Cyril Ramaphosa - Kiongozi wa Afrika Kusini anayepania kukibakiza madarakani chama cha ANC

Chanzo cha picha, Getty Images
Ni mpenda magari yanayoenda kwa kasi, mvinyo wa bei ghali, ni mvuvi na mkulima - si mwingine ni rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa
Bw. Ramaphosa ni mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa wa kisiaa na kiuchumi na utajiri wake unakadiriwa kuwa kiasi cha dola 450m (£340)
Zaidi ya mwaka mmoja baada ya kuchaguliwa kuwa kiongozi wa chama tawala cha African National Congress (ANC) na kufikia ndoto yake ya kuwa rais wa nchi hiyo.
Bw. Ramaphosa sasa anakabiliwa na kibarua cha kuhakikisha chama hicho kinasalia madarakani katika uchaguzi mkuu wa hapo kesho (Jumatano)
Aliwahi kuwa kiongozi wa chama cha wafanyakazi wa vyama vya ushirika, alikuwa ni alama ya watu weusi katika kukabilina na ubepari kabla ya ANC kuchukua nchi mwaka 1994 na kukomesha utawala wa watu weupe nchini humo.
Biashara haikuwa kipaumbele chake.

Chanzo cha picha, AFP
Chaguo lake la kwanza lilikuwa ni siasa na alikuwa na matarajio ya kuwa makamu wa kwanza wa rais Nelson Mandela, rais wa kwanza mweusi nchini Afrika ya kusini.
Mandela alipomkataa kuwa makamu wake alishikwa na hasira na kuamua kutohudhururia kuapishwa kwa Mandela kama rais wa kwanza nchi hiyo.
Na pia alikataa kuchukua nafasi yoyote ya uongozi serikalini.
Badala yake, Bwana Ramaphosa ambae pia ni mwanasheria - akajikita kuwa mwakilishi na mwenyekiti wa mkutano wa kikatiba, akiwa na jukumu la kuandaa katiba ya Afrika kusini baada ya kupita kipindi cha miaka mingi ya ubaguzi wa rangi.
Ramaphosa aliwashangaza wananchi wengi wa Afrika Kusini ambao walimwona kama mwanasiasa wa kuaminika zaidi wa kizazi cha baada ya Mandela, aliamua kuachana na siasa na kuwa mfanyabiashara.
Wakati huo, haikuwa kawaida kwa watu weusi, kuwa katika sekta ya biashara iliyokuwa inaongozwa na watu weupe.
Mnamo mwaka 1980 aliandaa mgomo mkubwa wa madini katika historia ya Afrika Kusini.
Wafanyabiashara wenye asili ya weupe walijaribu kumtumikia Bwana Ramaphosa ambae alipata hisa katika karibu kila sekta muhimu - kutoka kwa simu na vyombo vya habari (ambako hakuingilia kati katika uhuru wa wahariri wa magazeti ambayo alikuwa nayo) kwa vinywaji na chakula cha haraka alikuwa anaendesha msururu wa hoteli ya Marekani McDonalds nchini Afrika kusini.

Chanzo cha picha, AFP
Vibaraka wa kigeni
Bw Ramaphosa daima aliendelea kukiendeleza chama ANC, akiwa kiongozi mkuu wa kamati ya utendaji ya Taifa - nafasi ambayo, wakosoaji wake wanasema ilimpa habari za ndani na akiwa muhudumu wa serikali alitumia nafasi hiyo ya utawala wake kujijenga kibiashara.
Mashtaka haya yalikuja baada ya polisi kuwaua wachimba mgodi 34 wakiwa kazini mwezi wa Agosti 2012 katika mgodi wa Marikana - likiwa ni tukio baya kuwahi kushuhudiwa tangu kumalizike kwa utawala wa wazungu.
Ramaphosa akiwa ni mkurungezi wa Lonmin - kampuni ya kimataifa inayomilki mgodi huo - alituhumiwa kwa kuwasaliti wafanyakazi ambao kwa wakti mmoja aliwatetea.
Hususan baada ya kuzuka kwa barua pepe zinazomuonyesha kuwa aliitisha hatua kuchukuliwa dhidi ya wachimba mgodi kwa kushiriki katika 'hatua kali za uhalifu' - akimaanisha mgomo uliokumbwana ghasia ulioshuhudia.

Chanzo cha picha, AFP
Japokuwa uchunguzi wa hakimu ulimsafisha Ramaphosa na kesi ya mauaji kiongozi wa chama cha Economic Freedom Fighter (EFF) Julias Malema alimwambia Ramaphosa ni kibaraka wa watu weupe.
"Kila mmiliki wa mgodi ana uhusiano wa karibu na mwanasiasa. Wao [wazunzgu] huwapatia pesa kila mwezi, wanasema ni hisa, Lakini fedha hizo ni ada ya kuwalinda wazungu dhidi ya wafanyikazi weupe ," alisema.
Hata hivyo, Bwana Ramaphosa, ambae anatajwa na jarida la uchumi la Forbes kuwa mmoja wa wafanyabiashara wakubwa mwaka 2014 aliamua kuachana na biashara baada ya kuchaguliwa kuwa makamu wa rais.
Gazeti la kifedha la kimataifa la Forbes, lilimnukuu kwamba, "aliachana na shughuli zake za biashara ili kuepuka migogoro ya riba" baada ya kuwa Naibu wa rais wa Afrika Kusini mwaka 2014.


Chanzo cha picha, AFP
Cyril Ramaphosa ni nani:
- Alizaliwa Soweto, Johannesburg, mwaka 1952
- Mwaka 1974 mpaka 1976 aliwekwa kizuizini kwa shughuli za kupambana na ubaguzi wa rangi.
- Alianzisha muungano wa kitaifa wa wafanyakazi wa migodi 1982
- Mwenyekiti wa kamati ya mapokezi ya taifa yaliyoandaa kumpokea Nelson Mandela kutoka gerezani 1990
- Mbunge na mwenyekiti wa mkutano wa kikatiba wa mwaka 1994
- Mwaka 1997 aliamua kuingilia kikamilifu biashara kwa muda wote na kuwa moja wa matajiri wakubwa nchini Afrika kusini
- Alikuwa Katika bodi ya Lonmin wakati wa mauaji ya wachimba mgodi wa Marikana 2012
- Alichaguliwa kuwa makamu wa raisi wa Afrika kusini 2014
- 2017 alichaguliwa kuwa kiongozi wa chama cha ANC

Ndoto ya Bw. Ramaphosa kuwa rais wa Afrika Kusini ilizimwa na Mzee Nelson Mandela mwaka 1994 baada ya wandani wake katika chama cha ANC, kushawishi amchague Thabo Mbeki kama makamu wake wa raisi.
Wakati huo, Daktari wa zamani wa Bw. Mandela na mfanyibiashara Nthatho Motlana, alisema kuwa Ramaphosa - alikuwa mchanga kisiasa - na kupendekeza aendelee na biashara ili ajiunge na siasa baadae maishani.
Zaidi ya miaka 20 baadae Ramaphosa alifuata mwito huo na hatimae kuwa kiongozi wa ANC.
Hata hivyo bado anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa washirika wa Jacob Zuma ndani ya ANC - na wapiga kura wamechoshwa na kashfa za ufisadi, kukua pole pole kwa uchumi , ukosefu wakazi ambao sasa umefikia 27% na visa vya mara kwa mara vya kupotea kwa nguvu za umeme.

Chanzo cha picha, AFP
Kiongozi huyo wa miaka 66 anajaribu kutafuta mbinu ya kusawazisha matakwa ya wale wanaotaka mabadiliko makubwa kama yale anayoshinikizwa na EFF- na pia kuzingatia maslahii ya jamii ya kibishiara.
Miezi sita baada ya kuapishwa kuwa rais Bw. Ramaphosa alitangaza kuwa katika itafanyiwa marekebisho ili kuiruhusu serikali kutwaa ardhi bila kulipa fidia.
Suala hilo bado linajadiliwa bungeni lakini amejikuta akielezea hatua hiyo itakkuwa wana athari gani na kuongeza kuwa hakutakuwa na visa vya watu kupokonywa ardhi- kama ilivyoshuhudiwa katika taifa jirani la Zimbabwe.
Pia ameaahidi kutokomeza rushwa Afrika Kusini.
"Wale walioiba pesa za umma lazima wafungwe jela" alisema hivyo karibuni.
Wale wanaosubiri hatua dhidi ya rushwa zichukuliwe wanatarajia vita hivyo havitakwama njiani kama ilivyokwama treni iliyokuwa imembeba Bw. Ramaphosa mwezi Februari alipokuwa akielekea kwa mkutano wa kampeini.
Safari ambayo ni ya dakika 45 ilimchukua rais na abiria wengine saa nne.














