Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Unyanyasaji kingono ndani ya kanisa katoliki watu waanza kufunguka
Siku moja tu baada ya papa Francis kukiri hadharani kwa mara ya kwanza kwamba makasisi waliwanyanyasa kingono masista na kuahidi kukabiliana na suala hilo ambalo "bado linaendelea" ndani ya Kanisa Katoliki,huku wafuasi wawili wa jinsi ya kike wa zamani wa Kanisa katoliki wamezungumza na BBC kuhusiana na madhila yao.
wakiongea katika kituo cha redio cha Radio 4's Woman's Hour kilichoruka wiki hii nyakati za asubuhi, wanawake hao wawili walipokea kwa moyo mkunjufu ukubalifu wa makosa na kashfa zinazowaandamia makasisi wa kanisa hilo mahalia, huku wakisema kwa muda mrefu kumekuwa na utamaduni wa kukaa kimya na usiri mkubwa ndani ya uongozi.
Ingawa ukubalifu wa ufafanuzi wa uzoefu wao unatazamiwa kuimarisha kashfa inayoendelea kulisumbua Kanisa Katoliki.
.Dk Figueroa ni mwana teolojia na mwalimu huko Auckland, New Zealand, aliyenusurika kuangukia katika mikono ya kasisi mmoja kingono huko Lima, Peru
Aliiambia BBC kuwa alijiunga na jamii ya maisha ya kitume ndani ya kanisa Katoliki akiwa binti mdogo akiwa anaishi katika kitongoji masikini kutokana na hilo ilimlazimu kufanya kitu ili kujikimu.Nilikuwa na umri wa miaka 15 na mwanzilishi aliniomba kuanza uongozi wa kiroho na askofu msaidizi ambaye alikuwa mkurugenzi wangu wa kiroho.
Baada ya miezi kadhaa ya kupata uzoefu na kuongeza imani yangu, alitutaka mimi na baadhi ya vijana wa kiume kuanza kubeba nguo za michezo ili kujifunza mchezo wa yoga, baada ya mazoezi ya vikundi, baadaye aliaanzisha mazoezi ya mmoja mmoja, baadaye akaniambia atanifundisha mazoezi ambayo yatanisaidia kujizua na masuala ya ngono.
"Nilikuwa na ujinga sana, nilikuwa na uzoefu wa kabla ya ngono na hivyo akaanza kunishughulikia kila siku kwa kunishika shika mwili wangu mzima.. Nilikuwa nikifikiria - vibaya - kwamba alikuwa mwema na kwamba mimi ni mwovu.Nilihisi kuwa ni kosa langu na hatia ya kuharibiwa kwangu kabla ikawa ikinisuta.
Askofu huyu hakuwahi kunibaka, lakini kwa namna alivyokuwa akinishika shika , alinifanyia unyanyasaji wa kijinsia kwa namna ya aina yake, Mara ya kwanza kutambua kwamba mimi ni muathirika na vitendo vya unyanyaji kingono ni wakati nilipokuwa na umri wa miaka arobaini.Watu niliowaamini, wale wanaojifanya kumheshimu Mungu, hawakuwa halisi.
Daktari Dr Figueroa , amesema kwamba , aliamua kuzungumza juu ya alichowahi kupitia baada ya mtu aliyefanya unyanyasaji dhidi yake kufa. Alisema alihisi ni muhimu kujitokeza na kuzungumzia masuala hayo na kumshtaki kwa sababu wakati huo alikuwa bado anaonekana kuwa mtu mtakatifu kwa watu na ndani ya jamii yake.
Kabla ya kunyanyaswa kingono nilidhulumiwa kiroho kwasababu sikuruhusiwa kusoma vitabu au kuzungumza na mtu yeyote kuhusu masuala yangu binafsi. Nilipoteza hali ya kujiamini kwangu na kuwa mnyonge sana.
Miaka mitano baadaye, muumini wa kiume wa chama chetu, alianza kunifuata kila wakati ninapotembea peke yangu, anaweza kuja chumbani kwangu na kusimama tu pembeni yangu na kuanza kuongea, "hatimaye atanikumbatia na wakati fulani, alikuja ndani ya chumba changu jioni na kuanza kunivua nguo na kunibaka.
Hali hiyo ilinishtua, nilitambua kilichokuwa kinataka kutokea lakini sikuamini kuwa itakuwa kweli.nilitambua kuwa haikuwa sawa,kwahakika sikutaka hayo yanitokee, Lakini niliamini kabisa; yeye ni kuhani,na hii ni jumuiya takatifu, hii haiwezekani.
Sikuweza kutambua unyanyasaji wa namna hiyo unatekelezwa katika ulimwengu huu kamili ambao nilikuwa nikiishi, Ilichukua miaka mingi kutambua kwamba kile kinachotokea ilikuwa ubakaji na nilikuwa na uwezo wa kuzungumza juu yake.
"baada ya hapo nilikuwa na mgogoro mkubwa wa kiimani: msukumo wangu wa kwanza ilikuwa ni kufikiri kwamba, ikiwa nitasema nitaliharibu Kanisa, kwa hiyo Mungu anataka niwe kimya na sistahili kufumbua kinywa changu kwa yaliyonisibu , ikumbukwe kwamba "Sijaamini katika aina hiyo ya Mungu.
"Hatimaye nilikutana na kuhani mwingine katika jamii niliyoweza kuzungumza naye, na hatua kwa hatua tulipendana, Nilijua kwamba, ikiwa Mungu yupo ... basi amenitumia mtu huyu - mtu ambaye alinipenda. "
Doris Wagner-Reisinger aliacha jamii yake ya dini nchini Ujerumani na akaacha rasmi maisha ya dini mnamo mwaka 2011.