Mpigapicha bora wa chakula mwaka 2019: Ulaji wa tambi wapata zawadi bora

Mpigapicha Jianhui Liao ametajwa kuwa ndiye mshindi wa Picha bora ya chakula katika shindano la mwaka 2019

Picha ya Liao (juu),iliyoitwa Sinia la tambi ,inaonyesha sherehe za mungu wa kike Nuwa katika kaunti ya Shexian iliyopo katika jimbo la Hebei nchini Uchina

Kama sehemu ya tukio ambalo si la kawaida la mwaka ,wanavijiji huvaa mavazi ya mawala wa ufalme wa zamani wa kichina kuadhimisha siku ya kuzaliwa wa Nuwa ambapo watu hula tambi zilizopikwa kwenye vyungu majira yta saa sita mchana.

Kiongozi wa Shindano hilo Andy Macdonald alimkabidhi Liao zawadi ya pauni £5,000.

Macdonald alisema kuwa picha hiyo : "Ilikuwa bora kuliko picha nyingine zilizoshindania zawadi hiyo kwa jinsi ambayo [Liao] alivyowezesha kuonyesha umuhimu wa tukio ,ulaji wa jamii, nzuru sana na yenye kuonyesha mandhari .

"Mashindan yalikuwa makali, kulikuwa na picha 9,000 za washiriki kutoka nchiu 77 - idadi hiyo ikiwa ni kubwa zaidi ya washiriki na nchi kuwahi kushuhudiwa miaka ya nyuma na viwango vilikuwa vizuri"

Hizi ni baadhi ya picha zilizochaguliwa miongoni mwa picha zilizoshiriki vitengo vingine:

Zawadi ya Mwanamitindo wa chakula : Caramel Jammy Dodgers, kilichopigwa picha na Kim Morphew, Uingereza

Kim Morphew alikuwa mwanamitindo bora wa chakula kwa kutengeneza biskutiza kutengenezwa nyumbani, ambazo zilipigwa picha na Martin Poole.

Leta nyumbani mavuno: Harvesting Gold, iliyopigwa picha na Kazi Mushfiq, Bangladesh

Kazi Mushfiq: "Wakulima walikuwa wakifanya kwa bidii kuvuna mbunga, ambao ni kama dhahabu kwao."

Picha ya Marks & Spencer: Tarte Tatin with Thyme, iliyopigwa na Nick Millward, Uingereza

Nick Millward: "Aina rahisi ya mkate wa pai ulioongezewa kiongo cha ziada na unga mzito kidogo na mpishi Clodagh McKenna."

Siasa ya Chakula: Cow Tantrum, mtindo iliyoandaliwa na Martin Chamberlain, Uingereza

Martin Chamberlain: "Ng'ombe huyu huenda alifahamu hatma yake. baada ya kuletwa tu kutoka sokoni katika eneo la Nizwa, Oman, alithibitisha kuwa hakutaka kukubaliana na ' matwakwa ya mmiliki mpya - matokeo yake akaangusha migfuu yake ya mbele, na kuwaacha wamiliki wake wakiwaza ni nini la kufanya ."

Awali Production Paradise ilichapisha: Papa mwekundu, cha Cosimo Barletta, kutoka Italy

Cosimo Barletta: "Wakati unapo 'muweka shetani wa baharini ' mezani ... hujui ni nini kitakachotokea !"

Chakula cha Sale: Ramadan, kilichoandaliwa na Elise Humphrey, kutoka Uingereza

Elise Humphrey: "Mmiliki wa soko la njaa la Yogyakarta, Indonesia, ni miongoni mwa matunda yanayozuiwa kuliwa wakati wa Ramadhan ", huku akiota juu ya vyakula vingine

kitengo cha wanablogi wa Chakula : tambi zilizokaushwa cha Aimee Twigger, kutoka Uingereza

Aimee Twigger: "Tambi zilizochanganywa na majani ya dawa za mitishamba zikikaushwa kwenye dirisha."

Mwanafunzi wa Upigaji Picha picha za Chakula : Tuzo liliwaendea The Carnal Supper, na mpigapicha Chloe Dann, Kutoka Australia

Chloe Dann: "Picha hii ni kutoka katika msururu wa maonyesho ya sanaa juu ya tabia ya ulaji wa binadamu na namna tabia hiyo inavyohusiana na asili na utamaduni ."

Tuzo ya Fujifilm Award la Ubunifu : Ilikwenda kwa Broken Egg, iliyochukuliwa na mpigapicha Michael Hedge, kutoka Uingereza

Michael Hedge: " Picha hii ni sehemu ya msururu wa picha nilizopiga kwa ajili ya Jarida linaloelezea uhusiano baina ya chakula , kilimo na maeneo ya vijijini

Chakula cha Familia : Kabila la Bonda , picha iliyoipigwa na Sanghamitra Sarkar, kutoka India

Sanghamitra Sarkar: " Eneo la Odisha, nchini India, linakaliwa na jamii zenye makabila mbali mbali na kabila la Bonda ni miongoni mwake. Wanaishi maisha rahisi sana . jamii ya kisasa imeshindwa kubadili maisha yao kwasababu wanalinda utamaduni wao kwa makini sana na kuukinga usiingiliwe na tamaduni za kisasa

" Katika picha hii wasichana wa kabila la Bonda wanatengenea chakula chao katika vyungu na kufikicha moto kutoka kwenye miti."

Chakula cha watoto wenye umri wa miaka 10 & Chini: Mapenzi ya tunda la kara kara (passion), picha na Joshua George, kutoka Bahrain

Joshua George: "Kuwa na tunda la kara kara moja kwa moja kutoka kwenye mmea ilikuwa na ladha na raha ."

Unaweza pia kutizama:

Picha zote zilipigwa na Pink Lady Mpiga picha wa Chakula wa mwaka 2019.