Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwa nini wanaume hukaa kimya wanapofanyiwa unyanyasaji wa kijinsia?
Wanaume walioathirika na unyanyasaji wa kijinsia wakiwa watoto katika jamii ya watu weusi wamekuwa wakirudishwa nyuma na serikali, alisema kiongozi mmoja aliyewahi kufanyiwa unyanyasaji wa kingono wakati akisikiliza wanaume ambao walipitia unyanyasaji wa aina hiyo wakitaka suala lao liangaliwe kwa ukaribu.
" Nimjaribu kusahau lakini nimeshindwa. Nimejaribu kuendelea na maisha yangu lakini bado kitendo cha unyanyasaji nilichofanyika nikiwa mdogo bado kipo akilini mwangu", alisema Chris ambalo si jina lake halisi.
Chris aliongea mara baada ya chapisho la serikali nchini Uingereza kuchapisha ripoti likiwa linaelezea namna ambavyo waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia wanavyosaidiwa na serikali.
"Nilipokuwa na mika 11, huyo aliyenibaka alikwa alikuwa na kiongozi wa shule mwenye umri wa miaka 19".
Alikuwa analia wakati anasimulia mkasa wake.
"Nilivyobakwa nilijiona sina thamani tena, Niliugua kwa muda, Nadhani ilikuwa ni sonona ingawa ukiwa mtoto unakuwa huelewi mambo hayo.
Hilo jambo lilinichanganya sana na kubadilisha utu wangu mpaka leo, ni kovu ambalo ninalo gumu kulikabili."
Chris anasema bado anaishi katika maumivu. Ilimchukua miaka mingi kutafuta msaada.
Sikuongea na mtu yeyote kuhusu jambo ambalo nilifanyiwa. Wala sikutoa taarifa kwa vyombo vya sheria.
Huyo mtu aliyenifanyia jambo hilo hakuwa peke yake.
Nilinyanyaswa nikiwa na umri mdogo na mtu ambaye alikuwa amenipita umri na nilikuwa ninamuamini.
Hata wakati ninatafuta mtu wa kunisaidia sikupata kwa sababu sikuweza kumuamini mtu mwingine tena .
Nimejaribu kupata kitu ambacho kitaonesha kuwa sikuwa mtu mweusi pekee ambaye nilifanyiwa unyanyasaji wakati nikiwa mdogo .
Baada ya kutangaza jambo hilo chuoni, niliambiwa kumuona mtaalamu wa afya azungumze na mimi lakini wanaume wengi ambao walikuwa na tatizo kama la kwangu hawakujitokeza.
Wakati wanaporipoti , wataalamu wanaamini kuwa jambo hilo linatokea katika eneo ambalo lina matatizo.
Ripoti iliyotolewa na chama cha watu wazima waliathirika na unyanyasaji wa kingono inasema waathirika 365 wamesema kile ambacho walikipitia.
Wachache au zaidi ya robo ya watu hao wanasema
Jambo kubwa ambalo linawafanya kutotoa taarifa polisi ni kutokuwaamini.
"Wanaume weusi huwa hatufikirii kuhusu kutoa taarifa polisi ili muhusika aweze kukamatwa'," Kevin alieleza.
Unyanyapaa ni miongoni mwa matatizo yanayotukabili na bila kujua kuwa jamii ya watu weusi watafikiri kuhusu yeye.
"Tumetoka katika utamaduni ambao inakupasa kunyamaza na kukabiliana na jambo hilo mwenyewe", Solse ambaye alifanyiwa unyanyasaji pia .
"Huwezi kuongea kuhusu jambo la namna hiyo kama limekutokea, haswa kuongea na mtu ambaye hajatoka katika familia yenu", alisema mtaalamu.