walitaka kuniponya ulikuwa ni mmoja tu , "Yesu anaweza kuwaokoa watu wenye ulemavu".
Hivyo nitakapokubali kumfuata Yesu na kuwa mkristo nitapona.
Hata hivyo nilivutiwa kutaka kujua na kujifunza kutoka kwa baadhi ya walemavu wakristo kama huwa wanapitia changamoto kama zangu na huwa wanakasirika pia.
Mchungaji Zoe Hemming, wa kanisa moja katika kijiji cha Aston huko Shropshire, ambaye amekuwa akitumia kiti cha gurudumu kwa sababu ya ulemavu wa muda mrefu na akiwa anaishi katika maumivu makali .
Mchungaji huyo aliniambia kuwa alikuwa anapata wakati mgumu anapotoa huduma ya uponyaji kwa watu ambao hawafahamu na huwa anajihisi kuwa mbinu ambayo anaitumia ni kama haikubaliki.

"Kuna wakati nilikutana na mtu ambaye alikuwa mlemavu wa miguu na anatumia kiti cha magurudumu kama mimi na nilipaswa kutoa maombi ya uponyaji wa ulemavu wake .
Nilisikia minong'ono ya watu ya kuwa kuwa kwa nini niwaombee watu wengine na nisijiombee mwenyewe, jambo hilo huwa ninajihisi kudhaurika lakini huwa naacha kutilia maanani na kuendelea na kazi yangu ya kumuombea aliyekuja kupata huduma .
Lakini kiukweli huwa nnakasirika sana na kuishiwa nguvu ya kufanya kazi" Mchungaji mwenye ulemavu alieleza.
Mikono ya uponyaji
Wakristu ambao wanatoa huduma ya uponyaji huwa wanafanya hivyo kwa sababu za kidini, Yesu aliponya wagonjwa na aliwataka wafuasi wake kufuata njia hiyohiyo.
Shule ambazo nilisoma tulijifunza yote kuhusu miujiza ya Yesu ambayo aliifanya . Namna ambavyo alimponya mlemavu na akaweza kunyanyuka na kutembea.
Aliweza kumponya kipofu, alimponya mwanamke ambaye alikuwa ana upungufu wa damu na aliweza kumrudisha rafiki yake Lazaro kutoka mauti.

Jambo lingine ambalo lilikuwa linanipa msukumo ni ukweli kuhusu walemavu wengi kukatazwa kuabudu katika madhabahu chini ya sheria za dini za wakati huo, na kudaiwa kuwa hawakuwa safi.
Je, kama Yesu angekutana na mimi leo, mimi ambaye nina ajira yangu nzuri na mbwa ambaye ananiongoza, je, angeweza kufikiria kuwa nnahitaji uponyaji?
Kama yesu angekutana na mimi mtaani, sidhani kama angetaka kuniponya kwa namna hii ninayotaka kuponywa, sidhani kama Yesu angeniangalia katika jicho la kunionea huruma kuwa nnahitaji msaada.
Wengine walienda mbali zaidi na kufikiria kuhusu nini ambacho kimeandikwa katika biblia kuhusu ulemavu.

"Mungu angesema kuwa ananipenda sana. Ameniumba kwa mfano wake mwenyewe na ulemavu wangu haunifanyi niwe na mapungufu yeyote au kuwa tofauti na mtu asiyekuwa na ulemavu, anatupenda wote sawa."

Chanzo cha picha, SARAH DOUSSE
Licha ya ulemavu wangu matumaini yangu ni kuwa siku moja watu watabadili mtazamo juu ya watu wa aina yake.
Kwa kweli ninajipenda na nnapenda ulemavu wangu wa kuona na nnapenda vitu nnavyovifanya.
Siwezi kudai kuwa nnaweza kuponywa ulemavu wangu wa macho kwa matokeo ya maombi ya uponyaji lakini siwezi kusahau namna gani nina furaha na nnaridhika na muonekano wangu".














